Mawazo kwa wasanii wa filamu: Tumieni mbuga zetu/ Wanyama wetu biashara zenu zitapata pesa sana

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Biashara ya filamu imeenda chini sana kuanzia enzi za Kanumba kwasababu hakuna ubunifu. Mimi kama diaspora nimefanya uchunguzi kujua kwanini hii inatokea. filamu zetu zinaiga na kujaribu kushindana na Nigeria lakini Tanzania tuna kitu kimoja ambacho wenyewe hawana. Sijawahi kuona picha kutoka kwa wasanii wetu kuhusu wanyama, mbuga au namna yeyote kwa kutumia mbuga zetu. Hakuna ubunifu kabisa. Wazungu wengi wanapenda sana wanyama lakini movie hakuna movie. Wasanii wangeweza kutengeneza picha za watoto, vichekesho, elimu kwa wanyama n.k. Wanyama wengi tulionao wako sehemu chache sana Duniani. Hii ni sehemu ambayo wasanii wanaangaika wakati kuna watu wengi sana Duniani wanatafuta ubunifu kwenye mbuga na wanyama wetu.
 
No creativity at all
They're terrible. So terrible that I've considered quitting a certain program featuring them.
Those in charge please get it fixed.
 
Back
Top Bottom