MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Hapa namaanisha wale vijana ambao ndio wamekua amsha amsha na hamasa kubwa ndani ya CCM, hawana amani, hawkubaliani na kuonewa kwa baadhi ya watu ilihali wengine wanalindwa na kukingiwa kifua.
Kuna uwezekano kabisa vijana hawa wasikubaliane na kuzimwa kwa ndoto zao za kisiasa, kuna uwezekano nao wakamfuata kijana mwenzao ambaye kiutendaji na kiuhalali kabisa kawajibishwa pasina kosa.Hawa vijana wanatambua kua hata enzi za Mwalimu Nyerere wakati huo kina JK na EL walikua wakijijenga kisiasa na kujiimarisha kwa ajili ya kua viongozi wazuri baadaye, Vijana wa enzi hizo walipewa nafasi ya kujiimarisha na kutengeneza mitandao yao ya kuwaongezea nguvu katika harakati zao.
Wakati huo huo wakati wao wamebanwa kila kona,wapinzani wao kama kina Lissu,Lema na wengine wako tayari kulala mahabusu ili kujiimarisha kisiasa ilimradi tu umma uendelee kuwasikia. Hapa kuna hatari ya kupotezwa mtu kisiasa asipokua makini, kuna hatari kwa ndoto za watu kuzimwa enzi hizi.
Mzee JK alishaanza kuwalea na kuwanoa vijana wazuri,wasomi, wenye vyeti lakini naona jitihada hizi zimeshafifia na wanaibuka ama wanalelewa ambao wanalalamikiwa hata vyeti hawana!
Tusidanganyane kwenye vyama kikubwa na chenye wafuasi wengi mitandao ya kuutafuta uongozi wa juu haiepukii duniani kote. Mtu lazima achague wafuasi na sio yeye achaguliwe.