Mawazo haya yamechangiwa na nini Kikwete?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Kwangu mimi na ninaamini kwa watu wengi wanaoitakia nchi yetu maendeleo ya haraka, ni wazo mwanana,lisilo na ubishi, kwamba kwa mikoa iliyoko pembezoni mwa nchi yetu,jawabu la kuwafanya wafanyakazi wapende kufanya kazi huko, ni kuwapo posho za ziada.Haijalisi posho hizo zinapewa majina gani,la msingi ni kwamba wafanyakazi wapende kwenda huko.
Kilichonishangazi ni pale kiongozi wa juu kabisa serikalini,yaani Raisi Kikwete alipopinga wazo hilo, kwasababu kwa mawazo yake, kuwapa posho hizo ni kuwatishia zaidi,na kwamba hiyo inaweza ikawafanya wasiende huko.Ninakubali kwamba si wote watakao shawishika na posho hizo,lakini pia nakataa kwamba posho hizo zitawatisha. Ninaamini kwamba asilimia kubwa watashawishika kwenda kwa ajili ya posho hizo.Ikumbukwe kwamba, watanzania tulio wengi, tunafanya kazi si kwa kuzipenda,lakini kwasababu ya dhiki tulizo nazo.Watakao kataa kwenda ni wale tu wenye watu wakuwakingia vifua,ambao wana uhakika wa kupata kazi sehemu nyingine nzuri.Vinginevyo wengi wa wafanyakazi nikiwemo mimi binafsi, kama posho zitakuwa nzuri nitakwenda, ili niweze kuilisha familia yangu.Hakuna faida yeyote kufanya kazi kwenye mazingira magumu huku ukipata malipo sawa na mtu aliyeko Dar es Salaam.Taasisi zisizo za kiserikali,wabunge na hata mikoa iliyoko pembezoni mwa nchi yetu wameishauri serikali ifikirie swala hilo.Hata mikoa kama Rukwa kwa kiasi fulani imeshaanza kutekeleza wazo hilo.tamko la Kikwete lina turudisha nyuma, na wala haliitakii nchi yetu mema.
 
Back
Top Bottom