Mawaziri tisa wa Kikwete ni hatari-Wanatishia uchumi wa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri tisa wa Kikwete ni hatari-Wanatishia uchumi wa nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njowepo, Nov 27, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  [​IMG] Wanatishia uchumi wa nchi
  [​IMG] Kisa wanasaka urais 2015

  [​IMG]
  Zitto Kabwe

  Na Muhibu Said
  27th November 2011


  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, amesema mawaziri tisa wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wanatishia uchumi wa nchi kutokana na kuendekeza vita vya kuusaka urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa mwaka 2015.

  Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), japo hakuwataja mawaziri hao, alitoa madai hayo muda mfupi mara baada ya kufungua mkutano wa Muungano wa Vyama vya Kidemokrasia Afrika (DUA) jijini Dar es Salaam jana.

  Mkutano huo uliojumuisha vijana kutoka katika nchi 22, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) ndio wenyeji wao hapa nchini.

  "Mawaziri tisa, tunao nchini, wanaacha kufanya kazi wanaingia katika ugomvi. Mbona bado miaka minne Rais Kikwete ametoa ahadi kibao zitatekelezeka vipi ikiwa viongozi wenyewe ndio wapo katika ugomvi na wanashindwa kusimamia maendeleo ya nchi na kuiweka nchi katika sehemu nzuri kiuchumi?" alihoji Zitto.

  Zitto, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha na Uchumi, hakuwataja mawaziri hao.

  Alisema anashangaa kuona Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyokaa Dodoma hivi karibuni, kushindwa kutoa maamuzi mazito, badala yake inatoa maamuzi ya ajabu.

  Zitto alisema alifikiri maamuzi ambayo yangetolewa na CC, ni ya kuwatimua mawaziri walioingia katika ugomvi wa urais na kuteuliwa wengine ambao wanaweza kufanya kazi.

  Alisema kinachotakiwa kwa sasa kama Rais Kikwete amebakiwa na nafasi saba za viti maalum, basi awatimue mawaziri wanaotaka urais kwa sasa na awateue wengine, ambao watafanya kazi kwa ufasaha na kuinua nchi kimaendeleo.

  Zitto alisema hivi sasa uchumi wa Tanzania umeporomoka kufikia asilimia 17.

  Alisema hali hiyo imesababishwa na mawaziri hao kushindwa kufanya kazi za kujenga uchumi wa nchi, badala yake kujiingiza katika vita hivyo.

  Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kwa sasa hali ya nchi ni mbaya ukilinganisha na wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, ambao alisema uchumi ulishuka kwa asilimia 4.5.

  Hata hivyo, alisema anamshukuru Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, kwa kukiri kuchafuka kwa hali ya hewa ndani ya chama hicho kwamba, kunatokana na mbio za urais wa mwaka 2015.

  Alisema Mukama alisema kuchafuka kwa hali hiyo ndani ya kumesababisha kuwako kwa makundi makubwa mawili yanayopingana.

  Zitto alisema kutokana na kauli hiyo, CCM imepoteza nguvu, huku mawaziri wake hao kila mmoja macho yake yapo katika urais kiasi cha kuingia katika ugomvi na kuacha kufanya kazi za kuimarisha uchumi wa nchi unaoyumba kwa kiasi cha kutisha.

  Alisema kama mawaziri wameingia katika ugomvi wa kutaka nafasi ya urais, ni dhahiri kwamba, hakuna waziri atakayesimamia maendeleo ya nchi hasa kwenye madini, umeme na kudhibiti tatizo la kushuka kwa shilingi.

  Zitto alisema hali hiyo ni hatari hasa kwa taifa linaloendelea.

  Kuhusu kauli ya CCM kutaka vyama vingine viungane na Chadema katika kumuona rais, Zitto alisema chama chake kimeshatoa tamko na kama kuna chama kinahitaji kufanya hivyo, basi kiombe siku zao nyingine na wafanye mazungumzo yao.

  "Hapa CCM inadandia hoja yetu. Kama kuna vyama, ambavyo vinataka kukutana na rais, basi wapange siku yao waweze kukutana nao waweze kuzungumza yao na si kudandia katika chama chetu," alisema Zitto.

  Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, alisema katika mkutano huo mada kuu ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya vyama vyao kutumia kampeni za kisayansi ili kushinda chaguzi mbalimbali.

  Alisema mambo mengine wanayojadili, ni pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali za Afrika zinatumika kwa kuwanufaisha Waafrika wenyewe na jinsi ya kupiga vita rushwa na uzembe.

  CHANZO:
  NIPASHE JUMAPILI
   
 2. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Awataje kabisa hao mawaziri magarasha.
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,550
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Angewataja basi,ama nianze?
  Membe,Magufuli,Nchimbi,Mwakyembe,Mwandosya...Wengine wamalizie,nadhani pia alimaanisha kuna wanaowasapoti wengine.

  BTW Lowassa mbona si waziri?

  Ama na yeye anaangukia wapi?
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Yule wa Tanroad, Yule mama wa ardhi, yule wa ulinzi na mabomu, yule wa michezo,yule wa maji na umwagiliaji, yule mkubwa wa mawaziri,yule wa afrika mashariki.....yule wa.....!!!List ndefu
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Yule mama wa UN kila leo Ikulu naye sijui anaangukia wapi...?
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hawa wanaumwa na wako nje ya nchi. Tuwaombee kwa Mungu wapone haraka warejee kulijenga taifa letu
   
 7. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  do...... acha wauwane wenyewe
   
 8. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kweli Tanzania ni kichwa cha chizi sasa, hadi Nchimbi?

  Hamko serious jamani, hawezi kuwa na yeye anataka, hilo nakataa
   
 9. k

  kaeso JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huenda labda ana kundi analoliunga mkono.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,550
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Mkuu kumbuka Zitto analalamika kazi hazifanyiki.

  Sasa kama wanaumwa,then kazi zinafanyika saa ngapi?

  Ama umefikiriaje wewe mkuu?

  Neways tuwaombee wapone mapema warudi.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,550
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilishasikia Nchimbi na yeye anataka urais,ngoja Nyambala aje atakujulisha vyema.
   
 12. r

  raffiki Senior Member

  #12
  Nov 27, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili swali linaashiria mengi, Zito was a very good young politician and firm on National issues. Sahivi kaka unapoteza mwelekeo rafiki zako tunaweza kuwa tunakushauri ili upoteze mwelekeo na sie tu shine..watch out. Kitaa sahivi wameshaanza kupoteza mvuto na wewe kwa kushangaa hoja zako zinavyoishia hewani..mfano la mkulo umelianzishaa ukaumwa then ukapona bunge lilipo isha, umekaa kimya sasa umeanzisha move nyingine ya mawaziri kutofanya kazi na kuutaka urais na haujawataja...hauoni kama unajipoteza bro...!Elewa wanachi wanafuatilia nyendo zako maana hata urafiki na vijana wa CCM kitaaunatiliwa shaka... At the start of ur political carrier the ideology u had was so social related,now una urafiki na young politician ambao history yao na ambitions zao sio kwa maslahi kwa jamii..I advice u Mr.,tafuta move moja ya kuhusu maslahi ya wananchi ndio utokee nayo na ukomae hadi mwisho..hii ya kuibua mijadala kila siku bila kuwa na outcomes inakupotezea mvuto.
   
 13. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #13
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umemsahau mzee "6"
  Anausaka kwa udi na uvumba.
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jamani!
  Sasa hawa wanaung'ang'ania uraic wa nini?
  Hawa0n unavomtesa mr MsoGA?
   
 15. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Hawezi kuwataja,watampeleka mahakamani,ila wanajijua so message sent
   
 16. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280


  Mbona sielewi, kuwatimua uanachama au uwaziri?![/QUOTE]

  Alisema kinachotakiwa kwa sasa kama Rais Kikwete amebakiwa na nafasi saba za viti maalum, basi awatimue mawaziri wanaotaka urais kwa sasa na awateue wengine, ambao watafanya kazi kwa ufasaha na kuinua nchi kimaendeleo.[/QUOTE]


  Alaa! kumbe kuwatimua uwaziri; sasa suala la CC ya CCM hapo linatoka wapi!!!?[/QUOTE]


  Zitto alisema hivi sasa uchumi wa Tanzania umeporomoka kufikia asilimia 17.[/QUOTE]

  Hapa vilevile sijaelewa...umeporomoka asilimia 17 au umeporomoka kwa asilimia 17?! Kama umeporomoka asilimia 17, kabla ulikuwa asilimia ngapi?![/QUOTE]


  Alisema hali hiyo imesababishwa na mawaziri hao kushindwa kufanya kazi za kujenga uchumi wa nchi, badala yake kujiingiza katika vita hivyo.[/QUOTE]

  Hapa ningemuelewa endapo angesema "hali hiyo imesababisha mawaziri hao kukidhoofisha chama chao."[/QUOTE]

  Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kwa sasa hali ya nchi ni mbaya ukilinganisha na wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, ambao alisema uchumi ulishuka kwa asilimia 4.5.[/QUOTE]

  Kama anasema wakati wa Mkapa uchumi ulishuka kwa asilimia 4.5, basi bila shaka analinganisha na hali ya uchumi ilivyokuwa wakati wa Mwinyi. If so, is Honourable Zitto serious?![/QUOTE]

  Hata hivyo, alisema anamshukuru Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, kwa kukiri kuchafuka kwa hali ya hewa ndani ya chama hicho kwamba, kunatokana na mbio za urais wa mwaka 2015.[/QUOTE]

  Hapa ndo ananichanganya zaidi! Nini hasa concern ya Mheshimiwa Zitto!! CCM au serikali?! identifying a problem is a one step forward in solving the problem. kwahiyo anafurahi kwamba at last CCM kunaweza kukatulia?![/QUOTE]


  Alisema Mukama alisema kuchafuka kwa hali hiyo ndani ya kumesababisha kuwako kwa makundi makubwa mawili yanayopingana.

  Zitto alisema kutokana na kauli hiyo, CCM imepoteza nguvu, huku mawaziri wake hao kila mmoja macho yake yapo katika urais kiasi cha kuingia katika ugomvi na kuacha kufanya kazi za kuimarisha uchumi wa nchi unaoyumba kwa kiasi cha kutisha.

  Alisema kama mawaziri wameingia katika ugomvi wa kutaka nafasi ya urais, ni dhahiri kwamba, hakuna waziri atakayesimamia maendeleo ya nchi hasa kwenye madini, umeme na kudhibiti tatizo la kushuka kwa shilingi.

  Zitto alisema hali hiyo ni hatari hasa kwa taifa linaloendelea.

  Kuhusu kauli ya CCM kutaka vyama vingine viungane na Chadema katika kumuona rais, Zitto alisema chama chake kimeshatoa tamko na kama kuna chama kinahitaji kufanya hivyo, basi kiombe siku zao nyingine na wafanye mazungumzo yao.

  "Hapa CCM inadandia hoja yetu. Kama kuna vyama, ambavyo vinataka kukutana na rais, basi wapange siku yao waweze kukutana nao waweze kuzungumza yao na si kudandia katika chama chetu," alisema Zitto.

  Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, alisema katika mkutano huo mada kuu ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya vyama vyao kutumia kampeni za kisayansi ili kushinda chaguzi mbalimbali.

  Alisema mambo mengine wanayojadili, ni pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali za Afrika zinatumika kwa kuwanufaisha Waafrika wenyewe na jinsi ya kupiga vita rushwa na uzembe.

  CHANZO:
  NIPASHE JUMAPILI[/QUOTE]

  Nimeamini kwamba kijana mwisho miaka 35, huyu jamaa keshagonga 36 na ameshaanza kufikiria kinyumenyume!

   
 17. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #17
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wako speed kuelekea ikuru kwa kujua kuwa ikuru ye2 cku hizi si mahali patakatifu tena ila pameshakuwa pango la la walanguzi.Acheni wakachukue chao mapema.
   
 18. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Karunguyeye mbona anafikiria urais siku nyingi tu. Lakini kama alivyosema mchangiaji mmoja hili ni tusi kwa watanzania. Ni bora hata kutawaliwa na mbwa kuliko huyu jamaa
   
 19. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  "uchumi umeporomoka hadi kufikia asilimia 17" wtf is that?

  Wahariri wa magazeti yetu vichwa vya panzi, which makes the whole readership population vichwa vya panzi. Kazi tunayo.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,550
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye rangi ya gamba cjakupata kabaisa!

  Otherwise nakubali kuwa a number means nothing if you dont compare it to something(another figure)

  Ama pia ni kwamba hawaeleweki.

  Kwa wenzetu,waandishi wa habari wenye kuripoti issues za uchumi huwa mbali na taaluma ya uandishi, pia mara pengi wanakuwa wataalam wa uchumi ama ni vichwa vilivyosomea uchumi na vyenye utaalamu huo.

  Sasa kwetu hiyo haipo.
   
Loading...