nelvine
JF-Expert Member
- Nov 8, 2015
- 1,109
- 1,855
- Thread starter
- #21
Asante sana mkuu, wengi hawajui mazingira ninayowakuta hawa mabinti.Unajua mambo mengine kwenye forum unaweza kukosoa bila kujua hali halisi. Wasichana kama hao unaosema wengi unakuta wametoka familia maskini sana na huko walikukuwa walikuwa wanaishi kwenye mazingira magumu. Hata kama sheria inazuia kuajiri watoto wa umri huu lakini kiuhalisia wasipoajiriwa wataishia kubebeshwa mimba au kuolewa huko kwao na maisha kuwa mabaya zaidi. Mimi nadhani serikali inatakiwa kuangalia haya mambo kwa uhalisia wake. Mimi nakushauri ufanye hii shughuli kwa kuzingatia haki na uhakikishe unasimamia haki za hao wasichana kwani waajiri wengine wanaweza kuwatumikisha kama watumwa.
80% wengi wanakimbia ndoa, maana nna binti aliolewa akiwa na miaka 12, na ana mtoto.
98% hawa mabinti hata darasa la kwanza hawalijui.
90% mabinti wamekoswa koswa kuozeshwa kwa lazima na wazazi/walezi wao.
Hivyo kwa mazingira niyaonayo na wao kunisumbua kuhitaji kazi nimeona ni heri niwasaidie kwa njia hii niwe wakala wao hila nitawasimamia katika kupata haki zao wakiwa kwa maboss zao. Naamini kufanya hivi nitakuwa nimewasaidia hata angalau kujitambua na kupata ujuzi kidogo kuliko kuwaacha hivyo hivyo.