Mawaziri wakatiwa maji

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
kama Mawaziri wakatiwa maji..Mbona Dr I.Rashid alipotaka kiwanda kikatiwe umeme ikawa mzozo?naomba ufafanuzi tafandhali.
====================================================================================
2007-12-07 09:06:53
Na Simon Mhina

Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO), jana lilifanya kweli kwa kuwakatia maji baadhi ya Mawaziri na Naibu wao kadhaa wanaoishi maeneo ya Masaki na Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam kutokana na malimbikizo makubwa ya bili zao.

hatua hiyo ilikuja baada ya mwanzoni mwa wiki, DAWASCO kueleza bayana azma yake ya kuwakatia maji vigogo hao kwa maelezo kuwa madeni yao ni ya muda mrefu.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe umebaini kuwa, hadi kufikia jana, Mawaziri na Naibu wao kadhaa, tayari walikuwa wamekatiwa huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya DAWASCO
jijini jana, Meneja Uhusiano wa mamlaka hiyo, Bi. Badra Masoud, alisema huduma ya maji ilikatwa eneo la Masaki asubuhi na zoezi la kukata maji eneo la Mbezi Beach, lilikuwa likielekea kukamilika.

Alisema zoezi hilo pia litaendelea katika maeneo ya Msasani, Mikocheni, Ada Estate, Mikocheni na Mwenge.

Alisema baada ya ziara hiyo, amegundua kwamba wananchi wengi wamejitokeza kulipia ankara zao, ili kuepuka usumbufu na adha ya kukatiwa maji.

Hata hivyo, Bi. Badra alisema bado kiwango cha ukusanyaji wa madeni hakiridhishi, hivyo hawatasitisha zoezi hilo.
Alisema wamebaini kwamba watu ambao hawalipi bili ya maji wengi wao ni wale wenye uwezo na vipato vikubwa, na hatua yao ya kutolipa inatokana na kupuuza wajibu wao.

Bi. Badra alisema visingizio vya kusema mimi sijapata ankara ya mwezi huu au ule, havitasikilizwa na wala havisaidii.

Alisema imekuwa tabia ya wateja wakishakatiwa huduma hiyo, hutoa visingizio kama “Unajua mimi ni mtu wa kusafirisafiri sana au silipi kwa vile sijapatiwa ankra”
Bi. Badra alisema suala la kusafiri na kukosa nafasi ya kulipa bili haliingii akilini kwa vile DAWASCO inaendelea kuwapatia huduma.

Pia alisema si kweli kwamba kuna mteja ambaye hapelekewi ankara.

Katika kituo cha Kawe, ambacho kinawahudumia watu wa maeneo ya Mbezi, wafanyakazi walimlalamikia Bi. Badra kwamba wanapata adha kubwa, za kutukanwa, kukimbizwa na Mbwa na kutishiwa maisha, wanapokwenda kusoma mita.

Mmoja wa wafanyakazi hao, alimweleza Meneja huyo kwamba kuna siku aliwekwa `rumande` ndani ya chumba cha mkaa cha kigogo mmoja huko Mbezi beach, baada ya kuonekana akisoma mita ya maji.

Mfanyakazi mwingine alisema Sisi wafanyakazi wa Dawasco wanatuona nuksi kiasi cha kufukuzwa na walinzi tunapofika kusoma mita, yote hayo yanatokana na ukweli kwamba watu hawataki kulipa bili.

Akihitimisha ziara hiyo katika Kituo cha kinondoni, Bi. Badra aliwataka wateja wa DAWASCO, waelewe kwamba mamlaka hiyo inatumia gharama kubwa kuwapatia huduma ya maji hivyo wajenge moyo wa kulipa, ili kurahizisha kazi ya kuwapatia watu wengi zaidi huduma hiyo muhimu.

* SOURCE: Nipashe
 
Hivi wakubwa wanatikiwa vitu vidogo kama umeme na maji? wao wako busy kulijenga Taifa jamani..

..mjj,

..are you supposing that they can even pump gas in their private vehicles for free,just b'se they are ministers who are busy building the nation?

..unachokoza watu sio!?
 
Jambo moja ambalo utility companies zetu hazijalipa kipaumbele ni kumrahisishia mteja namna ya kulipa ankara zao. Inapokuwa kwamba ukitaka kulipa ankara ni lazima uende kwenye ofisi zao ambazo zinafanya kazi wakati ambapo wewe unahitajika katika sehemu ya kibarua chacho inatia uvivu. Ukiongezea mara baada ya kufika hapo mahali pa kulipia unahitajika kujipanga mstari ambao siku nyingine hasa mwisho wa mwezi inazidi kukatisha tamaa. Kwa nini pasiwe na uwezekano wa kulipia moja kwa moja kwenye account zao kwa kupitia benki yako? Hii inaweza kufanyika kwa mteja mwenyewe kwenda physically benki, kutumia ATM au kupitia mtandao! Hii itampa uhuru mteja kulipa kwa convenience yake na kupunguza adha ya kwenda mpaka Pugu road kulipia! Au mambo haya tayari yanawezekana maana niliishakatiwa maji na umeme miaka mingi kidogo iliyopita. Mimi ni mtu wa visima na solar.
 
..fundi,

..hivi mbona watu mnapata muda wa kwenda gtv kulipia?ili muone premier league sio?

..mbona unaweza tuna mtu mwingine kukufanyia hiyo kazi?unajua,uzuri wa kwenda wewe pale ni kama hiyo ankara yako mahesabu yake hayajakaa vizuri. na hizi za maji au umeme ni kitu cha kawaida!

..ila wazo la kulipia kupitia benki ni zuri pia!ila hizi benki zetu nyingine utapanga foleni pia!

..labda dawasco waweke sehemu za malipo kikanda na zaidi,jinsi iwezekanavyo.
 
Gtv ndiyo nini? Nadhani hiyo bidhaa ni ya wenye nazo ndiyo maana kulipa si matatizo! Nani mwingine nimtume wakati sijaoa na sina mfanyakazi wa ndani? Ninachosema tu ni hawa ndugu inabidi waturahisishie namna ya kuwalipa hizi huduma muhimu. Waturahisishie ili tuweze kuwalipa.Nakumbuka mistari ilivyokuwa pale Tanesco makao makuu kabla ya luku! Ulihitaji moyo kujiunga. Hata huyo ambaye ningemtuma si bora angekuwa anafanya kazi za maana zaidi badala ya kukaa siku nzima kwenye mstari?
 
..anyways,

..unajua,hii sekta ya umeme na maji ina matatizo ya muda mrefu ya kuibiwa!kukosewa ankara!na miundo mbinu mibovu!sijui nani ataweza kuyaweka sawa haya!

..naamini hayo yakikaa sawa,hata ulipaji wake utakuwa mzuri!

..kazi ipo!
 
Mawaziri wasiolipia maji watajwa

::Yumo Waziri wa Maji, Msola, Hawa Ghasia
::jumbe wa vitisho watumwa DAWASCO

na yasmine protace

MAJINA ya mawaziri sita, ambao ni miongoni mwa wateja wa Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO), waliokatiwa maji baada kushindwa kulipia ankara, yametajwa.

Mawaziri hao wanaoishi eneo la Masaki, jijini Dar es Salaam, pamoja na wakazi wengine wa eneo hilo, walikatiwa maji wiki iliyopita.

Kabla ya kuwakatia maji, DAWASCO kupitia Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Alex Kaaya, iliwaomba wateja wanaodaiwa kulipia ankara wanazodai.

Katika maombi hayo kwa wateja, DAWASCO ilitoa siku tatu wateja hao kulipia ankara hizo, hata hivyo ni wachache tu waliotii.

MTANZANIA imefanikiwa kupata baadhi ya majina ya mawaziri wanaodaiwa ankara, ambao ni pamoja na Waziri wa Maji, Dk. Shukuru Kawambwa.

Wengine wanaodaiwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mizengo Pinda na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Anthony Diallo.

Katika orodha hiyo, Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, naye ametajwa, pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, naye ni mmoja wa mawaziri hao.

Akizungumzia kilichomsibu hadi kushindwa kulipia ankara zake kwa kipindi kirefu, Waziri Ghasia alidai kuwa tangu aanze kuishi katika nyumba hiyo amekuwa hapati huduma ya maji.

Alisema amekuwa akinunua maji kutoka kwa wafanyabiashara binafsi na si kampuni ya DAWASCO.

“Kwa hili jambo ni la binafsi mno. Lakini hata hivyo, lakini sikuwahi kupata huduma ya maji ya DAWASCO na zaidi sikuwahi kupata hizo bili. Sikuwahi kuletewa bili hadi leo,” alidai Waziri Ghasia.

MTANZANIA pia iliwasiliana na Waziri Msolla kwa simu, ambaye alikiri kudaiwa, lakini akadai kuwa hakuwa akifahamu taratibu za kupata ankara na malipo.

“Ni kweli kwamba hilo suala (la kudaiwa) lilikuwapo, nami sikuwapo nchini… lakini last week (wiki iliyopita) tulipata bili na tumekwishalipia,” alisema Prof. Msolla, ambaye hakuwa tayari kuzungumza zaidi kutokana na kile alichodai yupo katika mkutano.

Waziri Simba hakuweza kupatikana, baada ya kuwasiliana naye kupitia simu yake ya mkononi. Majibu kutoka kwa aliyepokea simu hiyo yalieleza kuwa waziri huyo yuko safarini Marekani.

Waziri wa Maji, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Anthony Diallo, Waziri wa TAMISEMI, Mizengo Pinda, hawakupatikana, baada ya simu zao za mkononi kuita kwa muda mrefu bila kujibiwa.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza, DAWASCO imesita kuzungumzia majaliwa ya viongozi hao kurejeshewa huduma ya maji.

Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Badra Masoud, alisisitiza kwamba, walichokifanya ni kukata maji kwa wadaiwa.

“Tunadai fedha nyingi sana Masaki, hivyo tunataka tuendelee kutoa huduma bora kwa wateja wetu ambao wanalipa na wasiolipa tumewakatia mpaka hapo watakapolipa,’’ alisema.

Eneo jingine lililokatiwa maji mbali na Masaki ni Mbezi Beach. Hata hivyo, tofauti na Masaki, wateja wa Mbezi Beach wamekuwa wakijitokeza kulipia ankara zao.

Katika hatua nyingine, DAWASCO imedai kupokea vitisho baada ya kuwapo kwa operesheni hiyo ya ukataji maji.

“Watu wananipigia simu na kunitaka niwarudishie maji eti sijafanya vizuri, lakini mimi nimesema kwamba maji yatarudishwa kama watumiaji watalipia ankara zao,’’ alisema.

Aliongeza kwamba pamoja na kupigiwa simu, pia amekuwa akitumiwa ujumbe wa maneno ya kashfa kutoka kwa watu asiowafahamu.

Takwimu za DAWASCO zinabainisha kuwa, eneo la Masaki lenye wateja 1,270 linadaiwa Sh milioni 574, wakati Mbezi Beach kuna wateja 1,271 wanaodaiwa Sh milioni 578.

Eneo la Ada Estate lenye wateja 475 wanadaiwa Sh milioni 527, Mwenge wateja 733 wakiwa wanadaiwa Sh milioni 463 na Regent kwenye wateja 222 wanadaiwa Sh milioni 200,’’ alisema.
 
kaaazi kwelikweli
na inabidi waangaliwe kama wanalipa kodi hawa magogo ops vigogo
 
Haya hii ni nukuu kutoka kwenye post ya Keil:

"MTANZANIA pia iliwasiliana na Waziri Msolla kwa simu, ambaye alikiri kudaiwa, lakini akadai kuwa hakuwa akifahamu taratibu za kupata ankara na malipo."

Duh Waziri hapo inakuwa ngumu kweli Sayansi itafika na teknolojia inavyodhamiriwa?? Waziri hajui hata utaratibu wa kulipia maji nyumbani kwake jamani?? Hapo huyu mkuu am,evuka mipaka manake akikaa bungeni anatakiwa apitishe sheria nyingi zinazowagusa wananchi zikiwemo za maji, nishati, madini n.k. Sasa kama hajui hata maji yanaklipwaje, yanalipiwa kiasi gani; unategemea ataweza kuwa na chochoye cha kuwatetea wananchiu kweli...
Sasa kama hata bili ya maji hajui utaratibu huko kwenye mikataba ya nje ambapo wenzetu wapo roho juu kututafuna si watatumaliza jamani?? Ndio maana tunasema pamoja na rushwa, pia kuna swala la kujua/kufahamu "EXPOSURE" ambayo hakuna wa kukufundisha hii ni juhudi ya mtu mwenyewe kujisomea na kuangalia vitu kama TV, mtandao n.k
 
Hawa viongozi waangaliwe katika kila upande sio maji tu. nina hakika kuna kodi nyingi tu ambazo hawalipi. Watuibie mamilioni ya kodi halafu wasilipe kile wanachotakiwa kulipa. Shame on them.

Sisi walala hoi tubangaize tulipe zetu nyinyi wenye pesa mdaiwe mapesa mengi hivyo halafu mnataka ati msikatiwe maji. mbona operesheni ikipita uswahilini hakuna cha kusamehe ni mpaka bili ilipwe?

halafu nyinyi viongozi ndio mnahubiri maendeleo yatakujaje kama mtindo ndio huu mnafikiri hao DAWASCO watajiendeshaje.Style up na muache ubinafsi.
 
Nanukuu:
MTANZANIA pia iliwasiliana na Waziri Msolla kwa simu, ambaye alikiri kudaiwa, lakini akadai kuwa hakuwa akifahamu taratibu za kupata ankara na malipo.
Kama waziri wa Elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia hajui hii kitu, nanai atajua Tz hii.
'Mungu ulie juu sikia sala zetu'
 
Nawasalimieni wana JF toka Dar. Nimewasili hapa Jumapili Desemba 6, kwa ajili ya likizo, na nikakuta nyumbani kwangu wamekatiwa maji. Hakukuweko na deni la maji kwangu.

Jana Jumatatu nilikwenda Kawe kuulizia imekuwaje. Baada ya kucheki na kuhakikisha hakuna deni, waliahidi wangeleta maji kwa boza. Tuko wengi, kwa hivyo ni ahadi ya danganya toto. Sijaona boza kenyewe. Na likionekana bila shaka itakwa ni kutupatia ndoo mbili au tatu kila mtu, kwani tuko wengi sana.

Kuna kipindupindu hapa Dar. Kukatiwa maji wakati huu ni hatari sana. Nasikitika sana jinsi maisha ya Mtanzania yalivyokuwa magumu. Mimi niko likizo tu, nitaachana na hizi shida baada ya miezi miwili. Hata hivyo, nasikitika kweli kweli kuona hali halisi ilivyokuwa ngumu.

Kuna kosa la msingi linafanywa. Watu wameharakisha kulipia maji wakidhani kwamba wakishafanya hivyo basi wataunganishwa tena. Ukweli umekuwa tofauti. Fundisho ni kwamba hii operesheni itakapohamia kwingine, ulipaji utakwa mdogo sana, kwani hupewi maji hata kama ukilipia.

Kuna swala la kukosekana utawala wa kisheria hapa. Kisheria, yako makubaliano kati yetu sisi na Dawasco. Kutukatia maji wakati hatuna deni lolote kwao ni kukiuka makubaliano.

I did not know that the quality of life in Tanzania could get this bad. I guess I was not aware of how cruel some parastatal companies could be!

Huwa napenda kurudi nyumbani Tanzania kwa likizo kila mwaka. Hata wakitunyima maji bado naichukulia Tanzania kwamba ni nyumbani kwangu, sitaacha kurudi mara kwa mara.

Augustine Moshi
 
Pole sana Mkuu! Mimi ndiyo maana naamini kabisa kuwa kuna haja ya kubadilisha viongozi wa hizi utility companies zetu. Wamezoea mno kutuburuza wateja.
 
...Jana Jumatatu nilikwenda Kawe kuulizia imekuwaje. Baada ya kucheki na kuhakikisha hakuna deni, waliahidi wangeleta maji kwa boza. Tuko wengi, kwa hivyo ni ahadi ya danganya toto. Sijaona boza kenyewe. Na likionekana bila shaka itakwa ni kutupatia ndoo mbili au tatu kila mtu, kwani tuko wengi sana.

Kuna kipindupindu hapa Dar. Kukatiwa maji wakati huu ni hatari sana. Nasikitika sana jinsi maisha ya Mtanzania yalivyokuwa magumu. Mimi niko likizo tu, nitaachana na hizi shida baada ya miezi miwili.....
I did not know that the quality of life in Tanzania could get this bad. I guess I was not aware of how cruel some parastatal companies could be!

Huwa napenda kurudi nyumbani Tanzania kwa likizo kila mwaka. Hata wakitunyima maji bado naichukulia Tanzania kwamba ni nyumbani kwangu, sitaacha kurudi mara kwa mara.
Augustine Moshi

Pole Mwl Moshi kwa kukaribishwa nyumbani kiana aina!, inasikitisha kuwa hiyo ndiyo Tanzania baada ya miaka 46 ya uhuru. Pia kama ulivyosema kipindupindu ni kimeota sugu Dar, viongozi wetu hawaoni mahusiano ya karibu sana ya ukosefu wa maji dar, ukataji wa maji dar na kipindupindu mjini.

Sasa angalia jinsi maisha ya mtanzania wa kawaida yanavyozidi kuwa magumu siku hadi siku, je huko si ndiyo tunaita kuingizwa mjini na wawakilishi wenu mliowachagua?

Nimefurahishwa na uzalendo wako, kuwa pamoja na shida na karaha zote hizo nyumbani ni nyumbani ha hutowacha kurudi. Sikukuu njema!!
 
Hivi wakubwa wanatikiwa vitu vidogo kama umeme na maji? wao wako busy kulijenga Taifa jamani..

Mwanakijiji acha hizo hao wanahela kama nini baadhi wamefikia cheo cha Mafisadi. U-busy huo unaousema ni kwamba wanashughulikia mambo yao kabla ya kipindi hiki cha muungwana kumaliza muda wake. Lazima iwe ni mfano kuanzia kwao katika zoezi hili. Unaposema ni vitu vidogo mbona kwetu maji na umeme ni vitu vikubwa? Samahani Mwanakijiji sijawahi kukupinga hadharani lakini kwa faida ya wengi kuhusu msimamo wangu imenibidi nifanye hivyo. Mawaziri hawa hawa wameshindwa hata kuzungumza na waandishi wa habari kama walivyotakiwa kisa wako kusakanya kila mmoja kivyake.
 
unavunja collective responsibility hivyo si mngeteta chemba waungwna(jokes)
 
Back
Top Bottom