Mawaziri wa JK wagongana

Xuma

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
683
196
Mawaziri wa JK wagongana

na Asha Bani

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ametofautiana na Waziri mwenzake wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Thereza Huviza, akipinga hatua yake ya kuzifungia hoteli mbili za kitalii jijini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita, Waziri Huviza alizifunga hoteli za Double Tree iliyoko Masaki na Giraffe Ocean View iliyoko Kunduchi kutokana na kutotekeleza maelekzo ya wizara pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEC) na hivyo kuendelea kutiririsha maji taka baharini.

Akizungumza na Tanzania Daima, Waziri Kagasheki alisema kama wizara wameshtushwa na hatua hiyo ambayo aliita kuwa haikuzingatia sheria wala haki ya wawekezaji wa hoteli hizo.

Balozi Kagasheki alifafanua kuwa, hatua ya kufunga hoteli hizo haraka kiasi hicho haina maslahi kwa taifa.

Aliongeza kuwa, Waziri Huviza kabla ya kuchukua hatua, alipaswa kuwashirikisha Wizara ya Utalii, lakini cha kushangaza uamuzi huo ameufanya peke yake bila kujali kuwa kuna madhara gani kwa sekta ya utalii nchini.

“Unajua ni uamuzi hatari sana na finyu wenye haraka, kwanza alitakiwa kuangalia ni wakati gani ambao anafanya uamuzi huo. Hiki ni kipindi cha likizo, ameshindwa kujua kweli kwamba wageni wengi wanapaswa kuja nchini?” alihoji.

Waziri Kagasheki alisisitiza kuwa, uamuzi huo hauungi mkono hata kidogo, kwamba waziri mwenzake ameshindwa kuzingatia kuwa hoteli zile ni za kitaifa ambapo katika kipindi hiki cha likizo wageni wengi wanatarajia kuingia nchini.

Aliongeza kuwa, hata mataifa ya nje na kwenye mitandao yao suala hilo limeingizwa na yanasomwa, na watalii wengi waliopanga kuja kutembelea Tanzania watashindwa kuja.

Alisema mikakati ya wizara ni kuhakikisha kuwa wanafanya kampeni za kuongeza watalii nchini, lakini endapo kutakuwa na mambo yanayokinzana, ni lazima watashindwa kufanikiwa kwa hilo. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Giraffe Ocean View, Nicholas Rabilo, alisema tayari wameanza kupata madhara kwani watalii kutoka Ujerumani waliokuwa wameomba nafasi ya kukaa hapo kwa mapunziko kwa wiki mbili, sasa wameahirisha.

Alisema hasara nyingine ni watu wa Kampuni ya simu ya TTCL waliokuwa na sikukuu ya familia kwa watu 100 ambao wameahirisha pamoja na Fair Competition wenye watu 50 na vile vile wameahirisha.

Mawaziri wa JK wagongana
 
hawa nemc nao hawana akili,jee waliwapeleka wataalamu wao ili washirikiane na wenye hotel kurekebisha kasoro?
 
hawa nemc nao hawana akili,jee waliwapeleka wataalamu wao ili washirikiane na wenye hotel kurekebisha kasoro?

Soma thead vizuri mkuu. Wamefungiwa kwa "kutotekeleza maagizo waliyopewa" Hii inamaanisha walishapewa maagizo wakakaidi kama kawaida ya wawekezaji wetu waliozoea kuwaweka mfukoni viongozi wetu.

Kagasheki hapa waweza kuta anatetea maslahi flani.
 
huyu Kagasheki ni mpuuzi, yani yeye anaona watalii ni muhimu sana kuliko mazingira na afya yetu kwa ujumla??
kwa iyo mazingira yaendeleee kuchafuliwa kwa sababu ya wazungu??
ni migahawa mingapi midogo inayofungiwa kwa kushindwa kukidhi vigezo vya mazingira??
Kagasheki ana akili za funza kama huyo aliemteua.
 
Haya ndiyo matatizo ya Mitanzania Viongozi, unangalia mapato bila kuona madhara yake kwa taifa hilo hilo kimanzingira, usalama wa watu, mimea na viumbe hao wengine wote.

Kama walipewa maagizo na kutakiwa kuyatekeleza kwa wakati lakini hawakufanya hivyo, wenye hotel walitegema nini? Ndiyo maana kila eneo Taifa hili linashindwa kusnga mbele, ni kwa sababu kama hizi wanasiasa kutozingatia maadili ya kazi zao kama walivyo apa, sheria za nchi, kutoheshimu maamuzi na ushauri wa watalaam wa taasisi au wizara zao! Kagasheki umekurupuka, acha Sheria ichukue mkondo wake kama unavyo himiza kwenye vyombo vyako vya habari. Mtoto akifanya kosa usiache kumadhibu kisa atalia na pengine anaweza kuugua na akatakiwa kumtibisha (maan ya kupta hasara kwa namna moja au nyingine). Tibu tatizo, ndiyo maana watanzania wanawaona nyinyi viongozi kama fagilia na kutanguliza masilahi yenu!
 
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ametofautiana na Waziri mwenzake wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Thereza Huviza, akipinga hatua yake ya kuzifungia hoteli mbili za kitalii jijini Dar es Salaam. .....Akizungumza na Tanzania Daima, Waziri Kagasheki alisema kama wizara wameshtushwa na hatua hiyo ambayo aliita kuwa haikuzingatia sheria wala haki ya wawekezaji wa hoteli hizo.

"Unajua ni uamuzi hatari sana na finyu wenye haraka, kwanza alitakiwa kuangalia ni wakati gani ambao anafanya uamuzi huo. Hiki ni kipindi cha likizo, ameshindwa kujua kweli kwamba wageni wengi wanapaswa kuja nchini?" alihoji.

Waziri Kagasheki alisisitiza kuwa, uamuzi huo hauungi mkono hata kidogo, kwamba waziri mwenzake ameshindwa kuzingatia kuwa hoteli zile ni za kitaifa ambapo katika kipindi hiki cha likizo wageni wengi wanatarajia kuingia nchini.
huyu Kagasheki ni mpuuzi, yani yeye anaona watalii ni muhimu sana kuliko mazingira na afya yetu kwa ujumla??
kwa iyo mazingira yaendeleee kuchafuliwa kwa sababu ya wazungu??
ni migahawa mingapi midogo inayofungiwa kwa kushindwa kukidhi vigezo vya mazingira??
Kagasheki ana akili za funza kama huyo aliemteua.

Kagasheki why are you too pretentious? Can't you work and say these all through the power hierarch in your cabinet meetings? I hate this kind of Politicians who like to buy public attention for no action. Politicians who work through media by giving tough and ambiguous statements against the branches of the tree on which they have sat! if you connect this new statement with what Kagasheki has so far done in his previous statements immediately you realize Kagesheki to be the empty drum beat or a paper tiger. Can someone tell us what has come out of the Twiga Statement, Vifaru Statement, Pembe za Ndovu Statement, etc? NOTHING!

He has applied the same character to disturb the political stability and cohesion in the Bukoba Municipality as reported hereunder: Waziri Kagasheki, Meya waipasua CCM Kagera - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Namuunga mkono Kagasheki,kama kuna matatizo Wizara ya Utalii ingeshirikishwa kufikia muhafaka na hatua sahihi kuchuliwa. Kilichofanyika ni kuzikomoa hizi hoteli ktk kipindi hiki muhimu kibiashara.
 
Namuunga mkono Kagasheki,kama kuna matatizo Wizara ya Utalii ingeshirikishwa kufikia muhafaka na hatua sahihi kuchuliwa. Kilichofanyika ni kuzikomoa hizi hoteli ktk kipindi hiki muhimu kibiashara.

Kagasheki angeisoma sheria ya mazingira, au angalau angekuwa anafuatilia matukio kwenye vyombo vya habari.

Hivi nyinyi watz munataka hawa jamaa waachiwe wamwage uchafu kwenye bahari ya hindi halafu nyinyi muende kuogelea? Nani atapata madhara, unadhani huyo mwekezaji anajali?

Mama Terezya endelea nao hao, wakipewa maelekezo wanadharau lakini wakiona hatua muafaka imechukuliwa itakuwa funzo kwa wengine.
 
Roho mbaya tu hakuna issue hapo,kuna mengine yamejificha nje ya sababu za kitoto anazotoa huyo Terezya!
 
Pale wageni wanapothaminiwa bila kujali athari za Mazingira.
Kwamba hizo hoteli mbili ndizo pekee na spesho kwa wageni?

Namshangaa Kagasheki.

Anataka tuendelee kuogelea kwenye m*v* ya wazungu, kisa pesa, pesa yenyewe ikipatikana inapelekwa uswis.

Hivi waziri mzima anaweza kutoa kauli kama hii kweli,? Ni kwa nini viongozi na wasomi wetu huwa wanaongea pumba kiasi hiki? Hii hata nikimwambia mwamangu 7yrs old lazima ashangae.
 
Kagasheki, typical Tanzanian leader! Mara zote wanasimamia maslahi ya wawekezaji bila kujali maslahi ya wazawa. Anaona waziri mwenzake kafanya "uamuzi finyu" kwa kuzifunga hoteli hizo, huku akitambua kuwa yeye ndiyo ana upeo finyu kwa kuwakumbatia wawekezaji hata kama wanashindwa au kupuuzia kutekeleza maagizo halali ya mamlaka halali za serikali, kweli kazi tunayo na hawa mawaziri wa JK, pesa mbele!..tena afadhali pesa hizo tungeona zikichangia maendeleo vijijini, kinyume chake wanachafua mazingira na kuhatarisha afya za maskini!...puuuuuu.
 
Bora Punda afe mzigo ufike! Hapa naona kagasheki insider box thinker!
 
Namuunga mkono Kagasheki,kama kuna matatizo Wizara ya Utalii ingeshirikishwa kufikia muhafaka na hatua sahihi kuchuliwa. Kilichofanyika ni kuzikomoa hizi hoteli ktk kipindi hiki muhimu kibiashara.

Hatua sahihi ni zipi, kama walishapewa maagizo hawajatimiza? Unajua mazingira yanayoharibika ni yetu sote? Unafikiri hela wanazokusanya ni zetu sote? Acha u CCM wako"
 
Roho mbaya tu hakuna issue hapo,kuna mengine yamejificha nje ya sababu za kitoto anazotoa huyo Terezya!

Acha utoto' sababu alizosema ni "wachafu mazingira kwa kutiririsha maji machafu baharini" ungesema sio kweli ungeeleweka" acha u CCM wako!
 
Hivi kweli ndivyo jinsi viongozi wetu wanavyofikiri,Anawaaibisha sana viongozi huyu Kagasheki. Aisee! Nafikiri haya mambo yanafanyika kiurafiki zaidi. Tunaitaji maisha bora,maisha hayaji bila afya bora. Wanatia hasira sana viongozi wa namna hii

Hivi waziri kama huyu tunamuondoaje madarakani? Ki ukweli hatufai sasa tunaanzia wapi? Au yanaishia hapa kijiweni tu? Hawa jamaa watatuua!
 
Back
Top Bottom