Mawaziri wote ni mizigo... isipokuwa wawili

Mkuu hii thread imeanza Jana usiku Na kulikuwa na wachangiaji wengine zaidi lakini Leo naiona vipande!
Nakuomba Mkuu invisible angalia suala hili kwa undani Na siku moja niliweka thread ikayeyuka!

blueray unajua hata mimi post zangu kuna mda zinapotea tu! Halafu sielewi kwanini? Imetokea kama mara 4 hivi. Kumbe siko mwenyewe.
 
Kwa maana hiyo inabidi serikali iache kununua mashangingi, na badala yake yatafutwe mafuso ya kutosha kuhamisha hii mizigo. Ningeshauri treni zitumike lakini reli zetu ndo hozo tena.
 
hata magufuli ni mzigo, ikulu pia ni mzigo,

Mkuu si kwamba namshabikia Magufuli lakini kusema ukweli ukimlinganisha na wengine angalau yeye na Mwakyembe they twinkle out of faint stars.
 
Kwa maana hiyo inabidi serikali iache kununua mashangingi, na badala yake yatafutwe mafuso ya kutosha kuhamisha hii mizigo. Ningeshauri treni zitumike lakini reli zetu ndo hozo tena.

Hah hah hah hah hah, labda JK atapeleka semi trailer kuwaondoa!
 
blueray unajua hata mimi post zangu kuna mda zinapotea tu! Halafu sielewi kwanini? Imetokea kama mara 4 hivi. Kumbe siko mwenyewe.

Kuna siku Niliambiwa kuna Watu wamepandikizwa JK kushughulikia thread ambazo hazina mwelekeo!

Ninavyojua jf kuna sheria au maadili ambayo ndio member tunapaswa kuzingatia lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine thread zingine zinayeyushwa wala bila kuvunja maadili ya jf
 
Pamoja Na kwamba CCM imeamua kutosa mawaziri 7 lakini ukwei ni kwamba mawaziri wote ni mizigo kwa wananchi wakiongozwa Na mzigo namba 1 Mtoto Wa mkukima aka liwalo Na liwe.

Ni mawaziri wawili tu ambao mtu anaweza kusimama Na kujenga hoja kwamba wanachapa kazi. Hawa ni Magufuli Na mwakyembe.
Nashauri rais wetu JK futa baraza lote la mawaziri Na uunde baraza dogo lenye tija ili utupunguzie mzigo wananchi wako.

Subiri bwagizo la maneno matamu matamu, wakati anaunganisha magarasha kama ilivyo kawaida yao
 
Fanya uchunguzi zaidi, hao wawili unaowana pengine ndo mizigo mizito zaidi...in short Mawaziri wote wa JK ni mizigo isiyobebeka...
 
Kwa upande mwingine nakubaliana Na wewe, mi nilisema tu angalau wenye unafuu. Ila kweli baraza la awamu hii, kweli ni mzigo!

Ndio maana hajatokea mtuu wa angalau kuja hapa Na kutetea labda kwamba wanaonewa!

Inaelekea Watu wengi tunakubaliana mawaziri Wa JK ni mzigo
 
Yaani mizgo kweli kweli,nambari moja Kikwete mwenyewe. Na ikumbukwa rais ndiye alitakiwa aondolewe kwa kushndwa kujitambua na mawaziri wake. Hata mm nimekataa kumwita rais wangu huyu jamaa kama vp ning'oeni kucha,meno na macho na ninyi hukumu yenu siku ikifika kama ya yule wa jana huko MWANZA mabina mnamwita sijui.
 
LUKUVI na WASSIRA sio mzigo kwa Serikali. Wanachapa kazi vizuri.

Duh Mkuu, Lukuvi Na Wasira!

Hawa jamaa wanachapa kazi za kampeni za CCM ndani ya serikali, Hawa ndio hawafai kabisa kwa taifa hili wanagawa nchi kwa matabaka ya vyama!
 
Pamoja Na kwamba CCM imeamua kutosa mawaziri 7 lakini ukwei ni kwamba mawaziri wote ni mizigo kwa wananchi wakiongozwa Na mzigo namba 1 Mtoto Wa mkukima aka liwalo Na liwe.

Ni mawaziri wawili tu ambao mtu anaweza kusimama Na kujenga hoja kwamba wanachapa kazi. Hawa ni Magufuli Na mwakyembe.

Nashauri rais wetu JK futa baraza lote la mawaziri Na uunde baraza dogo lenye tija ili utupunguzie mzigo wananchi wako.
Katika mizigo namba 1 ni pamoja na mMagufuli aliyeweza kutumia sheria feki za barabara kwa miaka 13 kiasi cha kuwasababishia vifao watu kutokana na magonjwa yanayohusiana na mshituko wa damu, moya n.k. Hivi karibuni tarehe 31 Mei 2013 Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi ilitamka kuwa ardhi yote anayodai ni hifadhi za barabara ni mali ya wanavijiji kutokana na yeye kutumia sheria batili.

Nasikitika haukuambatanisha ushaihidi wowote katika hoja yako mimi naambatanisha hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi. Nakushauri wewe na wenzako wavivu wa kusoma na ambao huamini kauli za mdomoni mtumie muda kidogo kusoma hukumu hiyo ndio mtambue huyo mtu wenu ni dikteta wa kiasi gani.

Kutokana na ubabe wake amewavunjia malaki ya watanzania haki zao za kikatiba hususan haki za makazi kwa mujibu wa Tamko la Kimataifa la haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights) lililopitishwa tarehe 10 Desemba 1948, sambamba na sheria zake za barabara za kikoloni.

Aidha amewavunjia malaki ya watanzania haki zao za kikatiba kwa mujibu wa ibara 24 ya Katiba ya Tanzania ya kumiliki mali na kutokunyang'anywa wa la kutaifishiwa mali yako. Huku ni kukiuka kiapo alichokula cha kuilinda Katiba ya nchi.
 
Attachments

  • Road Reserve Land Case Judgement.pdf
    2.1 MB · Views: 39
hata magufuli ni mzigo, ikulu pia ni mzigo,

magufuli anajificha chini ya mwavuli wa mdomo lakini analitia taifa hili hasara kubwa kwa mradi wa mabasi yanayokwenda haraka. Ile barabara ni ya gharama kubwa mno na tija yake itakua ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa jiji ulivyo. Angemshauri rais lile fungu lijenge barabara nyingne mbadala,mf.toka tegeta mpaka mbagala ,kisarawe kwnd kibaha,bugurun kwnda kigogo,external kwnda kisukulu,yombo kwnda kitunda,barabara inayoambaa na reli kuanzia vingunguti mpaka pugu n.k.
Bila shaka ule mradi una 10% kubwa.
 
ule mradi sio wa 10%, magufuli na co wote wameramba 70%, ukijumlisha na hela ya consultant 12% the rest 18% ndo inafanya kazi ya kuwalipa mafundi na materials
 
Mkuu mi nilifikiri ana unafuu kidogo ukilinganisha Na mawaziri wengine. lakini Kumbe udhaifu wake umejificha kwenye makelele yake huku akitoa maamuzi ya kuvunja sheria za nchi Na kuingia mikataba ya kujinufaisha binafsi!

Kwa sababu hii Na hoja nyingi zinazotolewa dhidi yake inaonyesha hata yeye ni mzigo Na ni hatari pia
 
ule mradi sio wa 10%, magufuli na co wote wameramba 70%, ukijumlisha na hela ya consultant 12% the rest 18% ndo inafanya kazi ya kuwalipa mafundi na materials

Kama hali ndiyo hii basi hatuna kabisa viongozi wa wananchi. Tuna mawaziri ambao ni wachumia tumbo!
 
magufuli anajificha chini ya mwavuli wa mdomo lakini analitia taifa hili hasara kubwa kwa mradi wa mabasi yanayokwenda haraka. Ile barabara ni ya gharama kubwa mno na tija yake itakua ndogo sana ukilinganisha na ukubwa wa jiji ulivyo. Angemshauri rais lile fungu lijenge barabara nyingne mbadala,mf.toka tegeta mpaka mbagala ,kisarawe kwnd kibaha,bugurun kwnda kigogo,external kwnda kisukulu,yombo kwnda kitunda,barabara inayoambaa na reli kuanzia vingunguti mpaka pugu n.k.
Bila shaka ule mradi una 10% kubwa.

Kama huu mradi nao ni wa kifisadi basi watanzania katika huu Utawala Wa JK tumekwisha!
 
Back
Top Bottom