Mawaziri wanaojizulu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Waungwana mimi kwa maoni yangu Mawaziri wanaojizulu kwa kashfa mbali mbali za kifisadi inabidi pia wajiuzulu ubunge, ujumbe wa halmashauri kuu na kamati kuu pia kama wamo humo ama wafukuzwe.

Vinginevyo bunge, halmashauri kuu na kamati kuu kuendelea kuwakumbatia mafisadi hao ni kuonyesha kwamba ufisadi walioufanya hauna matatizo na hivyo kuendelea kulipwa mishahara na marupurupu manono toka pesa za walipa kodi. Kwa hiyo basi kuna haja ya Lowassa, Msabaha na Karamagi kujiondoa kwenye vyombo hivyo ama wafukuzwe.
 
Chenmge anaitaji tractor ije kumtoa ofisini sio rahisi namna hiyo.
Kwa mawaziri wanaojiuzuru nafikiri wanatakiwa wajiuzuru na vyeo vingine vyote maana sioni logic umearibu huku unaendelea kubebwa upande mwingine.
 
Mi ningependelea waswekwe Lupango waozee humo mpaka mauti (waliyoandikiwa) yatakapowakuta.
 
Mi ningependelea waswekwe Lupango waozee humo mpaka mauti (waliyoandikiwa) yatakapowakuta.

Hili likitokea ndio ufisadi unaweza kupigwa vita Tanzania, lakini vinginevyo utaendelea kushamiri tu maana mtu anafanya ufisadi wa mabilioni ya pesa anajiuzulu uwaziri lakini wakati huo huo anaendelea kuwa mbunge na kuendelea kulipwa mshahara na marupurupu manono kama vile hakuhusika na kashfa yoyote ile ambayo imesababisha Tifa kupoteza mabilioni ya shiling.
 
Back
Top Bottom