Mawaziri wa JK: Ngeleja na apartment ya $350,000

Mkuu Invisible heshima mbele!

Tunashukuru kwa taarifa. Ila kutoka kwenye exhibit 1 inasomeka Block A, Apptmnt A4 na 1st floor, Sep. Title 84881/10.

Kwenye Sep. Title ni No. 84881/17 na ni Block A iliyobadilishwa kusomwa C na Apptmnt C5 Second Floor. Exhibit 2.

Na umeweka picha ya Block C kwenye Exhibit 3.

Anaweza kuwa ameuziwa mbuzi kwenye gunia. Bongo hii!
nafikiri hapo ni swala la naming tu, kuna Block ya Site, Blocks letters za majengo kama yapomengi, blocks kwa maana ya floors kisha apartments numbers, nahisi walichemka kwenye kutoa majina.
 
Hivi mbona kwenye picha hakuna Block A? mimi naona Block C ama ni kama hii?. Halafu mbona hati yenyewe yaonekana kama zile za ,miaka ya 80? wakati hii yaonekana ni ya 2010?!!!. nauliza tu isije ikawa ni Photoshop?

Lakini kama ni kweli basi TWAFA


Unadhani itakuwa photocopy ya kitu gani? we nawe akili zako, hovyooooooooooo!

hizo rangi hazifanani.
 
Du kumbe uwazil deal kila mbunge aulilie maana unalipa kama watu miaka saba tayari wana mahekalu ,watanzania tutafika kweli?
 
Mbona ni kawaida sana, nawashangaa malimbukeni, mnaokosa kujuwa kuwa hata wabunge ambao si mawaziri wana assets zaidi ya hiyo. Mtu anaeendesha gari la millioni 150 unategemea akae madongo kuporomoka?

Vibanda tu vya Kariakoo kwa sasa vinathamani zaidi ya hiyo. Wacheni ushamba.
 
Nothing personal, hivi Ngeleja ana biashara gani? Ni mkopo? Ni mshahara wake tu? Isijekuwa ni mgawo wa DOWANS...
Kamanda;

Tunakushukuru sana kwa kutuwasilishia hii nyeti!

Aibu za namna hii kwa taifa na umaskini unaotutafuna, hazina majibu sahihi zaidi ya hawa mawaziri kukamatwa na wananchi wenyewe katikati ya maandamano ya ukombozi, kama ilivyotokea Libya na Tunisia, na kupewa hukumu ya umma badala ya kutegemea utawala uliokwishakufa uwakamate, ambao wao pia wamo ndani yake! Hilo halitawezekana kamwe!! Umma tu ndio wenye majibu sahihi ya uchafu huu!...na sio rais, wala watendaji wake kama PM!

Mbona apartment yenyewe inaonekana kubwa sana ila thamani yake (US$ 350,000.00) ni ndogo kuliko kale ka-pagale alikojibambikia mdogo wake Ezekiel Maige (US$ 410,000.00) au report ya Mh Lembeli ilivyomuanika kuwa aliipiga kwa cash ya zaidi ya US$ 700,000.00? Hii ya Ngeleja imejengwaje? au under-valued ili afiche ufisadi wake?

Then Mkuu, tunakuomba uendelee kutuwasilishia:
  • Tuwekee Mawaziri na miliki zao, vitalu na majumba na miradi - ya kifisadi wakati wananchi wanajifia wenyewe majimboni.
  • Makatibu wao na watendaji wakuu.

Umma unajiandaa na kujiwekea kumbukumbu kwa ajili ya kumiliki mali zao zote hizi ambazo watawala hawa wadhoofu na wabinafsi wamewaibia tangu siku zote.
 
Hivi hiyo figure ya $350,000. 00 imetoka wapi? Manake mi siioni kwenye hizo images zilizobandikwa hapa

Huyo mleta mada kaibuni tu hiyo, lakini haelewi kuwa hata vibanda vya Kariakoo ambavyo bado havijauzwa kwa sasa vina fetch zaidi ya hizo.

Mleta mada unazijuwa nyumba za Mbowe Uingereza na Dubai? na lile jumba la Disko pale Dar unaweza kutuambia kalipataje?
 
Hivi 'Uwaziri' ni DEAL?

Deal kwao ni nafasi yoyote ile mtu anapokuwa appointee wa mnene wa Nchi,yani ungejua mkuu kuwa watu wanashindana bei za nani apate wapi mnene amteue sijui ka mnene anajua kuwa kuwa nafasi zake za uteuzi ni the highest the bidder!!
 
Azimio la Zanzibar hilo......Mwl Nyerere alipokuwa anawashangaa viongozi wengine hamkumuelewa
 
Huyo mleta mada kaibuni tu hiyo, lakini haelewi kuwa hata vibanda vya Kariakoo ambavyo bado havijauzwa kwa sasa vina fetch zaidi ya hizo.

Mleta mada unazijuwa nyumba za Mbowe Uingereza na Dubai? na lile jumba la Disko pale Dar unaweza kutuambia kalipataje?

Mbowe amewahi kuwa hata DC acha Uwaziri?
 
Back
Top Bottom