Mawaziri wawili wa Rais Magufuli watajwa vyeti bandia

Kuna washkaji kama wa 5 wote kutoka mbeya tulisoma nao O level .
Wamesajiliwa form one na majina mengine,kufika form 3 wakaenda mahakamani kubadilisha majina.
Darasa LA 7 walifeli ,wakarudia kwa kutumia majina,either ya marehemu au watoro.
Sasa sijui kisheria inakuaje hapo
 
Usikurupuke wewe na mawazo mfu ya wivu.chuki.majungu na umaskini wa Kila kitu..yaani MTU atumie jina regardless alifanani na majina ya ndugu zake asome darasa la saba.form four.six.university level halafu apate kazi yake ya maana..wewe uje useme jina lake haliendani sijui na nn.haya hata mtume Paulo alibadilisha jina la awali sauli ndo akafanikiwa.
Suala ni kufanya udanganyifu. Tunazungumzia uadilifu. Hao unaowatetea hapa walisoma na kufeli mara nyingi darasa la saba, baadaye wakafanya udanganyifu kwa kutumia majina yasiyo yao wakarudia madarasa na baadaye kufaulu; miongoni mwao ni hao wanaotajwa sana akiwemo waziri anayejidai kuwa ni msomi sana anayetoa matamko kila siku kwamba tatizo la umeme Tanzania sasa ni historia huku tukiendelea kuwa na mgawo wa umeme kila siku katika maeneo tofauti tofauti. Hilo ni kundi la kwanza.

Kundi la pili, kuna vigogo katika taasisi mbalimbali za serikali, hasa kwenye majeshi yetu ambao walifeli lakini wakatumia vyeti vya watu wengine kabisa kujiunga na kwenye hayo majeshi na miongoni mwao wana vyeo vikubwa leo. Katika kundi hili hili kuna walimu wengi kweli kweli ambao walijiunga vyuo vya ualimu kwa kutumia vyeti visivyo vyao na wengine vyeti vya kughushi. Kwa hiyo ni suala la kuamua tu kwamba serikali inalenga nini katika hatua hii maana kuna wanaotumia vyeti visivyo vyao lakini wana uwezo mkubwa wa kiutendaji. Kwa maana hiyo basi, kama serikali imeamua kutafuta wale waliofoji, kwa maana ya kulinda uadilifu, hata yule waziri msomi sana pamoja na yule mwenye utambulisho wa uzalendo sana, wote wanaangukia katika kundi la waliofanya udanganyifu! vinginevyo serikali ifanye "msako" wa watendaji au wafanyakazi wasio na viwango ili kuwaepusha "double standard" katika zoezi zima maana ukweli ni kwamba udanganyifu ni udanganyifu tu, hakuna udanganyifu mdogo!
 
Hivi km mtu alitumia jina la mtu aliyeacha shule,yule aliyelitumia akalitumia vizuri na akafaulu nani atakayekuwa amefaulu!!??

Mtu aliechukua Mkopo kwa jina marehemu na kwenda chuo kikuu na aliyechukua jina mwanafunzi aliyeacha shule darasa la tano wote wezi tu
 
Msako wa watu wanaotumia fyeti vya bandia umeshika kasi.Taarifa zinasema kuwa vigezo vinavyotumika sio tu kwa waliofoji vyeti au kutumia cheti cha mtu mwingine,pia hata wale waliotumia majina ya watu wengine kujiendeleza kielimu. Wasaka vyeti hao wamekuwa wakizingatia pia vyeti vya kuzaliwa kama vinaendana na hali halisi ya kijijini kwenu.

Katika sakata hilo wametajwa mawaziri wawili wa awamu ya HAPA KAZI TU. Mawaziri hao ingawa hawajaguswa na wanaweza wasiguswe,wametajwa kutumia majina yasiyo yao kujiendeleza kielimu. Taarifa za ndani zinaonyesha kuwa vigogo hao walianza kutumia majina yasiyo yao katika kutafuta ufaulu wa elimu ya msingi.Kwa mantiki hiyo majina ya vigogo hao yana utata kiasi cha kutofanana kabisa na majina ya ndugu zao wa damu.

Vigogo hao wanatajwa kuwa wanaweza kuwa wamefoji vyeti vya kuzaliwa ili vioane na majina wanaotumia.Inawezekanaje katika familia yenu wote ni wewe tu utumie ubin wa peke yako?

Wanahoji wadukuzi.
udaku wa kibawacha........ wataje basi
 
cha msingi ni kwamba je cheti unachokitumia ni cha kwako? au umegushi, kuhusu majina wala hata sishangai maana kuna wengine unakuta wametumia majina ya uncle zao kama baba zao,wengine majina ya baba zao wa kambo nk kulingana na historia ya mtu.

Wale waliosoma seminary wanajua vzr kuhusu majina utakuta jina la primary ni lingine na alilotumia sekondari linakuwa tofauti,
 
Suala ni kufanya udanganyifu. Tunazungumzia uadilifu. Hao unaowatetea hapa walisoma na kufeli mara nyingi darasa la saba, baadaye wakafanya udanganyifu kwa kutumia majina yasiyo yao wakarudia madarasa na baadaye kufaulu; miongoni mwao ni hao wanaotajwa sana akiwemo waziri anayejidai kuwa ni msomi sana anayetoa matamko kila siku kwamba tatizo la umeme Tanzania sasa ni historia huku tukiendelea kuwa na mgawo wa umeme kila siku katika maeneo tofauti tofauti. Hilo ni kundi la kwanza.

Kundi la pili, kuna vigogo katika taasisi mbalimbali za serikali, hasa kwenye majeshi yetu ambao walifeli lakini wakatumia vyeti vya watu wengine kabisa kujiunga na kwenye hayo majeshi na miongoni mwao wana vyeo vikubwa leo. Katika kundi hili hili kuna walimu wengi kweli kweli ambao walijiunga vyuo vya ualimu kwa kutumia vyeti visivyo vyao na wengine vyeti vya kughushi. Kwa hiyo ni suala la kuamua tu kwamba serikali inalenga nini katika hatua hii maana kuna wanaotumia vyeti visivyo vyao lakini wana uwezo mkubwa wa kiutendaji. Kwa maana hiyo basi, kama serikali imeamua kutafuta wale waliofoji, kwa maana ya kulinda uadilifu, hata yule waziri msomi sana pamoja na yule mwenye utambulisho wa uzalendo sana, wote wanaangukia katika kundi la waliofanya udanganyifu! vinginevyo serikali ifanye "msako" wa watendaji au wafanyakazi wasio na viwango ili kuwaepusha "double standard" katika zoezi zima maana ukweli ni kwamba udanganyifu ni udanganyifu tu, hakuna udanganyifu mdogo!

Zoezi lisiishie kwenye mawaziri tu, Makatibu Wakuu pia. Yupo mmoja wizara nyeti Tambaza Sec na Galanos High School tukimfahamu kwa jina tofauti na hili analotumia sasa. Isiishie hapo, na uraia pia mashaka. (Labda awe ameukana ule mwingine).
 
Mkuu hapo ndipo tunapopishana mimi nawe, unaacha kujadili mada yaani Vyeti feki wewe unahamishia kwenye siasa
Shida IPO wapi
Nimesema waende kukagua hadi vyama vya siasa hukunielewa!!
Unategemea nini cdm ikija kuchukua nchi
Mawaziri watatoka wapi kama hatujajua vyeti vyao
 
Back
Top Bottom