Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 672
Magufuli awashtaki wenzake kwa JK
2007-12-08 09:07:03
Na Mashaka Mgeta, Chalinze
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Bw. John Magufuli, amewashtaki mawaziri wenzake kwa Rais Jakaya Kikwete, kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao.
Tukio hilo lilitokea jana, kabla ya Rais Kikwete, kuhutubia mkutano uliofanyika katika kijiji cha Bwilingi, Chalinze mkoani Pwani, ambapo alizindua nyumba za ghorofa, zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Mawaziri waliohusika katika kadhia hiyo, baada ya Bw. Magufuli `kuwaumbua` katika mkutano huo ni Bw. Andrew Chenge (Miundombinu) na Dk. Shukuru Kawambwa (Maji).
Bw. Magufuli, amefikia hatua hiyo siku chache, baada ya asasi ya Mpango wa Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (REDET), kutoa taarifa ya utafiti ambayo pamoja na mambo mengine, ilionyesha kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wasioridhishwa na utendaji kazi wa mawaziri.
Katika hafla ya jana, Bw. Magufuli, alianza kuishutumu Wizara ya Miundombinu, inayoongozwa na Bw. Chenge, kuwa imeshindwa kuboresha miundombinu inayoelekea katika maeneo yaliyotumika kwa ujenzi wa nyumba za NHC.
``Mheshimiwa Rais, Shirika la Nyumba la Taifa limejikuta linaingia gharama kubwa katika kuboresha miundombinu, iliyopaswa kushughulikiwa na wizara husika, lakini wameshindwa kutekelea wajibu wao huo,`` alisema.
Wakati akisema hayo, Bw. Chenge aliyehudhuria mkutano huo, alikuwa akimtazama Bw. Magufuli na baadaye kuelekeza macho yake kwa Rais Kikwete.
Bw. Magufuli, aliyeonekana kujiamini katika kutoa madai hayo, alitoa mfano wa miundombinu iliyogharamiwa na NHC, ni barabara, njia za maji na nguzo za umeme.
Aidha, alisema Wizara ya Maji inayoongozwa na Dk. Kawambwa, ambaye pia alikuwapo mkutanoni hapo, imeshindwa kufikisha huduma ya maji katika maeneo yenye nyumba hizo.
Bw. Magufuli, alitoa mfano kuwa, NHC ilitumia zaidi ya Sh. bilioni 1.4 kugharamia miundombinu kuelekea katika nyumba 213 zilizopo Boko na zaidi ya Sh. milioni 451 kwa nyumba zilizopo Mbweni, jijini Dar es Salaam.
Pia alisema zaidi ya Sh. bilioni moja zilitumika kwa ujenzi wa barabara ya kuelekea katika nyumba za Boko, na Sh. milioni 84 zilitumika kununulia transfoma, nguzo na nyaya za umeme.
Bw. Magufuli, alisema licha ya Wizara ya Maji kushindwa kufikisha maji katika eneo hilo, DAWASCO imeanza kuwatoza wapangaji wake Ankara za matumizi ya maji.
``Ninasema kwa uwazi Mheshimiwa Rais, na mawaziri wenzangu wapo hapa, siwateti wala siwachongei kwako, ninachokisema ni ukweli mtupu,` alisema na kusababisha watu waliokuwapo kumshangilia.
Hata hivyo, Rais Kikwete, alisema tofauti zilizojitokeza miongoni mwa mawaziri hao, zinastahili kusuluhishwa kwa njia ya kukutana na kuzungumza.
Rais Kikwete, alisema ikiwa mawaziri hao watakutana na kuzungumza kwa undani kuhusu mgawanyo unaopaswa kufanywa kuhusiana na gharama hizo, kuna uwezekano wa kupata suluhu.
Aidha, Rais Kikwete, aliwataka viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kupima maeneo ya Chalinze, na sehemu nyingine wilayani humo, ili yawe kivutio kwa makazi bora na kuinua thamani ya ardhi yake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Martin Madekwe, alisema majengo hayo yaligharimu Sh. 822,920,000, zilizotokana na mapato ya Shirika hilo.
Alisema wakati ujenzi wa nyumba hizo ukiendelea, NHC imepokea maombi 47 ya wapangaji, idadi ambayo ni mara tatu ya uwezo wa nyumba hizo.
SOURCE: Nipashe