Kuna mijadala inaendelea kuhusu mawaziri wanaolalamika kwamba fedha za OC zinazopelekwa katika wizara zao ni ndogo, watu wengi wasiojua hali halisi wamekuwa wakishabikia wasichokijua hasa kuhusu malalamiko ya mawaziri hawa.
Ni miezi kadhaa sasa, tangu serikali ipunguze ghafla kiwango cha fedha za OC kwenda kwenye wizara, zipo wizara hupatiwa shilingi milioni tano kwa mwezi mmoja. Na imefanyika kwa miezi kadhaa sasa tangu kuingia kwa serikali ya hapa kazi tu.
Ikumbukwe fedha hizi za OC ndio hutumika kulipa stahiki za wakurugenzi, fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya, kulipa umeme, maji, kununua mafuta ya kuendeshea ofisi, kununua shajala na posho za mawaziri wanapokuwa safarini.
Hali hiyo inasababisha mpaka sasa kuna wafanyakazi wapya wengi hawajalipwa fedha zao za kujikimu huku wakiwa hawana mishahara, wanamaisha magumu mpaka inatia huzuni. Ipo wizara iliwarudisha nyumbani kwa muda na hata waliporudi bado wakakuta hali ni ile ile, hapa tunatarajia waziri waache kulalamika.
Sasa hivi yapo magari hayatembei sababu hakuna mafuta, kazi hazifanyiki kwa ufanisi sababu hata karatasi hakuna, wanashindwa kulipa umeme, wanashindwa kulipa maji, wanakatiwa hizi huduma muhimu kwenye maofisi wataacha kulalamika. Kuna ofisi ziko kwenye majengo ya kupanga, hawawezi kulipa pango na wengine wameshapewa notice, ni dhambi kusema fedha hazitoshi?
Ni kweli kwamba mawaziri na makatibu wakuu wanapaswa kujua kwamba wapo kwenye zama nyingine, lakini tunapofanya maamuzi tunapaswa kuwasikiliza kwa maana wao wanajukumu la kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufanisi.