Wakati wapenda maneno na siasa za kukosoa wakati wote, wasio ona jema hata moja wakiendelea na uchambuzi wao wa jinsi wanavyoliona baraza la mawaziri la JPM, Askari wa mwavuli wa JPM wameanza kupiga kazi kwa kasi ya ajabu. Jionee mwenyewe hapa.
Baada ya Kuapishwa tu, Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza Hospitali ya Amana
Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Khamis Kigwangala akielekea katika hospitali ya Amana leo jijini Dar es Salaa mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli.
Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Khamis Kigwangala akizungumza na wauguzi aliowakuta katika hospitali ya Amana leo alipotembelea katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wagonjwa
=============
WAZIRI KITWANGA AKARIBISHWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI MARA BAADA YA KUAPISHWA IKULU LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo mara baada ya kumpongeza Waziri huyo mpya, nje ya Ukumbi wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimkaribisha Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya waziri huyo iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia ndani ya ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto) akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D/IGP), Abdurahman Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja (hayupo pichani). Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
SOURCE: FULLSHANGWE BLOG
HAPA KAZI TU
SOURCE: FULLSHANGWE BLOG
HAPA KAZI TU