Mawaziri vivuli na wapinzani kwa ujumla igeni mfano wa Zitto Kabwe na Hashimu Rungwe

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,912
Niliwahi leta uzi hapa nikiwashauri mawaziri vivuli kutokaa kimya katika jukumu lao la kuikosa serikali na pia nilifikia hatu nikaleta uzi nikiwata wapinzani wasiwe "mzigo".

Viongozi wa upinzani acheni kuwa "mizigo"

Hata hivyo, kwa juhudi alizozianza Zitto na Hashimu Rungwe za kufunguka zinatia moyo na ninawashauri wapinzani wengine wakiwemo mawaziri vivuli kufunguka kuisaidia mawazo hii serikali na Taifa kwa ujumla.

Mkiongea watawabeza lakini nyuma ya pazi wanayafanyia kazi na kama Taifa tunasonga mbele bila kujali huyu ni CCM au UKAWA.

Kama alivyosema wapinzani tu kwa sasa ndio wanaoweza kukosoa na kushauri maana wengine wamejaa hofu na hata Lissu juzi kakari kuwa huu si wakati wa kuendelea kukaa kimya hivyo na wapinzani wengine timizeni wajibu wenu.

Mnawajibu wa kupaaza sauti kwasababu vyama vyenu vinapewa ruzuku(kodi zetu) na huu ni wajibu wenu.Kumbukeni Hashimu Rungwe hana ruzuku yoyote ila anatimza wajibu wake kama mpinzani.

Tusimjadili Zitto na mapungufu yake bali tujadili hoja za Zitto.

Yametokea mengi na mmekaa kimya kwa mengi ila sasa naona imetosha.

Pale ambapo serikali haitatekeleza mapendekezo au ushauri wenu hilo ni jambo lingine lakini nyinyi mtakuwa mmetimiza wajibu wenu na watanzania watakuwa wamewasikia.
 
Back
Top Bottom