Mawaziri wangapi watarudi majimboni kufuta nyayo za chadema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wangapi watarudi majimboni kufuta nyayo za chadema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Seif al Islam, Jun 8, 2012.

 1. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa mawaziri wapatao watano wamerejea majimboni kwao huko mikoa ya kusini kwa kile kinachoelezwa kuwa kufuta nyayo za chadema katika majimbo yao.mimi nadhani kuipokea taarifa hii kishabiki na kucheka au kuchekelea ni makosa makubwa.hivi kweli ni sahihi kwa waziri kuacha kazi za wizara na kwenda eto kushindana na cdm huko majimboni?hivi hayo majimbo hayana viongozi wa ccm?kama wapo wanafaya nini?na tujiulize zaidi kuwa ni mawaziri wangapi watarudi huko majimboni?hapo ndipo wanaotoa hoja kuwa wabunge wasiwe mawaziri wanapojengea hoja yao. Hebu tujiulize hawa cdm hawana wizara za kutawala na wana muda mwingi wa kuhangaika huko majimboni na kuvuna wanachama wa ccm sasa kama kila wakipita mawaziri wanarudi huko waneteuliwa kufuta nyayo za cdm?hivi nape atafanya kazi gani?kwa mfano wassira hapatikani ofisini kwake kiguu na njia anazurura kutwa kucha kuitukana cdm.tujiulize atafanya hivyo hadi lini?ilani ya ccm itatekelezwa vipi kwa stail hiyo?

   
 2. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Achana nayo, magamba hayajielewi sa iv, yamefikia point of no return.
   
Loading...