Mawazo kama haya ya watawala ni hatari kwa maendelo ya nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo kama haya ya watawala ni hatari kwa maendelo ya nchi yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bemg, Jul 26, 2012.

 1. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Pinda aliitisha kikao hicho ili wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini waache kuishinikiza serikali kumwajibisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, ambaye anatuhumiwa kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma katika kutoa zabuni ya ununuzi wa mafuta mazito ya kuzalishia umeme wa dharura katika kwa kampuni ya Puma ambayo ilipewa vibali vya kuiuzia serikali mafuta lita milioni tisa kwa mwaka 2011 na lita milioni tisa kwa mwaka huu.

  Kibali cha kwanza kilitolewa Septemba 28, mwaka jana, huku kingine kikitolewa kwa utaratibu huo huo wa kutofuata Sheria ya Manunuzi ya Umma Julai 12, mwaka huu kwa ajili ya kuuza lita milioni tisa.

  Habari kutoa ndani ya kikao hicho zinasema kuwa, Waziri Mkuu, aliwaambia wabunge hao kuendelea kushikilia uamuzi huo wa kutaka waliohusika na sakata hilo kujiuzulu kutaiathiri serikali kwa kuwa ni muda mfupi kumefanyika mabadiliko katika Baraza la Mawaziri.

  Chanzo chetu kilisema Pinda aliwaambia wabunge hao kuwa, kitendo cha kushinikiza mawaziri kujiuzulu kinaweza kuitia aibu serikali kwa mara nyingine.


  Nipashe.

  Hivi ccm kitaacha lini kuwafumbia macho watendaji wabovu wanaotuibia waziwazi na kuingiza nchi kwenye hasara?
   
Loading...