Ndugu zangu Watanzania sote tunakumbuka kuwa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dr.John Pombe Magufuli lilipotangazwa ulikuwa ni mshindo mkubwa Nchi nzima!
Kwanza katika historia ya Nchi yetu Baraza hilo lilichukuwa muda mrefu kuundwa hadi kutangazwa! Na hata baada ya kuundwa Mawaziri hao walianza kazi (sema mbwembwe) kwa kasi ya ajabu (speed of light).
Kadri muda unavyosonga naona kasi inapungua kwa kasi ya ajabu na sasa linakwenda kuanguka kama "free fall object"!
Wale Mawaziri wetu kama Dr.Hamis Kigwangala ambao pamoja na kuapishwa jumamosi hawakusubiri hata jumatatu ifike wakaripoti ofisini wakapate status ya Wizara wao wakaelekea Amana Hospitali kuanza kazi ! Na hata walipofika Wizarani walichofanya ni kukimbia kufunga Mageti,wako wapi hawa!?
Yuko wapi Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi na uvaaji wake wa "ajabu ajabu" wa Maskafu,Makombati ya JKT na Vifulana vya Bendera ya Taifa kana kwamba eti hiyo ndo alama ya Uzalendo! Zile ziara zake za ajabu ajabu pale vingunguti usiku wa manane kukagua mbuzi wanaochinjwa bila vibali ziliishia wapi!?
Eti Waziri anamuuliza Afisa soko alipotunza jenereta ya soko pale Mwaloni Mwanza! Yuko wapi!? Sukari ni Chakula na Bodi ya Sukari iko chini ya Wizara yake lakini Waziri kimya wala husikii anachosema Mchumi wetu daraja la kwanza! Mwigulu Lameck Nchemba Madelu uko wapi?!
Kila Waziri ilikuwa angalau asikike mara moja kwa siku,awe ama amemtumbua mtu au amefanya ziara ya kushitukiza mahali fulani! Sasa wamekuwa kimya! Najua Bunge la Budget linaendelea lakini pia wengi wenu hamwonekani!
Mbaya zaidi naona tangu Kitwanga ametwangwa no ametumbuliwa na "Swaiba" wake ndo kabisa Mawaziri wetu mmenywea kabisa ! Tatizo ni nini!?