Mawaziri wa JK kama Kondoo wasiye na mwenyewe!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wa JK kama Kondoo wasiye na mwenyewe!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUMBUZI, Mar 13, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ukiwasikia mawaziri wa JK wanavyotoka kila mtu na statementi yake unaona kabisa ndani ya serikali M/kiti wa baraza la mawaziri si tu kazi imemshinda bali amepoteza udhibiti wa baraza lake na uongozi mzima wa serikali.

  Kwa mfano wakati Sofia Simba anataja CHADEMA kwa jina kwamba wanapokea misaada kutoka balozi za nje kuleta vurugu yeye Benard Membe anatumia mafumbo yasiyoeleweka kusema kitu kilekile.
  mfano mwingine ni ule wa Waziri wa afya kusitisha huduma ya Babu kule Loliondo lakini kesho yake Wiliam Lukuvi anamkana waziri wa afya na kusema hawajasitisha huduma.
  Ndugu zangu wana JF hii inatuonyesha kuna kila dalili kuwa kila waziri anatoka nyumbani kwake kutoa matamko anavyojisikia. Hakuna tena Collective statement inayotokana na makubaliano ya pamoja kama mawaziri. Nchi imekuwa kama jukwaa la vichaa kila mtu anaibuka na kuongea anavyojisikia maana yake nini?
  Hii ni dhahiri kuwa hawa mawaziri sasa wamekuwa kama kondoo wasio na mwenyewe kwani JK angekuwa in control wangeweza kutoa matamko kwa niaba ya serikali na siyo kila mmoja anatoa tamko lake. Mbaya zaidi wanatoa matamko yanayopingana huku rais badala ya kukemea yeye anabaki akilia na unstoppable CHADEMA bila mafanikio.

  What are you doing my beloved president? The country is going astray.

  Naomba sana mkuu usiruhusu after shocks za uchaguzi zikakunyima ujasiri wa kuongoza nchi hatimaye ukashindwa kumaliza kipindi chako cha pili Salama.
  Hali ikiachiwa iendelee hivi basi ujue ule mwisho wa CiCi Majizi kutawala utakuwa umefika na ni irreversible.
   
Loading...