Mawaziri wenye tamaa ya urais ni kikwazo kwa Rais Samia

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
709
2,858
Gazeti la mwananchi limekuja na report inayofafanua vizuri jinsi mawaziri wenye tamaa wanavyoweza kumvuruga rais aliyepo madarakani kwa kujijenga wao binafsi badala ya kumsaidia rais kutumikia wananchi.

=======

Tuanze hapa; kuna tofauti kubwa kati ya ndoto na tamaa. Mwenye kuota huwa na subira, huamini wakati wake sahihi utafika. Aliyejawa tamaa, huona zamu yake inachelewa.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 2022, yapo majina mawili yanatawala; Raila Odinga na William Ruto. Kuna mmoja ana ndoto, mwingine ni mwenye tamaa kubwa. Nitafafanua!

Raila ana ndoto, ndio maana mwaka hadi mwaka anagombea urais, anashindwa, lakini anabaki na subira. Ruto ana tamaa. Ikawa sababu ya kutoelewana na Rais Uhuru Kenyatta, kisa ukaribu wake na Raila.

Uhuru na Raila walipofanya maridhiano na kufanikisha Mpango wa Ujenzi wa Daraja (BBI), kwa ajili ya kuzika uhasama wa kisiasa, Ruto akakasirika. Akaona Uhuru anataka kumbeba Raila kwenye uchaguzi ujao Kenya.

Wakati Uhuru alikuwa akijitetea kuwa ukaribu wake na Raila sio wa kisiasa, bali ni kwa masilahi ya Kenya na Wakenya. Ruto hakuelewa maelezo hayo. Ni kwa sababu fikra zake zilikuwa zinawaza urais kuliko chochote.

Hapo ndipo kwenye elimu ya msingi; kwamba mtu mwenye tamaa ya urais, hata akiwa sehemu ya Serikali yenye Rais mwingine, hufanya mambo kwa ajili ya kujisafishia njia kwenda Ikulu kuliko kuitumikia nchi inavyopasa.

Huu ndio ujumbe ambao nimekusudia kumfikishia Rais Samia Suluhu Hassan. Ndani ya Serikali anayoiongoza, Baraza la Mawaziri, anaweza kuwa na maadui, ingawa hawatajipambanua mbele yake. Inawezekana akawaamini lakini watamwangusha.

Rais Samia anatakiwa kuwabaini mawaziri wenye tamaa ya urais na kuwaweka kando, kisha ajitenge nao kabisa. Hawatamsaidia yeye kama rais na taifa, bali siku zote itakuwa kujionesha ili kujisafishia njia ya kushika mpini.

Akumbuke jinsi watu walivyoshughulikiana nyakati za mwisho wa urais wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi, vita ikawa kubwa kuelekea kumrithi Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, vivyo hivyo wakati wa kumpokea kijiti Rais wa Nne, Jakaya Kikwete.

Hili sio la Tanzania tu, mfano upo kwa Uhuru na Ruto, hawaelewani. Rais wa Pili wa kidemokrasia Afrika Kusini, Thabo Mbeki, alivurugana na Makamu wake, Jacob Zuma. Mbeki Rais, halafu kuna msaidizi wake anautaka urais, pakachimbika. Mbeki akalazimishwa kujiuzulu. Zuma akaingia.

Rais akiwa na msaidizi mwenye tamaa ya urais, hawezi kuwa na uaminifu wa kuitetea serikali. Machoni kwa rais anaweza kutoa kila aina ya sifa, pembeni atamponda kiongozi wake kwamba hawezi kazi.

Kipo kiburi hujengeka kwa mwenye kuusaka urais. Hujiona yeye ndiye anayeweza kazi kuliko hata aliyepo madarakani. Na kwa kawaida huwezi kumwongoza mtu anayejiona ana uwezo mkubwa kuliko wewe.

Suala la rais kufanya kazi na wapinzani wake ndani ya Serikali anayoiongoza, lipo pia kwenye kitabu cha “Team of Rivals: The Political Genius of Abraham Lincoln” – “Timu ya Wapinzani: Maarifa ya Kisiasa ya Abraham Lincoln.”

Mwanahistoria wa Marekani, Doris Kearns Goodwin, kupitia kitabu hicho, aliandika kuhusu serikali iliyoundwa na Rais wa 16 wa nchi hiyo, Abraham Lincoln, kwamba alifanya kazi na watu ambao walikuwa na ndoto ya kupata urais.

Washindani wa Lincoln wa kisiasa ambao walikuwepo kwenye Baraza la Mawaziri aliloliunda ni Waziri wa Fedha, Salmon Chase, Waziri wa Mambo ya Nje, William Seward, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edward Bates. Hao ni kuwataja kwa uchache.

Shida kubwa kwa mawaziri wenye uchu ya urais ni kutengeneza makundi. Utakuta mpaka Serikali inapita vipindi vyenye joto kali, kisa makundi ya wasaka madaraka. Rais Samia akitaka uongozi wake usipitie joto hilo, ajitenge na asiwape nafasi wote wenye tamaa ya urais. Waliopo awatoe.

Urais hauji kwa nguvu

Uongozi huletwa na Mungu, japo jitihada hazikatazwi. Samia hakuwahi hata kujitokeza kugombea urais, lakini leo ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Alipewa nafasi kwa kuwa mgombea mwenza, akawa Makamu wa Rais, kisha ikampendeza Mungu kumtwaa Rais John Magufuli.

Mwinyi (baba) na hata mwanawe, Hussein Mwinyi, hawakuwahi kujipambanua popote kutaka urais, lakini utulivu wao uliwezesha kupendekezwa. Hata Mkapa, hakupata kujionesha mwenye tamaa ya urais, lakini muda ulipofika aligombea na kupata. Kadhalika, Magufuli.

Kikwete, mwaka 1995, hakutaka kujitokeza kugombea urais. Alitaka kutulia na uwaziri.

Chanzo: Mwananchi
 
Siyo kweli, na hakuna ubaya wowote mtu kuutamani Urais! Naona mnatamani zirudi zile zama za kusikiliza simu private za watu, utawala wa kishamba TZ umeenda na aliyeenda!

Mkapa alikaa na JK miaka 10 kama waziri wake huku akijua dhamira ya JK ni nini katika Urais na hilo halikumsumbua hata kidogo!

Awamu hii kila mtu ataonesha kipaji chake na hakuna atayebanwa...No udikteta wakishamba tena TZ
 
Hakuna kosa lolote mtu kuutamani urais na kujipanga. Hata Hangaya mwenyewe alikuwa anautamani huoni sasa kaanza kutangaza mapema kuwa atagombea? Mimi mwenyewe nautamani
 
Rais SSH ameziba masikio, mwacheni awashikilie kina Mwigulu Nchemba wampeleke shimoni kabisa.

Nchi hii imefikia Police wanateka Makomandoo Wa Jeshi na kuwatesa. Jeshi liko wapi? Police hawajui mipaka yao? Mawaziri husika wako wapi?
 
Vyovyote vile unavyoweza kuita, bali ndoto ama dira ndiyo huweza kujenga dhamira ama dhima ya mtu kufanikisha kufanya jambo lolote lile la kimkakati.

Tamaa ama hamu hujengwa kupitia "risk appetite" ya mtu kuweza kufanikisha lengo la mtu. Tamaa hizi ni lazima zichukuliwe kwa tahadhari kubwa ili kukwepa kupoteza ama kupotezwa uelekeo.

Tamaa ya kufanya jambo lolote lile kwa nia njema si kosa wala dhambi. Tunapata mfano wa hitaji la kila mtu pale anapotamani ama kuwa na ndoto ya siku moja aweze kufika mbinguni kwa Mola wake. Matayarisho ya kuweza kufika huko huanza ndoto na kisha hatimaye kuthibitishwa na matendo. Binadamu aliyezaliwa na mwanamke inampasa kwanza aishi maisha ya kimwili ya uchaji Mungu, aweze kufa (mwili utengane na roho) na hatimaye aweze kwenda kwenye maisha ya kiroho mbinguni.

Tunaweza kujifunza kitu kwa kuiangalia nadharia ya Maslow juu mahitaji mtu yanayojengeka kupitia udadisi, uchu na hamasa iliyopo ndani ya mtu. Nadharia hii huangalia uchu na hamaniko la mahitaji katika mpangilio wa ngazi tano mfano wa umbo la piramidi.

Katika mpangilio huo, toka chini kwenda juu mahitaji huwa mpangilio ufuatao;
1) Hitaji la chini la kila mtu hutokana na maumbile yake kibinadamu mf. tamaa ya chakula na mavazi
2) Hitaji la pili baada kupata hakikisho ya lile kwanza hufuatia tamaa ya usalama mf. kazi, malazi, matibabu
3) Hitaji linalofuatia baada ya hakikisho juu ya lile la kwanza na pili huja hitaji la upendo na mahusiano na watu wengine
4) Baada ya hayo ya awali kupata hakikisho basi huja uchu ama hitaji la kujijengea heshima mbele ya jamii.
5) Uchu ama hitaji la juu kabisa la mtu ni lile la kutaka kujipambanua ili kufanikisha lengo maalum na kuweka alama ya kipekee katika maisha ya mtu mf. kuwa Rais wa nchi

Kwa hiyo basi ili mtu afanikishe ndoto yake ni lazima awe na tamaa ya kufanikisha ndoto hiyo kupitia hakikisho la mahitaji yake ya msingi. Tamaa ya kupata kitu kizuri kupitia njia nzuri si kosa, ila kinyume chake ndiyo kosa.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Gazeti la mwananchi limekuja na report inayofafanua vizuri jinsi mawaziri wenye tamaa wanavyoweza kumvuruga rais aliyepo madarakani kwa kujijenga wao binafsi badala ya kumsaidia rais kutumikia wananchi.

=======

Tuanze hapa; kuna tofauti kubwa kati ya ndoto na tamaa. Mwenye kuota huwa na subira, huamini wakati wake sahihi utafika. Aliyejawa tamaa, huona zamu yake inachelewa.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 2022, yapo majina mawili yanatawala; Raila Odinga na William Ruto. Kuna mmoja ana ndoto, mwingine ni mwenye tamaa kubwa. Nitafafanua!

Raila ana ndoto, ndio maana mwaka hadi mwaka anagombea urais, anashindwa, lakini anabaki na subira. Ruto ana tamaa. Ikawa sababu ya kutoelewana na Rais Uhuru Kenyatta, kisa ukaribu wake na Raila.

Uhuru na Raila walipofanya maridhiano na kufanikisha Mpango wa Ujenzi wa Daraja (BBI), kwa ajili ya kuzika uhasama wa kisiasa, Ruto akakasirika. Akaona Uhuru anataka kumbeba Raila kwenye uchaguzi ujao Kenya.

Wakati Uhuru alikuwa akijitetea kuwa ukaribu wake na Raila sio wa kisiasa, bali ni kwa masilahi ya Kenya na Wakenya. Ruto hakuelewa maelezo hayo. Ni kwa sababu fikra zake zilikuwa zinawaza urais kuliko chochote.

Hapo ndipo kwenye elimu ya msingi; kwamba mtu mwenye tamaa ya urais, hata akiwa sehemu ya Serikali yenye Rais mwingine, hufanya mambo kwa ajili ya kujisafishia njia kwenda Ikulu kuliko kuitumikia nchi inavyopasa.

Huu ndio ujumbe ambao nimekusudia kumfikishia Rais Samia Suluhu Hassan. Ndani ya Serikali anayoiongoza, Baraza la Mawaziri, anaweza kuwa na maadui, ingawa hawatajipambanua mbele yake. Inawezekana akawaamini lakini watamwangusha.

Rais Samia anatakiwa kuwabaini mawaziri wenye tamaa ya urais na kuwaweka kando, kisha ajitenge nao kabisa. Hawatamsaidia yeye kama rais na taifa, bali siku zote itakuwa kujionesha ili kujisafishia njia ya kushika mpini.

Akumbuke jinsi watu walivyoshughulikiana nyakati za mwisho wa urais wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi, vita ikawa kubwa kuelekea kumrithi Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, vivyo hivyo wakati wa kumpokea kijiti Rais wa Nne, Jakaya Kikwete.

Hili sio la Tanzania tu, mfano upo kwa Uhuru na Ruto, hawaelewani. Rais wa Pili wa kidemokrasia Afrika Kusini, Thabo Mbeki, alivurugana na Makamu wake, Jacob Zuma. Mbeki Rais, halafu kuna msaidizi wake anautaka urais, pakachimbika. Mbeki akalazimishwa kujiuzulu. Zuma akaingia.

Rais akiwa na msaidizi mwenye tamaa ya urais, hawezi kuwa na uaminifu wa kuitetea serikali. Machoni kwa rais anaweza kutoa kila aina ya sifa, pembeni atamponda kiongozi wake kwamba hawezi kazi.

Kipo kiburi hujengeka kwa mwenye kuusaka urais. Hujiona yeye ndiye anayeweza kazi kuliko hata aliyepo madarakani. Na kwa kawaida huwezi kumwongoza mtu anayejiona ana uwezo mkubwa kuliko wewe.

Suala la rais kufanya kazi na wapinzani wake ndani ya Serikali anayoiongoza, lipo pia kwenye kitabu cha “Team of Rivals: The Political Genius of Abraham Lincoln” – “Timu ya Wapinzani: Maarifa ya Kisiasa ya Abraham Lincoln.”

Mwanahistoria wa Marekani, Doris Kearns Goodwin, kupitia kitabu hicho, aliandika kuhusu serikali iliyoundwa na Rais wa 16 wa nchi hiyo, Abraham Lincoln, kwamba alifanya kazi na watu ambao walikuwa na ndoto ya kupata urais.

Washindani wa Lincoln wa kisiasa ambao walikuwepo kwenye Baraza la Mawaziri aliloliunda ni Waziri wa Fedha, Salmon Chase, Waziri wa Mambo ya Nje, William Seward, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edward Bates. Hao ni kuwataja kwa uchache.

Shida kubwa kwa mawaziri wenye uchu ya urais ni kutengeneza makundi. Utakuta mpaka Serikali inapita vipindi vyenye joto kali, kisa makundi ya wasaka madaraka. Rais Samia akitaka uongozi wake usipitie joto hilo, ajitenge na asiwape nafasi wote wenye tamaa ya urais. Waliopo awatoe.

Urais hauji kwa nguvu

Uongozi huletwa na Mungu, japo jitihada hazikatazwi. Samia hakuwahi hata kujitokeza kugombea urais, lakini leo ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Alipewa nafasi kwa kuwa mgombea mwenza, akawa Makamu wa Rais, kisha ikampendeza Mungu kumtwaa Rais John Magufuli.

Mwinyi (baba) na hata mwanawe, Hussein Mwinyi, hawakuwahi kujipambanua popote kutaka urais, lakini utulivu wao uliwezesha kupendekezwa. Hata Mkapa, hakupata kujionesha mwenye tamaa ya urais, lakini muda ulipofika aligombea na kupata. Kadhalika, Magufuli.

Kikwete, mwaka 1995, hakutaka kujitokeza kugombea urais. Alitaka kutulia na uwaziri.

Chanzo: Mwananchi
ACHENI maneno, hata mie nitagombea 2025,na ccm kwisha habari yake
 
Sijapiga chochote ila mzunguko wa fedha na ajira zilikuwa bwelelee
Mungu ambakiriki Mzee wetu Jakaya.

Jakaya alitengeneza bomu sio ajira... kwa sababu 95% ya ajira zote serikalin zilikuwa za . Waalimu wa msingi sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Kwamba ukuaji wa sekta Ya elimu haukuendana na ukuaji wa uchumi jambo linalopelekea tatizo kubwa la ajira hv sasa ambalo ndilo BOMU linalosubiri kulipuka.
KAWAUZIA KESI WENZAKE
 
Back
Top Bottom