Xuma
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 683
- 196
Mawaziri wa JK wagongana
na Asha Bani
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ametofautiana na Waziri mwenzake wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Thereza Huviza, akipinga hatua yake ya kuzifungia hoteli mbili za kitalii jijini Dar es Salaam.
Wiki iliyopita, Waziri Huviza alizifunga hoteli za Double Tree iliyoko Masaki na Giraffe Ocean View iliyoko Kunduchi kutokana na kutotekeleza maelekzo ya wizara pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEC) na hivyo kuendelea kutiririsha maji taka baharini.
Akizungumza na Tanzania Daima, Waziri Kagasheki alisema kama wizara wameshtushwa na hatua hiyo ambayo aliita kuwa haikuzingatia sheria wala haki ya wawekezaji wa hoteli hizo.
Balozi Kagasheki alifafanua kuwa, hatua ya kufunga hoteli hizo haraka kiasi hicho haina maslahi kwa taifa.
Aliongeza kuwa, Waziri Huviza kabla ya kuchukua hatua, alipaswa kuwashirikisha Wizara ya Utalii, lakini cha kushangaza uamuzi huo ameufanya peke yake bila kujali kuwa kuna madhara gani kwa sekta ya utalii nchini.
Unajua ni uamuzi hatari sana na finyu wenye haraka, kwanza alitakiwa kuangalia ni wakati gani ambao anafanya uamuzi huo. Hiki ni kipindi cha likizo, ameshindwa kujua kweli kwamba wageni wengi wanapaswa kuja nchini? alihoji.
Waziri Kagasheki alisisitiza kuwa, uamuzi huo hauungi mkono hata kidogo, kwamba waziri mwenzake ameshindwa kuzingatia kuwa hoteli zile ni za kitaifa ambapo katika kipindi hiki cha likizo wageni wengi wanatarajia kuingia nchini.
Aliongeza kuwa, hata mataifa ya nje na kwenye mitandao yao suala hilo limeingizwa na yanasomwa, na watalii wengi waliopanga kuja kutembelea Tanzania watashindwa kuja.
Alisema mikakati ya wizara ni kuhakikisha kuwa wanafanya kampeni za kuongeza watalii nchini, lakini endapo kutakuwa na mambo yanayokinzana, ni lazima watashindwa kufanikiwa kwa hilo. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Giraffe Ocean View, Nicholas Rabilo, alisema tayari wameanza kupata madhara kwani watalii kutoka Ujerumani waliokuwa wameomba nafasi ya kukaa hapo kwa mapunziko kwa wiki mbili, sasa wameahirisha.
Alisema hasara nyingine ni watu wa Kampuni ya simu ya TTCL waliokuwa na sikukuu ya familia kwa watu 100 ambao wameahirisha pamoja na Fair Competition wenye watu 50 na vile vile wameahirisha.