Mawaziri wa JK: Ngeleja na apartment ya $350,000

KUna mwalimu wangu mmoja wa chuo kikuu, aliwahi ksema vijana mkibahatika kushika hela, msikimbilie kuanzisha biashara za kuumuza vichwa. Wekezeni ktk Real Estate, mtakuwa mmejiwekea amana ya kipato cha uhakika kwenu na kwa vizazi vyenu milele. Na hapa naanza kuamini kwa asilimia zote.

Kwa hawa mawaziri viongozi kuwa wezi kiasi hiki si ndo wazee watapata sababu ya kusema vijana hawafai kuwa viongozi na vijana tutakuwa na sababu ya kupinga ukweli huu?

Kumbe Ngeleja ni mwizi kiasi hiki, mweeeeeee!
 
tayari kiasi kikubwa cha pesa za umma zimeibiwa na inawezekana kikazidi hawamu zote za utawala zilizotangulia. Na kibaya zaidi hawa wa sasa hivi wamejawa na dharau za kutisha.

Lakini tukumbuke hii nchi tayari ina hisitoria ya utaifishaji ambao ulifatiwa na uhujumu uchumi. Hivyo hatuwezi kukaa na kujidanganya kuwa hawa watu watakaa tu na kuisha raha mustarehe, ni lazima katika mkakati wa urudishaji wa nyumba za serikali na wenyewe wataguswa na hizo mali zao zitakuwa questioned.

Kinachotoa matumaini zaidi ni ile imani(sera) iliyokuwa imejengwa na hawa wenyewe kuwa "huwezi kupata madaraka bila pesa".
Dalili zote zinaonyesha wazi kuwa hiyo sera inaanza kushindwa na sasa tunawaona akina Kafulila, Sirinde, Nassari nk ambao ni Watanzania ambao wasingetarajiwa kuingia bungeni.

Tukae tukilitegemea hilo wote


Asante sana mkuu Invisible
 
hakuna waziri maskini labda wale wa enzi za Nyerere.
wanahonga kuwa wabunge wakijua mbeleni kuna neema
inabidi katiba iweke wazi kuwawajibisha walanguzi na mafisadi
kama tulichukua sheria za India tukaziingiza kwetu kwanini tusichukue za China kuhusu kunyonga mafisadi hadharani?
 
Hahahaaaa nadhani tukiendelea kulisaidia bunge la CDM kwa njia hii ni wazi kuwa Mawaziri na Manaibu wote wataikimbia nchi, thanks JF
 
Mgao wa Dowans.

Huyu Dogo shule yote na Experience ya Coopers and Lybrand anishia kuwa Mwizi???

This is shame.

Hivi wanajiandaa kuja kuishi huku Ughaibhuni siku ya gharika??


Hivi mbona kwenye picha hakuna Block A? mimi naona Block C ama ni kama hii?. Halafu mbona hati yenyewe yaonekana kama zile za ,miaka ya 80? wakati hii yaonekana ni ya 2010?!!!. nauliza tu isije ikawa ni Photoshop?

Lakini kama ni kweli basi TWAFA
 
Mara zote ukiona Mkuu wa Kaya anamng'ang'ania Waziri ndani ya serikali yake, ujue kuna namna sio bure. hapa ukweli unajidhihirisha kwa mara nyingine tena! Hebu tuleteeni madudu ya wengine. Two down, six more to go............!
 
As usual mke anahusishwa kwanza........wanasiasa hawajifunzi yaliyompata Mama Gbagbo

pb-110411-simone-gbagbo-2p.photoblog900.jpg
 
Watu wanasahau kuwa mwanadamu miaka yake ya kuishi duniani si mingi, hivi tungekuwa tunaishi milele hapa duniani ingekuwaje
 
Nothing personal, hivi Ngeleja ana biashara gani? Ni mkopo? Ni mshahara wake tu? Isijekuwa ni mgawo wa DOWANS...

attachment.php

attachment.php

attachment.php

Mkuu Invisible heshima mbele!

Tunashukuru kwa taarifa. Ila kutoka kwenye exhibit 1 inasomeka Block A, Apptmnt A4 na 1st floor, Sep. Title 84881/10.

Kwenye Sep. Title ni No. 84881/17 na ni Block A iliyobadilishwa kusomwa C na Apptmnt C5 Second Floor. Exhibit 2.

Na umeweka picha ya Block C kwenye Exhibit 3.

Anaweza kuwa ameuziwa mbuzi kwenye gunia. Bongo hii!
 
Hivi mbona kwenye picha hakuna Block A? mimi naona C. Halafu mbona hati yenyewe yaonekana kama zile za ,mika ya 80? wakati hii yaonekana ni ya 2010?!!!. nauliza tu isije ikawa ni Photoshop?

Lakini kama ni kweli basi TWAFA

Unadhani itakuwa photocopy ya kitu gani? we nawe akili zako, hovyooooooooooo!
 
Hii inatisha!
Lakini kama hili ndilo limefanyika kwa uwazi (Apartment 1 kwa $ 350,000/=), je yale yanayofanyika gizani????
Sasa Harry nae aje hapa atuambie kama hawa watu wanalipa kodi, kuanzia hawa mwenye majengo na hawa wanunuzi kama huyu Ngeleja na Maige
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom