Mawaziri wawili wajiuzuru uganda, kwanini tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wawili wajiuzuru uganda, kwanini tanzania?

Discussion in 'International Forum' started by bampami, Feb 17, 2012.

 1. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,854
  Likes Received: 1,297
  Trophy Points: 280
  Mawaziri wawili ambao
  waliamuliwa kuwajibika
  nakuisababbishia serikali
  hasara ya dola milioni 60,
  kutokana na malipo ya
  kufidia mfanya biashara baada ya kupoteza umilikaji
  wa soko kadhaa mjini
  Kampala,wamejiuzulu.Hii
  inatokana na mapendekezo
  ya tume iliyochunguza
  matumizi ya mali ya Umma. Aliekuwa waziri aliehusika
  na masuala ya jinsia pamoja
  na waziri mwingine katika
  ofisi ya waziri mkuu Kiddu
  Makubuya si mawaziri tena.
  Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Genarali
  Moses Ali kabla ya mjadala
  ulioanza kwa agenda kuhusu
  wahusika hao wawili
  kuendelea. Generali Ali
  alisoma taarifa ya serikali kuhusu mapendekezo ya
  kamati ya bunge na kueleza
  kuwa wahusika wamekubali
  kuwajibika kisiasa, na
  kukubali kuwa walikosa na
  hivyo wakajiuzulu. Bw.Khiddu Makubuya
  amesema kuwa kutokana na
  hayo anachukua uwamuzi
  wa kujiuzulu wadhifa wake
  kama waziri wa masuala ya
  jumla katika ofisi ya waziri mkuu. Lakini mwenzake Syda
  Bumba aliekuwa waziri
  anayehusika na masuala ya
  jinsia licha ya kukubali
  kuwajibika kisiasa lakini
  anadai kuwa hana hatia kwa sababu aliyoyatenda alikuwa
  akifuata sheria ya kutekeleza
  mapendekezo ya
  mwanasheria mkuu. Haya yote yamesababishwa
  na uchunguzi ulionza mwaka
  uliopita ambapo tume ya
  bunge ilikuwa ikichunguza
  hasara ya dola million 60
  zilizopewa mfanya biashara Basajjabalaba ikiwa ni fidia
  kwake baada ya hasara
  aliyopata kutokana na
  kupoteza tenda ya masoko
  ya mjini Kampala. Mfanya biashara huyo
  alipoteza Tenda ya kumiliki
  masoko hayo baada ya Rais
  kuamua kuwa masoko yote
  yasimamiwe na wananchi wa
  kawaida walio katika masoko hayo. Kwa sababu hizo uwamuzi
  ulipitishwa Bw.Hassan
  Basajjabalaba alipwe fidia,
  lakini wabunge wanasema
  kuwa pesa hizo zilikuwa
  nyingi kupita kiasi. Mawaziri hao walidai kuwa walipokea
  maagizo kutoka kwa Rais
  ambaye hata hivyo
  aliwaruka alipofika mbele ya
  Kamati ya Bunge
  inayochunguza kashfa hii. Hawa mawaziri ni watatu
  kujiuzulu katika kipindi cha
  miezi mitatu kuanzia mwezi
  Disemba mwaka jana.
   
 2. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Huu ndio uwajibikaji katika utawala bora
   
Loading...