Mawaziri waliokumbwa na kashfa Kuburuzwa Mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri waliokumbwa na kashfa Kuburuzwa Mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 10, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimehakikisha kuwaburuza mahakamani mawaziri ambao wamekumbwa na kashfa za ufisadi iliyotajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mawaziri sita wametajwa katika ripoti hiyo na tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inafanya uchunguzi dhidi ya mawaziri hao

  Hayo yalithibitishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipokuwa akizungumza na wanahabari jana
  Nnauye alisema kuwa kama uchunguzi wa Takukuru utathibitisha tuhuma hizo kuna ulazima wa kuwapandisha kizimbani kwani hakuna aliye juu ya sheria.

  Mawaziri walioachwa katika baraza jipya na wanaokabiliwa na kashfa hizo akiwemo Dk Hadji Mponda aliyekuwa [Afya na Ustawi wa Jamii), William Ngeleja (Nishati na Madini).
  Mustafa Mkulo aliyekuwa (Fedha), Omary Nundu (Uchukuzi, Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara), na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii)

  Wengine wenye kashfa waliobahatika kuhamishwa wizara ni George Mkuchika aliyekuwa Ofisi ya Waziri Mkuu na sasa amehamishiwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), na Profesa Jumanne Maghembe aliyuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika na sasa amepewa wizara ya Maji.

  Nnauye pia aliwaambia wanahabari jana kuwa Mei 12 Rais Jakaya Kikwete atafungua kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM Mei 13, itakuwa ni siku ya semina kwa wajumbe wa NEC ambayo pamoja na mambo mengine, watapata nafasi ya kuipitia Katiba mpya ya CCM pamoja na marekebisho.

  Mei 14, kutakuwa na kikao cha NEC ambacho kitajadili mustakabali wa siasa nchini pamoja na mabadiliko ya Katiba ya nchi.

  Mawaziri waliokumbwa na kashfa Kuburuzwa Mahakamani[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Waache usanii! Wameshafanya nini na watuhumiwa wa rada, richmond, meremeta, nk! Wajinga ndiyo waliwao. Wakitaka tuone waki serious tuone kwanza mramba akisota nyuma ya bars, mkapa akisimama mahakamani kujitetea kwa tuhuma za kiwa nkma ya bars
   
 3. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Hii ni filamu ingine tena kwani hao TAKUKURU, si ndo waliowahi kutueleza kuwa hakukuwa na mazingira ya rushwa kwenye ishu ya Richmond...tusubiri mwisho wa filamu,,,,,,
   
 4. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hizi Filimee sijui zitaisha pindi Dr. Slaa atakapokuwa Rais... Kesi za EPA ziko wapi, polisi wanakamata madawa ya kulevya (mtoto wa liyumba alikamatwa), lakini hadi leo maruerue, huu ni upuuzi tu...
   
 5. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CCM wanaendeleza igizo lao hii nadhani itakuwa sehemu ya 30 ukianzia tangu kwa kina Balali.....,
  Wanadhani wanawaongoza vipofu kama wao walivyo
   
Loading...