Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,939
- 6,848
Kwa maelezo ya Fundi Mchundo hapo juu, inamaanisha kwamba haya malalamiko ya Bw Makufuli hayana msingi wowote. Kwamba NHC imeingia gharama si kwa sababu mawaziri wameshindwa kazi, bali kwa kuwa wanataka nyumba walizojenga ziuzike, ni biashara. Na moja ya gharama ya kuzifanya nyumba hizo ziwe bora ni huko kuweka umeme, maji nk. Wangeweza kusubiri ratiba za wizara hizo za kuweka hizo huduma, lakini wao wenyewe NHC wakaona waingie gharama wenyewe ili mradi wao "usidode". Kwa hiyo ni choice, au siyo? Kumbe pengine Makufuli, licha ya uchapaji kazi wake uliotukuka, hakupaswa "kuwaumbua" mawaziri wenzake mbele ya kadamnasi, kweli au si kweli?
Hapana, Mheshimiwa Kithuku. Nilichokisema ni kuwa ilibidi NHC kama developer (ukiangalia bei ya nyumba zao, hawafanyi charity hawa mabwana) kuingia mikataba na watakaowapatia huduma wanazohitaji katika mradi wao. Si kungoja mpaka hayo mashirika ( si wizara) yatakapopanga kwenye ratiba zao. Hii ni biashara, NHC kwa kufanya hivi anawaletea wateja na ndio maana ilibidi hizo utility companies zichangamkie tenda. Kama NHC akiona wanazembea anaingia nao mkataba wa kuwafanyia yale wanayotakiwa kuyafanya ili mradi watamrudishia gharama zake au atafute njia mbadala za kupata hizo huduma. Unajua mtu unaweza kujenga nyumba ambayo inajitolesha kwa mahitaji yake ya umeme? Unaweza kuvunamvua, kuchimba visima ili uondakane na hao Dawasco. Mipango ya barabara kuu ni ya wizara na manispaa lakini feeder roads si jukumu lao.
Hivi, mkuu, unadhani kipi kingewastua zaidi hao Tanesco na Dawasco kati ya kuletewa barua ya madai na mawakili wa NHC na hili la kutajwa kwenye jukwaa la siasa? Mimi sizungumzii uchapa kazi wa mheshimiwa Waziri, ninachozungumzia ni hili suala ambalo kwa upeo wangu finyu naona lingeshughulikiwa tofauti. Kwa kufanya hivi walivyofanya tunawapatia sababu viongozi wa mashirika yetu kudai kuwa walikuwa wanatimiza maagizo ya waziri. Mimi naamini waziri anatakiwa kusimamia sera na si utendaji wa kila siku wa shirika. Management wapewe full responsibility ya kutekeleza sera na pale wanapozembea washughulikiwe.