Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

jamani kununua au kujenga nyumba sio lazima iendane na mshahara wako na sio lazima mtu atoe cash, si kuna mikopo inatolewa na bank? hamjui hawa watu kabla ya kua mawaziri walikua wanafanya biashara gani sio kila waziri alikua maskini kabla hajapewa huo uwaziri...
 
Kumbe ana nyumba nyingine tena! Mi nyumba ninayoijua iko barabara ya Njiro kabla ya Tiger Supermarket upande wa kulia wa barabara inayoelekea Njiro. Hii ndiyo nyumba aliyokuwa akiishi na Faraja Kota yule mlimbwende wetu wa Tanzania

Mungi nafikiri mheshimiwa Nyalandu alikuwa amepanga nyumba ya NHC maeneo hayohayo unayoyataja jirani na supermarket ya Tiger upande wa kulia wa barabara inayoelekea Njiro kabla ya kujenga kwake maeneo ya Sanawari ya juu mkuu
 
Nyalandu usiwasikilize hawa wote ni wachumia matumbo wanaosubiri sema hawajapata fursa tu. kuna mtu kule kwenye thread ya kigwangalla amepost majumba ya fahari na magari ya zitto kabwe naye ameyatoa wapi? naona homeboy wangu zitto naye anachangamka, mjanja sana, safi. kuleni nchi vijana msiwasikilize hawa
 
Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)

Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!

Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.
Mimi hata sioni cja jabu hapa. Kwani bosi wao hajui? Na usalama wa taifa hawjui? Hili ni tatizo la mfmo. Na bado kidogo wataanza kutuchinja na kutula nyama.
 
Hili jumba la Bw. Nyalandu nilifanikiwa kuliona mwaka huu wakati Bw. Nyalandu na Mkewe Faraja Kota walipokuwa Arusha mwanzoni mwa mwaka huu. Jamani kila mtu anapenda raha kwa kweli, ukiwa na jumba kama lile ni sawa na kuwa peponi hapa hapa Tz!
 
amenunua flats za benki zote pale singida mjini barabara ya kuelekea mwanza na ameshazifanyia marekebisho.
 
huyu jamaa nyalandu sio kiongozi kabisa maana tangia awe waziri sioni cha maana alichowahi kufanya zaidi ya tetesi kibao za kashfa naona angekuwa msanii tu ingependeza sanaaa
 
Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)

Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!

Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.

Mkuu si kama hawajui, wanajua fika tena wanajua zaidi ya unayojua wewe. Lakini huo ni mchezo tu wa kutugeresha mimi na wewe. Mwenyekiti wa kijiji akinunua pikipiki atafuatiliwa sana aeleze amepata wapi hela ya kununulia pikipiki, lakini waziri haguswi. Believe me wote hao kina Maige, Nyalandu, Ngeleja hakuna atakayefanywa kitu.

Mfano mzuri wezi wa EPA wote wanajulikana lakini serikali ilisema haiwajui, Richmond wezi wanajulikana, Kagoda same. Kwa hiyo still it will be same story, hawatafanywa kitu. This is Tanzania.
 
Weka picha basi.... kwa nini tuandikie mate wakati wino upo? Hii kitu ni hatari sana jamani wana JF mwenye picha tafadhali....
 
Hivi watanzania lini tutaendelea?, mlitaka waziri asijenge?, je, mtampangishia nyumba katika maisha yake yote hata akiwa nje ya uongozi? Acheni wivu wa kike. Naomba mawaziri wote wajenge majumba ya zaidi ya shilingi Bn 3 ili wachonga midomo wachonge zaidi hadi midomo itanuke.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
Wivu wa kike ndo nini?umeambukizwa na Mh,Dr. mkapa nakumbuka watu walipolalamikia Mh.Sumaliye kununua lanchi za serikali alitumia neno hilo hilo.Hivi mnaufahamisha umma wa watanzania kuwa wake zenu wana wivu?? kama ndivyo achaneni na nyumba ndogo na wake zenu watapona ugonjwa wa kuwa na wivu.
Kinachozungumzwa hapa ni kuhujumu uchumi wa nchi kwa kutumia madaraka waliyopewa na wananchi.Kama ni wivu ni wafanyabiashara wangapi tanzania wana majumba mazuri na hakuna anayejishughulisha na mambo yao? Tunachokataa ni hawa mawaziri wetu kuimba wimbo kuwa tanzania ni masikini na wakipewa misaada ya kuwasaidia watz wanaitumia kwenye mambo yao binafsi.
 
Hivi watanzania lini tutaendelea?, mlitaka waziri asijenge?, je, mtampangishia nyumba katika maisha yake yote hata akiwa nje ya uongozi? Acheni wivu wa kike. Naomba mawaziri wote wajenge majumba ya zaidi ya shilingi Bn 3 ili wachonga midomo wachonge zaidi hadi midomo itanuke.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".

Ondoa AVATAR yako hiyo kutokana na RED, kwenye blue katoe kwa masikini ndivyo tunafundisha makanisani, kana dini yako kisha rudi
 
Back
Top Bottom