Mawaziri wawili wa Rais Magufuli watajwa vyeti bandia

Hoja yako imeonesha vendetta dhidi ya huyo unayemtaja kuwa msomi sana na huyo mzalendo wako. Unatakiwa kuelewa sera yetu ya elimu ilivyobadilika (1961 - 1978), na baada ya 1995, na sababu/ malengo ya mabadiliko hayo. Huyo unayemlenga alipata elimu ya msingi kabla ya 1978 wakati sera ya elimu iliruhusu wanafunzi kukariri madarasa; IV, VII/VIII. Sasa kama alikariri na baadaye kusoma na ku-excel hadi kuwa professa kwa uwezo wake mwenyewe hoja yako ni nini? Binafsi kuna Profesa wiwili maarufu ninaowafahamu; mmoja mchumi mwingine mtaalum wa hisabati. Hawa wote wali-'disco' mwaka wa pili UDSM baadaye walirudi tena baada ya miaka 5, walisoma na ku-excel non-stop hadi kuwa profesa. Hapa tunaangalia mambo makuu 2; sera ya UDSM, na uwezo wa wahusika ku-muster masomo. Nadhani tuache kutumia mipango ya serikali kufanya witch-hunting ua ku-settle old scores dhidi ya watendaji/viongozi tusiowapenda. Waliorudia darasa la saba na kuendelea hadi kuwa nguli wetu wa sasa hawakuwahi kughushi cheti chochote hivyo siyo target ya mpango wa kufurumusha wafanyakazi wenye vyeti fake. Hoja ya mpango wa serikali ni si waliowahi kurudia darasa la saba na baadaye kuwa wataalam nguli waliobobea, la hasha. Ni wafanyakazi walioghushi vyeti kujipatia ajira serikalini. Tusichanganye mambo.
Mkuu Sophist asante kwa kunisaidia kuelewa. Nisaidie nielewe zaidi-hiyo sera iliruhusu udanganyifu? Yaani unaghushi jina lisilo lako ili ukariri darasa? Ni kwanini basi kama serikali ilikuwa imeruhusu kabisa kabisa hao wanafunzi wasingekuwa wanatumia majina yao halisi? Mimi sijasema kama kuna tatizo kwa mtu kukariri darasa na baadaye ku-excel hadi kuwa profesa, nilikuwa nazungumzia udanganyifu, na ndio maana nilihitimisha kwa kusema hakuna udanganyifu mdogo wala mkubwa. Umekosea sana kwenda umbali wa kuhitimisha kuwa watu tunaowatolea mfano hatuwapendi!
 
Jamani me ndio maana nasemaga tujenge nchi kwa upya tukianza kuyachokonoa yanyuma asilimia kubwa ya ndugu rafiki au jamaa zetu hawako salama katika hili.
 
Mkuu Sophist asante kwa kunisaidia kuelewa. Nisaidie nielewe zaidi-hiyo sera iliruhusu udanganyifu? Yaani unaghushi jina lisilo lako ili ukariri darasa? Ni kwanini basi kama serikali ilikuwa imeruhusu kabisa kabisa hao wanafunzi wasingekuwa wanatumia majina yao halisi? Mimi sijasema kama kuna tatizo kwa mtu kukariri darasa na baadaye ku-excel hadi kuwa profesa, nilikuwa nazungumzia udanganyifu, na ndio maana nilihitimisha kwa kusema hakuna udanganyifu mdogo wala mkubwa. Umekosea sana kwenda umbali wa kuhitimisha kuwa watu tunaowatolea mfano hatuwapendi!
Labda nikuulize kisheria utawezaje kumtambua mtu ambaye kuanzia darasa la vii hadi phd vyeti vyake vyote vimeandikwa jina lilele analotumia, na kwenye passport yake pia, kuwa alighushi jina? Jina asilolitumia mahali popote? Sana sana utaambulia kuambiwa kuwa kijijini kwake wanamwita jina fulani, lakini kuitwa hivyo kijijini kwake haina legal weight. Sijui iwapo unajua kuwa Jakaya Mrisho Kikwete enzi za utoto wake kule Msoga, Mboga na Msata aliitwa Micho? Lakini ni rahisi ku-establish ilegality kwa mtu aliyegushi cheti aweze kupata kazi au kendelea na masomo. Maana utakuta mtu hana cheti cha darasa la vii au cha form iv au cha form vi au anavyo ila vinatofautiana na majina yaliyoamdikwa kwenye shahada.
 
Kumbe Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete pale kwao Msogani anaitwa Micho???
Kweli mkuu,umesema ukweli kabisa,Mimi natoka kijiji cha Lowa wilaya ya Kahama,huyu mkurugenzi mkuu wa TACAIDS Dr Leonard Maboko kule kwetu tunamjua kwa jina la Shilaga...!!! Hakuna mtu anayemjua kwa jina la Leonard...
 
Assume tumejitoa ufahamu na kumfukuza kazi
huyu aliyesoma lakini akatumia jina ambalo si la kwake
unadhani akienda nje ya nchi atakosa kazi kwa sababu ya jina?
kama ni mtaalam wa jambo fulani au mwalimu chuo kikuu
utalazimika kuazima mtaalam wa kuziba nafasi yake na kumlipa fedha ya kigeni
kwa sababu tu ya kukomoana.

Nakuhakikishia msomi aliyetoa jasho lake mpaka akapata shahada ya udaktari,
hata ukimfukuza kazi kwa madai ya eti kafoji jina, utakuwa umejikomoa mwenyewe
na wala si yeye maana kama kweli ana huo udaktari hatakosa chuo binafsi akafundisha
au kutoka nje ya nchi na kuchapa kazi na maisha kusonga.

Binafsi naona sehemu hii serikali iwe makini
Lengo la serikali ni kuondoa makanjanja na si kukomoa
watu,makanjanja hawatoi huduma ipasavyo
bali wamefoji vyeti ili wapate vyeo waibe hela.Wasomi waliotumia majina bandia
ili mradi utaalam wao unasaidia watanzania hatuna haja ya kuhangaika nao.

Tatizo ni nchi kukosa mwelekeo. Haya madudu yalijulikana miaka kadha iliyopita na hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wahusika ambao baadhi yao ilisemekana walikuwa mawaziri! Kwa vyombo husika kupuuza tuhuma nzito kama hizi kwakuwa ziliwagusa wakubwa, vyombo hivyo vilipanda mbegu ya kutokuwajibika. Matunda yake ndiyo haya, elimu ya TZ imekuwa magumashi matupu, samaki mmoja akioza, tenga zima limeoza.
 
Kuna washkaji kama wa 5 wote kutoka mbeya tulisoma nao O level .
Wamesajiliwa form one na majina mengine,kufika form 3 wakaenda mahakamani kubadilisha majina.
Darasa LA 7 walifeli ,wakarudia kwa kutumia majina,either ya marehemu au watoro.
Sasa sijui kisheria inakuaje hapo
hiI ILIKUWEPO SANA MIAKA YA 90 MTU AKIFELI LA SABA ANARUDIA KWA JINA LINGINE
 
Back
Top Bottom