Mawaziri wapya na 'maneno bila matendo' - tumechoka!

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Imekuwa ni kawaida kwa viongozi wateule wa JK kuanza na mbwembwe nyingi na kauli za kuonyesha kufanya kazi na kulijua tatizo, la kushangaza huishia kwenye matamko na mbwewe. Waziri wa ardhi Prf Anna Tibaijuka alikuja na mbwembwe nyingi sana leo kama hayupo vile.
Leo hii Prof wa Nishati na madini anakuja na mbwewe huku akisema madudu aliyoyakuta hawezi kuyaweka hadharani, ila baada ya hapo tutasikia ufisadi na uzembe chini yake.

Kagasheki naye kaja na kelele kibao utazani kesho wahalifu na wezi watafikishwa kisutu kumbe wanajitafutia upenyo wa kujichotea.

Kauli za JK za bandari kwamba anawajua wezi bila kuchukuliwa hatua ndizo kauli wanazotumia wasaidizi wake.

Tumechoka na maneno tumechoka na mbwembwe tunataka mfanye kazi hatutaki kauli wala matamko tunataka matendo yataongea yenyewe.
 
Tusiwe wepesi wa kulaumu kabla muda wa kulaumu haujawadia, Ndo kwanza mawaziri wanaanza kazi, wasi wasi wa nini?
 
Wanaiga stail ya bos wao jk,siku za mafisadi zinahesabika mara nina orodha ya wauza unga na ahadi hewa kigoma itakuwa dubai,train ya umeme mwanza dar.,usitegemee chochote china ya utawala wa wezi ccm!
 
Wewe mbwembwe za Mawaziri wakichaguliwa umeanza kuzisikia leo? kila waziri akiteuliwa tu maneno meeeeengi hakuana lolote umesahau waziri wa nishati aliyepita,Huyo Prof tusubiri tu,hayo madudu anayosema sisi wananchi tutamuelewa kama mfano atashusha bei ya umeme hiv hapo ndio tunaweza kuelewa kweli amekuta madudu vinginenevyo hizo ni bongo 'fleva'.
 
Wanaiga stail ya bos wao jk,siku za mafisadi zinahesabika mara nina orodha ya wauza unga na ahadi hewa kigoma itakuwa dubai,train ya umeme mwanza dar.,usitegemee chochote china ya utawala wa wezi ccm!

Tambua kwamba udhaifu upo katika sheria zetu.
 
Kila anaechaguliwa maneno maneno tuu vitendo hakuna hatushangai ni serikali ya waongo waliotokana na chama cha waongo uongo kwao ni sera ya chama chao
 
Ni mapema mnoo, wapeni muda wafanye kazi.

Mimi huwa siamini kwenye mawaziri wapiga kelele. Waziri mchapa kazi kamwe huwezi kumsikia sikia kwenye vyombo habari kila siku.
 
Tuwape Muda wajipange ka kazi. Ni mapema mno hata mshahara mmoja bado hawajapokea. Tuwe na subira.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Kama ndio hivyo,basi kuna walakini katika mfumo mzima wa utendaji ambao waziri anatakiwa kuufuata,yawezekana matakwa yake yasipewe baraka na muundo uliopo.Sio busara kuwatupia lawama mawaziri wote walioingia kwa matarajio lakini wakakutana na vigingi.
 
Tusiwe wepesi wa kulaumu kabla muda wa kulaumu haujawadia, Ndo kwanza mawaziri wanaanza kazi, wasi wasi wa nini?

historia inawahukumu wao sio wapya kwenye hilo baraza madudu matupu nambie ni kttu gani walichosema huko nyuma kikakamilika?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom