Mawaziri wa JK hawajui chanzo cha matatizo ya wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri wa JK hawajui chanzo cha matatizo ya wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Mar 10, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Jana nilikuwa natazama taarifa ya habari TBC1 saa mbili usiku,moja ya habari zilizonivutia ni mgogoro wa ardhi wilaya ya Babati.Palikuwa na kikao kilichowashirikisha wananchi na mawaziri wa tano Dr Mary Nagu,Prof Jumanne Maghembe,Dr Matayo David na wengine wawli majina nimeyasahau.Wenyeji hawana mashamba ya kulima ardhi kubwa inashikiliwa na wahindi wenye uraia wa Uk na India.

  Mawaziri wanawasihi wananchi wasiokuwa na ardhi wasiharibu mali [mashamba,matrekta na nk] za wawekezaji wahindi wala wasiwatumie sms za kuwatisha.Kilichonishangaza zaidi hakuna waziri hata mmoja aliyekuwa tayari kukiri kwamba serekali itawatafutia ardhi sehemu nyingine au ardhi kubwa iliyogaiwa wawekezaji itapunguzwa ili wananchi wazalendo wazawa wagaiwe.Wote wanajaribu kukwepa kuzungumzia chanzo cha mgogoro ni nini.Mwananchi mmoja aliyepewa fursa ya kuzungumza aliwaambia mawaziri wakamwambie Rais hawana ardhi ya kulima sasa hivi wameongezeka sana ardhi waliyopewa wawekezaji ni kubwa ipunguzwe na kugawanywa kwa wananchi.

  Najiuliza maswali kibao bila majibu kwamba kulikuwa na haja gani kuwatuma mawaziri watano ilihali chanzo cha mgogoro uliodumu kwa miaka ishirini kinajulina ?.Hivi serekali inajua inatengeneza bomu lingine kubwa iwapo itatekeleza mpango wake wa kuwaita wawekezaji wakubwa kupora ardhi yetu kupitia sera yake ya KILIMO KWANZA?.
   
Loading...