Mawaziri wapishana mgodini kutatua matatizo Kahama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wapishana mgodini kutatua matatizo Kahama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 10, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,812
  Likes Received: 83,186
  Trophy Points: 280
  Date::10/10/2008
  Mawaziri wapishana mgodini kutatua matatizo Kahama
  Na Mwandishi Wetu
  Mwananchi

  WAKATI Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja akiondoka jana wilayani hapa kumaliza mgogoro wa mgodi wa Bulyanhulu na wanakijiji wa Kakola, naibu wake ameingia Kahama kumaliza mgogoro wa wananchi wa Buzwagi na kampuni ya Barrick.

  Naibu huyo, Adamu Malima ameingia jana ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali ililolitoa mwezi Mei mwaka huu la kutaka mikataba yote ya fidia kwa wananchi wa Buzwagi ipitiwe upya ndani ya miezi mitatu, muda ambao umeshapita.

  Wakati naibu waziri huyo akiingia Kahama, tayari bosi wake ameondoka jana katika mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa pia na kampuni hiyo ya Barrick baada ya kushughulikia mgogoro wa wananchi wa kijiji cha Kakola wa kufungiwa umeme kama makubaliano baina ya wananchi na serikali yanavyoeleza.

  Katika makubaliano hayo, kampuni hiyo ilikubali kuwapa wananchi hao huduma za kijamii baada ya serikali kukitangaza kijiji hicho kuwa ni halali kuliko ilivyokuwa hapo nyuma wakati ilipotaka kukihamisha ili kupisha mgodi huo.

  Akiwa katika kijiji cha Kakola, Waziri Ngeleja alizindua mradi wa umeme ambao umegharimu kiasi cha dola 500,000 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh500 milioni za Tanzania) zilizotolewa na Kampuni ya Barrick kupitia mgodi wa BGML.

  Katika uzinduzi huo, Ngeleja aliwataka Wanakijiji wawe watulivu na kujenga urafiki kati yao na Mgodi hali itakayo wajengea mahusiano mazuri ya kupatiwa huduma mbalimbali za kijamii kuliko kujenga uhasama na wawekezaji, akisema migogoro huchukua muda mrefu kuitatua.


  Kabla ya kauli ya waziri huyo, meneja mkuu wa Barrick Tanzania, Deo Mwanyika aliwambia wananchi hao kuwa kampuni yake itaendelea kutoa misaada ya kijamii iwapo wananchi watajenga mahusiano ya kirafiki na mgodi huo.

  Mapema mwaka jana, wananchi hao waliziba barabara zinazoingia mgodini na kuzuia magari wakidai kupatiwa huduma za kijamii ikiwemo maji , umeme, barabara. Tayari mgodi huo umeanza kutekeleza masuala hayo.

  Akiwa Kahama, Naibu Waziri Malima anatarajiwa kumaliza mgogoro wa Buzwagi ambao unaendelea kuwa na mgogoro na wawekezaji baada ya wananchi kukata uzio na kuingia kwa nguvu ndani ya Mgodi huo wakitaka kulipwa fidia kw amadai kuwa walipunjwa katika malipo ya awali.

  Hali ya wananchi hao kuingia kwa nguvu kwenda kuishi katika makazi yaliomo ndani ya mgodi kulimfanya kaimu mkuu wa wilaya ya Kahama, Magesa Mlongo kuwatawanya kwa nguvu wananchi hao, akitumia polisi ambao wakati fulani walifyatua mabomu ya machozi.

  Baada ya Vurugu hizo, serikali iliingilia kati na kuagiza mikataban yote ya malipo ya fidia kurudiwa upya kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sidhani kuwa wananchi wa Tanzania wanataka "handouts" Ni haki yao kupewa stahiki yao kutokana na mapato ya madini yanayotoka kwenye ardhi yao.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,812
  Likes Received: 83,186
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa Jasusi. Wakati Barrick wanavuna mabilioni wakitoa vijisenti vichache kuwadanganya Watanzania wa maeneo hayo wanaonekana wamewafanyia mambo ya maana sana kumbe hakuna lolote ni wizi tu tena wa mchana kweupe. Na huyo Ngeleja bado hajatoa mapendekezo ya serikali kuhusiana na ripoti ya kamati ya madini iliyoongozwa na Bomani eti kwa kuwa Sitta 'hakumpa" muda wa kufanya hivyo kwenye kikao cha bunge la bajeti.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh!...Mradi wa umeme umegharimu dollar 500,000!.. Yaani waziri mzima anakwenda kufungua mradi ambao ni punje ya kile Barricks wataweza kuvuna within no time!..
  Lini wananchi watakuwa na hisa katika mashirika yanayokuja chukua ardhi na rasilimali zao?..hivi kweli sisi tunashindwa kuweka Umeme wa dollar 500, 000 ikiwa tutakatiwa chetu.
  Mbona tunazidi kuuza nchi?...
  Kuna hili swala jingine nimelisikia sijui kama kuna umkweli naomba mtu mwenye taarifa atufahamishe vizuri.
  Barricks wanaendelea na Ujenzi wa mgodi wa Buzwagi kama kawaida na wapo karibu kabisa kuanza uzalishaji...Wananchi tayari wamekwisha hamishwa na hakuna kitu kilichobadilika kutoka mkataba wa kwanza..
  Habari hizi zina ukweli?...
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,812
  Likes Received: 83,186
  Trophy Points: 280
  Date::10/11/2008
  Mgogoro wa wanakijiji na Mgodi wa Buzwagi walipuka upya
  Shija Felician, Kahama
  Mwananchi

  MGOGORO wa wananchi wa kata ya Mwendakulima wilayani Kahama waliokuwa wamehamishwa kupisha ujenzi wa mgodi wa Buzwagi kulipwa fidia, juzi ulianza upya baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kupewa taarifa zisizo sahihi na uongozi wa Kampuni ya Barrick.

  Tarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi, Benard Mihayo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama ilidai wananchi wa eneo hilo la mgodi ni wakorofi na hawataki kutoa ushirikiano kwa mwekezaji kuwalipa fidia.

  Naibu Waziri Malima yupo Kahama kutekeleza agizo la serikali lililotolewa mapema mwaka huu kupitia upya mikataba ya fidia baada ya wananchi kulalamika kuwa walipewa malipo madogo.

  Baada ya kubaini taarifa aliyopewa juzi kuwa haikuwa sahihi aliwataka viongozi wa mgodi kufuatana naye hadi katika mkutano wa hadhara kwa wananchi ili kuhakikisha kama taarifa aliyopewa ni ya kweli.

  Katika Mkutano wa hadhara uliowakutanisha wananchi wa Kata ya Mwendakulima, viongozi wa Mgodi wa Buzwagi walishindwa kufika hali iliyomfanya Naibu waziri huyo kuchachamaa akiamini kuwa wananchi hao wanaidharau serikali.

  Aidha katika mkutano huo wananchi walilalamika kuwa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya mgodi wa Buzwagi hawashirikishi katika vikao vya kumaliza mgogoro kama ilivyokuwa imeagizwa na serikali na badala yake wamekuwa wakikaa wao peke yao.

  Kitendo hicho cha kukosekana kwa uongozi wa mgodi katika mkutano huo kilimwudhi Waziri Malima na kumfanya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kahama Magesa Mulongo kumwamuru Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya kumkamata mara moja Afisa Uhusiano wa mgodi huo.

  '' Naagiza mbele ya mkutano huu kuwa Afisa Uhusiano wa mgodi wa Buzwagi Mihayo, akamatwe ifikapo saa 2:00 usiku OCD wa Kahama unipe taarifa kuwa amekamatwa, '' Mulongo alisema.

  Hata hivyo, katika mkutano huo Malima aliagiza kuwa vikao vya malipo ya fidia ikiwamo ya makazi mbadala viaze upya kwa kushirikisha viongozi wa serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama akiwamo Mwanasheria na mwakilishi mmoja toka wizarani na kubatirisha vikao vyote vya nyuma.

  Kampuni ya Barrick inajenga mgodi wake katika Kata ya Mwendakulima na mkataba wake kuzuia mjadala mzito bungeni ukidaiwa kuwa hauana manufaa kwa wananchi.

  Mjadala huo ulisababisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe kusimamishwa wakati akidaiwa kusema kulidaganya bunge wakati akihoji uhalali wa mkataba huo.
   
Loading...