Mawaziri wa nchi ofisi ya Rais, makamu wa Rais n.k wanafanya nini?


Kiwi

Kiwi

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
1,029
Likes
252
Points
180
Kiwi

Kiwi

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2009
1,029 252 180
Heshima zenu wanajamvi,

Ningependa kufahamishwa kazi za mawaziri wa nchi kwenye ofisi za Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni zipi? Ama ni njia mojawapo inayotumika kuwapa vyeo mlolongo wa watu na kuongeza gharama za utendaji kazi wa serikali? Mimi ninavyoelewa waziri anaongoza wizara. Hizo zenyewe ziko nyingi kupita uwezo mdogo wa kifedha tulio nao nchini kwetu, pamoja na kwamba karibu kila wizara ina naibu waziri. Hiyo kama haitoshi, bado tuna mawaziri wa nchi kwenye ofisi za wakuu wa nchi. Wanafanya kazi gani? Pamoja na kwamba kuna namna inayotumika kuwapa 'kazi' mfano Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji) Mary Nagu. Hivi kweli tunahitaji waziri wa kuwezesha na kuwekeza?

Ama kweli tuliambiwa kuichagua ccm ni kujitakia maafa, naam twafa!
 

Forum statistics

Threads 1,236,902
Members 475,327
Posts 29,271,842