Mawaziri/Wabunge kuchukua mchango kutoka kwa wenye kesi na serikali ni rushwa!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,725
9,033
Prof Tibaijuka anajaribu kudanganya watu kuwa ni sawa tu kuchukua pesa kutoka kwa mmiliki wa kampuni ambayo ina kesi na serikali kwa muda mrefu. Kwamba ni urafiki wa kawaida tu kwa mfanyabiashara kutoa Bilioni 1.6 kuchangia shule ingawa kuna kesi na madai ya serikali!. Kwa mfanyakazi yeyote wa serikali huwezi kuchukua pesa kwa mtu ambaye anafanya kazi biashara na serikali hasa wale wenye kesi inaitwa "conflict of interest" ni sawa sawa na kumpa tender ndugu yako kwenye serikali bila kusema kwamba ni ndugu yako wakati na kufanya bid za kushindana. Hivyo basi Tanzania kama nchi nyinghine Tibaijuka anatakiwa (1) kuacha/kuachishwa kazi (2) kurudisha pesa au kutoa kwa charity. Vilevile serikali inatakiwa kuchunguza hiyo shule na nani ni wachangiaji je hiyo shule ni ya Non-profit au ni ya biashara! kama ni ya biashara michango yote inatakiwa kuhesabiwa kama capital na ina tax zake. Kama ni Non-profit viilevile shule hiyo inatakiwa kuwa na list ya wazi kwenye mtandao ambayo kila mtu anaweza kuona nani kachanga na ni kwa kiasi gani kama yalivyo shule za kidini.
 
Back
Top Bottom