Mawaziri wa JK waliolazimishwa kujiuzulu kwa kashifa mbalimbali hakuna anaestahili kushitakiwa?


S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
33,765
Points
2,000
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
33,765 2,000
Tangu Raisi Kikwete aingie madarakani teyari kuna idadi kubwa ya mawaziri walioshinikizwa kujiuzulu au kulazimika kutemwa katika baraza la mawaziri kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwemo wizi,ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.Kinachonishangaza na pengine kuniumiza mimi kama mlipa kodi ni kuwa sidhani kama kuna awamu iliyowahi kuendesha semina elekezi za kumwaga na katika mahoteli ya kifahari kama awmu hii.Semina hizo elekezi zililenga kuwajengea uwezo viongozi na watendaji mbali mbali serikalini wakiwemo mawaziri.Hata hivyo,hakuna awamu iliyokithiri kuwa na viongozi na watendaji wa bovu kama hii ya sasa.Mlolongo na orodha ya viongozi na watendaji waliokumbwa na kashifa ni ndefu kuliko maelezo.Hapa cha kujiuliza ni kuwa ina maana hawa wote tuhuma zao zilikuwa za uongo au za kisiasa tu?Kama zilikuwa ni za kweli ni kiongozi gani mwandamizi chini ya JK ameshitakiwa hata tu kwa matumzi mabaya ya madaraka?Semina hizo za mabilioni kwa viongozi na watendaji wa serikali zimeleta tija gani?Mwisho,hivi mkuu wa kaya hastahili kuingia katika kumbukumbu za dunia kwa kuwa kiongozi namba moja duniani anaengoza kwa maneno zaidi kuliko vitendo?
 

Forum statistics

Threads 1,284,961
Members 494,371
Posts 30,846,038
Top