Mawaziri waanza kuumbuana mchana kweupe!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Magufuli awashtaki wenzake kwa JK

2007-12-08 09:07:03
Na Mashaka Mgeta, Chalinze

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Bw. John Magufuli, amewashtaki mawaziri wenzake kwa Rais Jakaya Kikwete, kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Tukio hilo lilitokea jana, kabla ya Rais Kikwete, kuhutubia mkutano uliofanyika katika kijiji cha Bwilingi, Chalinze mkoani Pwani, ambapo alizindua nyumba za ghorofa, zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mawaziri waliohusika katika kadhia hiyo, baada ya Bw. Magufuli `kuwaumbua` katika mkutano huo ni Bw. Andrew Chenge (Miundombinu) na Dk. Shukuru Kawambwa (Maji).

Bw. Magufuli, amefikia hatua hiyo siku chache, baada ya asasi ya Mpango wa Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (REDET), kutoa taarifa ya utafiti ambayo pamoja na mambo mengine, ilionyesha kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wasioridhishwa na utendaji kazi wa mawaziri.

Katika hafla ya jana, Bw. Magufuli, alianza kuishutumu Wizara ya Miundombinu, inayoongozwa na Bw. Chenge, kuwa imeshindwa kuboresha miundombinu inayoelekea katika maeneo yaliyotumika kwa ujenzi wa nyumba za NHC.

``Mheshimiwa Rais, Shirika la Nyumba la Taifa limejikuta linaingia gharama kubwa katika kuboresha miundombinu, iliyopaswa kushughulikiwa na wizara husika, lakini wameshindwa kutekelea wajibu wao huo,`` alisema.

Wakati akisema hayo, Bw. Chenge aliyehudhuria mkutano huo, alikuwa akimtazama Bw. Magufuli na baadaye kuelekeza macho yake kwa Rais Kikwete.

Bw. Magufuli, aliyeonekana kujiamini katika kutoa madai hayo, alitoa mfano wa miundombinu iliyogharamiwa na NHC, ni barabara, njia za maji na nguzo za umeme.

Aidha, alisema Wizara ya Maji inayoongozwa na Dk. Kawambwa, ambaye pia alikuwapo mkutanoni hapo, imeshindwa kufikisha huduma ya maji katika maeneo yenye nyumba hizo.

Bw. Magufuli, alitoa mfano kuwa, NHC ilitumia zaidi ya Sh. bilioni 1.4 kugharamia miundombinu kuelekea katika nyumba 213 zilizopo Boko na zaidi ya Sh. milioni 451 kwa nyumba zilizopo Mbweni, jijini Dar es Salaam.

Pia alisema zaidi ya Sh. bilioni moja zilitumika kwa ujenzi wa barabara ya kuelekea katika nyumba za Boko, na Sh. milioni 84 zilitumika kununulia transfoma, nguzo na nyaya za umeme.

Bw. Magufuli, alisema licha ya Wizara ya Maji kushindwa kufikisha maji katika eneo hilo, DAWASCO imeanza kuwatoza wapangaji wake Ankara za matumizi ya maji.

``Ninasema kwa uwazi Mheshimiwa Rais, na mawaziri wenzangu wapo hapa, siwateti wala siwachongei kwako, ninachokisema ni ukweli mtupu,` alisema na kusababisha watu waliokuwapo kumshangilia.

Hata hivyo, Rais Kikwete, alisema tofauti zilizojitokeza miongoni mwa mawaziri hao, zinastahili kusuluhishwa kwa njia ya kukutana na kuzungumza.

Rais Kikwete, alisema ikiwa mawaziri hao watakutana na kuzungumza kwa undani kuhusu mgawanyo unaopaswa kufanywa kuhusiana na gharama hizo, kuna uwezekano wa kupata suluhu.

Aidha, Rais Kikwete, aliwataka viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kupima maeneo ya Chalinze, na sehemu nyingine wilayani humo, ili yawe kivutio kwa makazi bora na kuinua thamani ya ardhi yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Martin Madekwe, alisema majengo hayo yaligharimu Sh. 822,920,000, zilizotokana na mapato ya Shirika hilo.

Alisema wakati ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea, NHC imepokea maombi 47 ya wapangaji, idadi ambayo ni mara tatu ya uwezo wa nyumba hizo.

SOURCE: Nipashe
 
Sasa tutaona muziki ukianza kupigwa hadharani... Ile ripoti ya REDET imeingiza changamoto kwenye Cabinet yetu jaman, Heko wana REDET - Keep up the Good work of waking up our "sleeping elephant"...
Unajua sisi binadamu tunatabia ya kusinzia au kujiinamia mpaka tunapokuwa tunachokozwa. Hapo naona Magufuli amejitutumua kusema "jamani ee hata kama baraza halijafanya kazi, wengine tunapigika lakini kuna mizigo tunaibebeba beba humu ndani"
Keep it up maybe one day our mighty comments in JF will be presented to the public "officially" na moto wake nadhani utakuwa wa kuotea mbali!!!
Long live tabia ya kusema ukweli na kukosoa..... However "Constructive Critisism is what we all throng for", Long live JF!!!
 
Hivi hawa mawaziri wetu hawajui kazi zao au ni kwamba baraza limekuwa kubwa mno wanagonganagongana tu hawajui nani anawajibika kwa lipi au kuna la ziada?

Kitendo cha Magufuli kama kilivyoripotiwa kinatoa ishara kuwa humo kwenye cabinet hamkani si shwari tena, hakuwa na haja ya kuwaumbua mawaziri wenzake mbele ya Rais na wananchi hivyo, unless ndio anajaribu kujikorokomba kwa rais, kwa lipi hasa, sijui...
 
Magufuli awashtaki wenzake kwa JK

2007-12-08 09:07:03
Na Mashaka Mgeta, Chalinze

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Bw. John Magufuli, amewashtaki mawaziri wenzake kwa Rais Jakaya Kikwete, kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Tukio hilo lilitokea jana, kabla ya Rais Kikwete, kuhutubia mkutano uliofanyika katika kijiji cha Bwilingi, Chalinze mkoani Pwani, ambapo alizindua nyumba za ghorofa, zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mawaziri waliohusika katika kadhia hiyo, baada ya Bw. Magufuli `kuwaumbua` katika mkutano huo ni Bw. Andrew Chenge (Miundombinu) na Dk. Shukuru Kawambwa (Maji).

Bw. Magufuli, amefikia hatua hiyo siku chache, baada ya asasi ya Mpango wa Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (REDET), kutoa taarifa ya utafiti ambayo pamoja na mambo mengine, ilionyesha kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wasioridhishwa na utendaji kazi wa mawaziri.

Katika hafla ya jana, Bw. Magufuli, alianza kuishutumu Wizara ya Miundombinu, inayoongozwa na Bw. Chenge, kuwa imeshindwa kuboresha miundombinu inayoelekea katika maeneo yaliyotumika kwa ujenzi wa nyumba za NHC.

``Mheshimiwa Rais, Shirika la Nyumba la Taifa limejikuta linaingia gharama kubwa katika kuboresha miundombinu, iliyopaswa kushughulikiwa na wizara husika, lakini wameshindwa kutekelea wajibu wao huo,`` alisema.

Wakati akisema hayo, Bw. Chenge aliyehudhuria mkutano huo, alikuwa akimtazama Bw. Magufuli na baadaye kuelekeza macho yake kwa Rais Kikwete.

Bw. Magufuli, aliyeonekana kujiamini katika kutoa madai hayo, alitoa mfano wa miundombinu iliyogharamiwa na NHC, ni barabara, njia za maji na nguzo za umeme.

Aidha, alisema Wizara ya Maji inayoongozwa na Dk. Kawambwa, ambaye pia alikuwapo mkutanoni hapo, imeshindwa kufikisha huduma ya maji katika maeneo yenye nyumba hizo.

Bw. Magufuli, alitoa mfano kuwa, NHC ilitumia zaidi ya Sh. bilioni 1.4 kugharamia miundombinu kuelekea katika nyumba 213 zilizopo Boko na zaidi ya Sh. milioni 451 kwa nyumba zilizopo Mbweni, jijini Dar es Salaam.

Pia alisema zaidi ya Sh. bilioni moja zilitumika kwa ujenzi wa barabara ya kuelekea katika nyumba za Boko, na Sh. milioni 84 zilitumika kununulia transfoma, nguzo na nyaya za umeme.

Bw. Magufuli, alisema licha ya Wizara ya Maji kushindwa kufikisha maji katika eneo hilo, DAWASCO imeanza kuwatoza wapangaji wake Ankara za matumizi ya maji.

``Ninasema kwa uwazi Mheshimiwa Rais, na mawaziri wenzangu wapo hapa, siwateti wala siwachongei kwako, ninachokisema ni ukweli mtupu,` alisema na kusababisha watu waliokuwapo kumshangilia.

Hata hivyo, Rais Kikwete, alisema tofauti zilizojitokeza miongoni mwa mawaziri hao, zinastahili kusuluhishwa kwa njia ya kukutana na kuzungumza.

Rais Kikwete, alisema ikiwa mawaziri hao watakutana na kuzungumza kwa undani kuhusu mgawanyo unaopaswa kufanywa kuhusiana na gharama hizo, kuna uwezekano wa kupata suluhu.

Aidha, Rais Kikwete, aliwataka viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kupima maeneo ya Chalinze, na sehemu nyingine wilayani humo, ili yawe kivutio kwa makazi bora na kuinua thamani ya ardhi yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Martin Madekwe, alisema majengo hayo yaligharimu Sh. 822,920,000, zilizotokana na mapato ya Shirika hilo.

Alisema wakati ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea, NHC imepokea maombi 47 ya wapangaji, idadi ambayo ni mara tatu ya uwezo wa nyumba hizo.

SOURCE: Nipashe

Hivi ndivyo inavyotakiwa hakuna cha siri kama wameanza hata kuwatoza kodi hata bila huduma na wizara yake imelipia ukarabati huo tatizo ni nini? BRAVO Magufuli na wengine wafuate mfano naona hii ni katika ile ile ya kuomba msamaha wa kodi ambapo yeye aliumbuliwa na JK kwa hiyo kaamua kuwatolea uvivu.

Kwa style hii naona tutapiga hatua, wajitetee tusikie - Pesa si wamepewa tayari.
 
Hivi
kweli alishindwa kuwachongea hao wenzake mpaka kwenye mkutano wa hadhara?[/
B]

Sioni haja kwanini Magufuli umtafutie sababu.Au kuna maandishi yanayomlazimu kueleza ugumu wa kazi yake mahala fulani tu.Yeye hakuwa anawachongea, ila alikuwa anaeleza mafanikio ya mradi na matatizo aliyokumbana nayo, na nani source ya matatizo yake.
Sasa wewe ulitaka asiseme kwa kuwa uzembe umefanywa na Mawaziri wenzake??Wao kama wanaona wameaibishwa kuanikwa mkutanoni ilitakiwa wawajibike na sio kuanza kutafuta sababu za kuonyesha maelezo yake hayana uhalali.
 
Hivi hawa mawaziri wetu hawajui kazi zao au ni kwamba baraza limekuwa kubwa mno wanagonganagongana tu hawajui nani anawajibika kwa lipi au kuna la ziada?

Kitendo cha Magufuli kama kilivyoripotiwa kinatoa ishara kuwa humo kwenye cabinet hamkani si shwari tena, hakuwa na haja ya kuwaumbua mawaziri wenzake mbele ya Rais na wananchi hivyo, unless ndio anajaribu kujikorokomba kwa rais, kwa lipi hasa, sijui...

Magufuli hajakosea,Rais alikuwepo na Chenge alikuwepo isitoshe walikuwa eneo husika la mradi kwa nini wasubiri mpaka kikao cha baraza la mawaziri? Sawa sawa alivyofanya tu maana mambo ya kuoneana aibu ndio maana watu hawapati huduma muhimu.
 
There is such a thing as "collective responsibility". Naelewa alichosema ni kweli na kinahitaji kusemwa but not in such a fashion.Serikali lazima i present a united front hata kama kuna tofauti.Hii inaonyesha jinsi tatizo lilivyo kubwa, incompetence mpaka kufikia mawaziri kulumbana hadharani.
 
haya mambo ya kutafuta fasheni za kusema ukweli ndo yametufikisha hapa tulipo, just call a spade a spade and not...

Hapo Magufuri nakupa tano mzee, hivo ndivo inavo takiwa, hao mawaziri wakiritimba wasio timiza wajibu wao, ukiwakuta kwenye viti vyao utadhani miungu watu, dawa yao ndo hii, ukweli tena ule unao umma,

hayo mambo ya 'collective responsibility' tazama yalivo sababisha CCM wakamfungia Zitto Bungeni, eti wanatoka hapo tuna wasikia kina Masilingi wana lalama kwamba hata wao japo walimtetea mwenzao Nk lakini hawakujua mkataba ukoje! Tazama madudu yanaanza anikwa sasa wachimbaji hawalipi ushuru wa mafuta milele!!!, huo ni unafiki, unao limaliza taifa letu,

Tazama Jk anashindwa panguwa mawaziri wazembe kisa?? anatafuta jinsi na fasheni ya kusema/kuwaondoa?

hakuna haja ya kuficha uozo /udhaifu eti collective responsibility!

We need more magufuris kutoka tulipo, keep it up bro.
 
Sina matatizo na Mheshimiwa Waziri kuzungumzia adha NHC walizozipata katika kupata hizo huduma. Wasiwasi wangu ni kuwa kama kiongozi kama waziri inabidi asubiri mpaka kwenye mkutano wa hadhara ili aweze kumweleza Mh. Rais kuhusu haya matatizo ni alama ya deeper malaise. Ni kama vile ninaposikia wakuu wakitembelea mikoani wanapokea ripoti za utendaji wa kazi kwenye mikutano ya hadhara! Hivi kweli hakuna taratibu zilizomo serikalini za kuweza kuwasilishwa hizi ripoti, kuchambuliwa na pale zinapoonekana kuna mapungufu mhusika kushughulikiwa? Wasiwasi wangu ni kuwa katika fora kama hizi ni vigumu kupata the true picha maana upande mmoja unakuwa hauna nafasi ya kujieleza! Pengine mimi ni naive!
 
Sioni haja kwanini Magufuli umtafutie sababu.Au kuna maandishi yanayomlazimu kueleza ugumu wa kazi yake mahala fulani tu.Yeye hakuwa anawachongea, ila alikuwa anaeleza mafanikio ya mradi na matatizo aliyokumbana nayo, na nani source ya matatizo yake.
Sasa wewe ulitaka asiseme kwa kuwa uzembe umefanywa na Mawaziri wenzake??Wao kama wanaona wameaibishwa kuanikwa mkutanoni ilitakiwa wawajibike na sio kuanza kutafuta sababu za kuonyesha maelezo yake hayana uhalali.

Sijasema maneno yake yalikuwa hayana uhalali. Kwangu mimi kinachogomba ni namna yalivyoanikwa! Ule ni mradi wa kibiashara na unaongozwa na mikataba. Pale mmoja anapoonekana hajatimiza kinachotakiwa kuna njia za kumshughulikia. NHC walipaswa kuingia mkataba na providers wa hizo services ( kama ni barabara ni makandarasi wa barabara na si wizara, na kama ni maji ni makandarasi wa kuweka mabomba na kama ni umeme ndani ya eneo ni makandarasi wa umeme na si wizara). Baada ya hili kufanyika ndipo hizi utility companies zingewajibika kuwaunganisha kwenye mtandao, nao kwa mikataba. Mimi NHC ninahitaji hiki, na mimi shirika la maji nitafanya hiki kama ukinilipa na ukifanya hiki n.k. Shirika la Maji lisipotimiza ni arbitration au kortini, na sio kwenye majukwaa ya kisiasa. Hatari ya hili ni kuwa tutapoliticise kila kitu badala ya kuwawajibisha watu kutona na kanuni za utendaji makini.
 
Wote hao pamoja na magufuli ni wa kufukuza kazi.
 
Bravo makufuli
Jamaa kuja kufikia hatua hii ,si kwamba amewavizia Naamini atakuwa amefanya nao mawasiliano na pia bado naamini atakuwa ameshaangea na Rais kuhusu hilo lakini response ikawa zero.

Angalia JK alivyojibu mgogoro ulio ndani yao inabidi wakae wa ujadidili ,hii inaonyesha kabisa JK si mara ya kwanza kulisikia swala hili.
Pili wenda mangufuli nae ameamua kuwachongea kwa wananchi kwa staili hiyo yani Kimbowe mbowe/ ki Zito

JK angekuwa na kazi ndogo sana kama PM angemweka Makufuli kizuri cha jamaa huyu huwa hana huruma wala aibu. Na hii ndio sifa nzuri na sahihi ya kuwaongoza watanzania
 
2007-12-08 10:29:04
By Guardian Reporter

Lands, Housing and Human Settlements Development minister John Magufuli yesterday complained to President Jakaya Kikwete that his efforts to build houses that ordinary wananchi can afford are consistently frustrated by two of his cabinet colleagues.

He said his ministry was doing a good job building decent but affordable houses but was repeatedly let down by Infrastructure Development and Water ministers Andrew Chenge and Shukuru Kawambwa, respectively, following their failure to improve infrastructure at construction sites.

Magufuli expressed his concern shortly after Kikwete inaugurated National Housing Corporation flats at Bwilingi village in Chalinze, Coast Region, saying Chenge`s ministry had failed to build roads to areas where the new houses have been built.

``Mr President, we have built good residential quarters in some areas but the respective occupants are finding it hard to reach them because there are no roads,`` he said.

He said NHC has often incurred expenses to build roads to houses it had put up in some parts of the country, work he said was supposed to be done by the Infrastructure Development ministry.

The corporation has spent more than 1.4bn/- on the improvement of infrastructure to facilitate access to the 214 houses it has built in Boko in suburban Dar es Salaam and more than 451m/- to those in Mbweni, also on the outskirts of the city, according to Magufuli.

He told the President that NHC spent another 1bn/- on the construction of a road to the Boko quarters and 84m/- on the purchase of a transformer and electricity poles for the area.

The minister said Dr Kawambwa`s ministry had failed to connect water to the Boko and Mbweni quarters but the Dar es Salaam Water and Sewerage Corporation (Dawasco) kept charging their occupants ``for a service they have never enjoyed``.

Both Chenge and Dr Kawambwa were around as Magufuli explained his case.

``Mr President, I am telling you all these problems because they give me sleepless nights. It is good that I am saying this while the two ministers responsible are here with us.

What I am saying is the truth and nothing but the truth and I do not want to speak behind my colleagues� backs,` he stated.

President Kikwete, who is on a working tour of Coast Region, promised that the government would work on the problems cited.

My Take:

a. Ni kweli sasa tuna ushahidi kuwa Mawaziri hawawasiliani na hawazungumzi. Inawezekana vipi Waziri kumtumia ujumbe Waziri mwingine mbele ya Rais tena hadharani?

b. Inapotokea kuwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi inafanya kazi za Wizara ya Miundo Mbinu na ile ya Nishati basi tuna matatizo

c. Inapotokea kuwa jina la mtu mmoja linajitokeza mara kwa mara kwenye mambo mengine yanayoenda kombo halafu mtu huyo bado analindwa, basi tuna tatizo.

haya mambo ya kutafuta fasheni za kusema ukweli ndo yametufikisha hapa tulipo, just call a spade a spade and not...
Hapo Magufuri nakupa tano mzee,

Koool, just call a spade, exactly what it is a spade tena mbele ya hadhara yaani mambo hadharani, ndio hasa tunayoyataka yaani mchana kweupeee!
 
Magufuli ndio zake mbona! Hamkumbuki jinsi alivyowashitaki kwa raisi wetu Mkapa katika awamu iliyopita, wale vigogo waliokuwa wanasuasua kulipia nyumba zetu walizokuwa wamejiuzia kwa bei ya madafu? Kufumba na kufumbua mara moja wakalipa. Nahisi hata hii aliyowachomea utambi kwa Kikwete lazima wahusika watatia akili na kurekebisha pale ambapo Magufuli anapalalamikia.
Hali kadhalika mumkumbuke Magufuli awamu iliyopita pale ambapo aliwanyang'anya mashangingi wale mawaziri waliokuwa wameyasajili kwa namba binafsi badala ya namba rasmi za sirikali. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa namba mpya za magari ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili toka nje ya nchi (DFP), yaani Donor Funded Projects.
 
Mimi nashauri tuangalie suala hili kwa umakini zaidi. Yafuatayo ndiyo NHC wanavyosema juu ya mradi wa nyumba zao Mbweni:

MBWENI - DAR ES SALAAM:

Currently, the NHC is constructing two types of houses for sale at its Mbweni JKT estate, which is close to the Ocean beach. The estate is about 35 kms from Dar es Salaam City centre. The types of houses that are being constructed in this estate are up-market bungalow and double storey houses. These houses are constructed in medium density plots. The estate is serviced with fully developed on- and off-site infrastructure that includes water, electricity and estate roads. The following are the particulars for the said houses:

(i) Double storey House (Type MB1):
The ground floor of the house consists of a sizeable sitting-room, dining-room, one en-suite bedroom, kitchen, store, carport, toilet and bathroom. The first floor consists of a bathroom, toilet and three bedrooms one of which is en-suite. The size of the house is 420m2.The sale price of the house is TShs 140,000,000.

(ii) Bungalow (Type MB5):
The house consists of three bedrooms one of which is en-suite, sitting–room, dining–room, kitchen, store, carport, toilet and bathroom. The size of the house is 203m2. The sale price is TShs 72,000,000.

The terms and conditions of the sale for both the double storey and bungalow houses are as follows:

(i) Down payment is 50% of the sale price of the house.
(ii) The balance has to be paid within one year from the date of effecting the down-payment on quarterly equal installment.

You may approach the banks with which we have understandings to provide housing loans to our house buyers. These banks include CRDB Bank, Azania Bancorp and International Commercial Bank.

Huu ni mradi wa biashara na hizo nyumba zinauzwa kibiashara. Developer yeyote anapoamua kufanya maendelezo anaangalia sehemu itakayompa manufaa zaidi. Mantra yao ni location,location and location. Wakichagua sehemu isiyo na infrastructure ni kwamba wameishaziingiza katika gharama zao na wanaamini kuwa wateja watakubali kulipa ( nyumba na maelezo ya infrastructure) kutokana na location. Makubaliano haya yote yanafanyika kabla ya kuanza development. Kwa wenzetu hauanzi development yeyote kabla hujaweka infrasture hata kama unaweka mwenyewe maana hii itakupunguzia gharama za ujenzi na kuongeza mvuto wa nyumba zako. Kwa hali hiyo NHC wanatakiwa waongee na Dawasco na Tanesco na kuhakikishiwa kimaandishi kuhusu upatikanaji wa huduma hizo kabla ya kuanza ujenzi. Sasa wao wameeleza kwenye tovuti yao kuhusu mradi wa Mbezi kuwa huduma hizo ZIPO itakuwaje leo wazilalamikie wizara mama na sio mashirika kwa kutotimiza miadi? Wateja walionunua nyumba wakiamini kuwepo kwa huduma hizo wanahaki ya kushitaki NHC kwa kudanganywa. NHC nao vile vile wana haki ya kuwashitaki Tanesco na Dawasco, kama palikuwa na makubaliyano ya awali na wao hawakutimiza. Huwezi kuilaumu wizara kwa kutokukujengea barabara kama haikuwa katika mipango yake. Kama walikuahidi watakuwekea barabara, nao ni kuwashitaki wakurudishie gharama zako.Kuhusu kubambika bill, hii ni kawaida ya mashirika yetu ya huduma. Dawa ni kukataa kulipa na kuwapeleka mahakamani. Inabidi tuanze kuheshimu mikataba na kufanya kazi kitaaluma.
 
This is mutiny! Simply what Magufuli has done is to declare to the nation that The Cabinet and President have no interest with Wananchi.

Kama amediriki ku"ropoka" hivyo kwenye umati wa watu, inamaana hana imani na Kiranja Mkuu na ujumbe huu haukuwa kwa Chenge au Kawambwa bali ni kwaahisi!

Inabidi JK ajihoji nafsi kama kweli yeye ndiye kiongozi makini na kaui zake kuwa ataanza kutimiza ahadi alizotoa miaka mitatu iliyopita!
 
Kwa maelezo ya Fundi Mchundo hapo juu, inamaanisha kwamba haya malalamiko ya Bw Makufuli hayana msingi wowote. Kwamba NHC imeingia gharama si kwa sababu mawaziri wameshindwa kazi, bali kwa kuwa wanataka nyumba walizojenga ziuzike, ni biashara. Na moja ya gharama ya kuzifanya nyumba hizo ziwe bora ni huko kuweka umeme, maji nk. Wangeweza kusubiri ratiba za wizara hizo za kuweka hizo huduma, lakini wao wenyewe NHC wakaona waingie gharama wenyewe ili mradi wao "usidode". Kwa hiyo ni choice, au siyo? Kumbe pengine Makufuli, licha ya uchapaji kazi wake uliotukuka, hakupaswa "kuwaumbua" mawaziri wenzake mbele ya kadamnasi, kweli au si kweli?
 
Back
Top Bottom