..Mawaziri saba watoswa.....

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
22,750
19,985
...

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuwatosa mawaziri saba wanaotajwa kuwa ni mizigo kwa serikali inayoongozwa na chama hicho.

Hatua hiyo ya kuwatosa mawaziri hao waliohojiwa na Kamati Kuu (CC), iliyokutana juzi mkoani Dodoma, inalenga kukinusuru chama katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka 2015.
Mawaziri waliowekwa kwenye kikaango cha kung’olewa ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza; Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa; Waziri wa Utumishi, Celina Kombani na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia.



Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda; Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.



Tanzania Daima Jumapili, imedokezwa kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wamekuwa wakitaka mawaziri wanaofanya vibaya kwenye wizara zao wawajibishwe kila mara ili kuiepusha serikali kuchukiwa na wananchi.

Inadaiwa wanataka utaratibu uliokuwa ukifanywa miaka ya nyuma na chama chini ya utawala wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere wa kuwaita mawaziri na kuwahoji kwenye vikao vya chama urejewe.



Hoja kubwa wanayoijenga ni kuwa chama ndicho kinachopata wakati mgumu katika chaguzi kwa sababu ya watendaji au mawaziri kutowajibika ipasavyo.


Inaelezwa kwa muda mrefu kumekuwa na mipango ya kuwaondoa mawaziri hao, lakini mazingira ya kuwaondoa ndiyo yamekuwa yakikosekana. Lakini hivi sasa mkakati umeshaiva.
Inadaiwa ziara za kuimarisha chama zilizofanywa na viongozi wa CCM katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Njombe na Mtwara ndizo zimetumika kuandaa mashtaka ya mawaziri hao ambayo waliyajibu walipoitwa kujitetea.
Tanzania Daima Jumapili limedokezwa kuwa licha ya utetezi huo, Kamati Kuu imemtaka Rais Jakaya Kikwete apime hoja zilizotolewa na wajumbe wa CC kama mawaziri hao wanafaa kuendelea na nyadhifa zao.



Uamuzi wa CC



Kikao cha CC kilichoketi juzi, kimemtupia mzigo wa kuwang’oa mawaziri Rais Kikwete ambaye ndiye aliyewateua.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CC imetoa mapendekezo kwa Rais Kikwete ambaye ndiye mwenye hatima ya mawaziri hao.



Alisema Rais Kikwete ni mamlaka ya uteuzi wa mawaziri na ndiye atakayeamua kuwaadabisha, kuwasukuma au kuwaondoa madarakani mawaziri mizigo.



“Aliyewaweka ndiye atakayewaondoa, Kamati Kuu haijamwabia awaondoe, inachokifanya ni kushauri tu. Lakini madaraka yote anayo rais aliyewachagua.


“Kwa mfano Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika hajafika kwa muda wa miaka minne na nusu mkoani Ruvuma ambako ndiko kuna ghala la chakula…, tulipofika Tunduma tulikuta foleni pale mizani eti watumishi wanafanya kazi kwa saa 9, lakini sasa wamebadilisha utaratibu huo wanafanya kwa saa 24 baada ya sisi kwenda,” alisema.


Nape akiwa katika ziara ya siku 26 mikoa mbalimbali, aliwataja mawaziri hao ambao wamekuwa mizigo katika serikali ya Rais Kikwete na kumtaka awatimue.



Hata hivyo Waziri Chiza na Kawambwa walisema kuwa hawafanyi kazi kupitia majukwaa ya siasa na wanasubiri kuitwa na Kamati Kuu, ili waieleze wanavyofanya kazi.


Waziri Kawambwa, alijinasibu kwa kujifafanisha na mti wenye matunda ambao hauishi kupigwa mawe kila kukicha.
Waziri Chiza alimtaka Nape aache kukimbilia kuzungumza hadharani juu ya madai ya wakulima wa korosho na badala yake atafute sababu ya wakulima hao kutolipwa na serikali.
Mabadiliko ya mawaziri
Kama Rais Kikwete ataamua kulifanyia mabadiliko Baraza la Mawaziri itakuwa ni mara ya tatu, ambapo mwaka 2008, alilivunja kutokana na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kujiuzulu kuguswa na kashfa ya kuipa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond.

Mabadiliko mengine aliyafanya Mei mwaka jana baada ya wabunge na wadau mbalimbali kushinikiza kuondolewa kwa mawaziri waliodaiwa kutowajibika ipasavyo.



Maagizo mengine ya CC



Kamati Kuu pia imeiagiza serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa pamba nchini.
“Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu,” alisema Nape.



Aliongeza kuwa CC imeitaka serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nchini.



Nape aliongeza kuwa kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa pamba, serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wake ikiwemo kutowalazimisha.


Kuhusu wakulima wa korosho, alisema kuwa kamati hiyo imeisisitiza serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho na kuhakikisha inabanguliwa nchini.


“Serikali inatakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato kwa wakulima, hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima na kuongeza kipato cha mkulima.


“Kuhusu pembejeo za ruzuku Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa,” alisema.


Kwa upande wa wakulima wa mahindi, Nape alisema kuwa serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.


“Utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua mahindi wa serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa,” alisema.


Nape alisema kwa upande wa madai ya walimu, CC imeiagiza serikali kukamilisha uhakiki wa madai hayo na kuwalipa haki zao ikiwemo kuhakikisha madeni hayazaliwi tena.


Kamati hiyo pia imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye halmashauri mbalimbali nchini.



“Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye halmashauri mbalimbali nchini,” alisema Nape.

Source: Tanzania Daima

Note: CCM wameshaona hali ni mbaya AHADI Hazitekeleziki cc maisha bora ...kigoma kuwa Dubai
 
..

...Mods nisaidieni kurekebisha hapo juu !!

....hakuna kulala mpaka kieleweke!!!

maksibuku ng'wabhejasana.......
 
unaona sasa maudhi ya commies people(wcomunist). CC imewahoji na kupendekeza ila haijsema wafukuzwe bali raisi ndiye aliyeshauliwa kuwafukuza!!!!!!!!! sasa kwa nini basi CC iwahoji kama haina uwezo wa kuwapendekeza wafukwe? katika hao mawaziri wazembe wa kupindukia saba, wapo madokta wanne! sasa kama hata hao madokta uwezo wao wa kufikiri umekuwa mdogo, je hao wengine ilikuwa je?

Jamni watanzania, tuanze kuwasaka hao watu ma-docta waliupata kwa kuokota.
 
Kuna hatari ya kuingiza "mawaziri wapya wabovu zaidi ya waliokuwepo!"who shall suit,for the post among ccm MPs?mapito yatakuwa mlemle,na walewale,president JK mtihani mgumu huu,my "opinion"wenye rekodi za utendaji bora tutawapata kule alipotokea PROF.SOSPETER MULONGO
 
Raisi mwenyewe ndio mzigo namba 1.Hivi yeye huwa haoni uzembe wa mawaziri wake mpaka bunge au kamati kuu ya chama imshinikize?!

Hivi hata utekelezaji wa maazimio ya bunge tatizo ni mawaziri peke yao bila JK kuhusika?

Haya ndio madhara ya Raisi kutwa kupiga misele badala ya kuangalia nchi inakwendaje

Raisi ukingojea kuletewa taarifa tu, ujue kazi itakushinda.
 
kuna hatari ya kuingiza "mawaziri wapya wabovu zaidi ya waliokuwepo!"who shall suit,for the post among ccm MPs?mapito yatakuwa mlemle,na walewale,president JK mtihani mgumu huu,my "opinion"wenye rekodi za utendaji bora tutawapata kule alipotokea PROF.SOSPETER MULONGO

...

jomba tangia aanze kupiga sub zote zimeoza juu mpaka chini maparachichi tu!!!

.....
olo lyobhoya elentwe pyee .....
 
CCM nao wanataka kuhadaa wananchi kwamba na wao wanaweza kuchukua maamuzi magumu baada ya kupata challenge ya CHADEMA! Hebu kama kweli magamba maamuzi magumu mnayaweza shughulikieni ile list ya mafisadi papa mliyokabidhiwa na Dr Slaa tuone! Tofauti na hapo, hilo ni changa la macho na siasa na mazingaombwe ya mchana kweupe!
 
Raisi mwenyewe ndio mzigo namba 1.Hivi yeye huwa haoni uzembe wa mawaziri wake mpaka bunge au kamati kuu ya chama imshinikize?!

Hivi hata utekelezaji wa maazimio ya bunge tatizo ni mawaziri peke yao bila JK kuhusika?

Haya ndio madhara ya Raisi kutwa kupiga misele badala ya kuangalia nchi inakwendaje

Raisi ukingojea kuletewa taarifa tu, ujue kazi itakushinda.

..
....Mkuu Kigoma = Dubai....aiseehh!!!
 
CCM nao wanataka kuhadaa wananchi kwamba na wao wanaweza kuchukua maamuzi magumu! Hebu kama kweli magamba maamuzi magumu mnayaweza shughulikieni ile list ya mafisadi mliyokabidhiwa na Dr Slaa tuone. Tofauti na hapo, hilo ni changa la macho na mazingaombwe ya mchana kweupe!!


...Mkuu jamaa wana phd ya mazingaombwe...
 
Hiyo ndiyo kazi iliyotakiwa ifanywe na chama tawala siku zote kama njia ya kujibu mapigo ya upinzani....cyo kudanganya wananchi majukwaani na kutumia media za umma kama tbc Taifa kujinadi mambo yasiyo na tija wala yasiyoleta mabadiliko ya ukali wa maisha ya wananchi huku wenye kupewa dhamana wakiishi kama peponi: CCM kina mchango mkubwa sana ktk kuboronga kwa serikali. Kitendo cha wao kujibu mapigo ya vyama pinzani bila kutizama realities, kiliwafanya watendaji wabweteke kwa muda mrefu. kwa sasa nawapongeza kama itakuwa na dhamira ya kumkomboa maskini na c kushinda uchaguzi mkuu 2015

Napata wasiwasi sijaskia swala meno ya tembo na waziri anayehusika mh kagasheki au kuna maslahi ya wakubwa??
Vipi kuhusu kashfa za dawa za kulevya na waziri wa ulinzi nchimbi, au ni deal za vigogo?
Vipi mgao wa umeme, na waziri husika, au kwenu haupo?
 
Hiyo ndiyo kazi iliyotakiwa ifanywe na chama tawala siku zote kama njia ya kujibu mapigo ya upinzani....cyo kudanganya wananchi majukwaani

Hata hii Mkuu wanatudanganya tu!

JK hawezi mtosa Dr Kawamba na Adam Malima!

Nape anajifurahisha tu
 
Hiyo ndiyo kazi iliyotakiwa ifanywe na chama tawala siku zote kama njia ya kujibu mapigo ya upinzani....cyo kudanganya wananchi majukwaani na kutumia media za umma kama tbc Taifa kujinadi mambo yasiyo na tija wala yasiyoleta mabadiliko ya ukali wa maisha ya wananchi huku wenye kupewa dhamana wakiishi kama peponi: CCM kina mchango mkubwa sana ktk kuboronga kwa serikali. Kitendo cha wao kujibu mapigo ya vyama pinzani bila kutizama realities, kiliwafanya watendaji wabweteke kwa muda mrefu. kwa sasa nawapongeza kama itakuwa na dhamira ya kumkomboa maskini na c kushinda uchaguzi mkuu 2015

Napata wasiwasi sijaskia swala meno ya tembo na waziri anayehusika mh kagasheki au kuna maslahi ya wakubwa??
Vipi kuhusu kashfa za dawa za kulevya na waziri wa ulinzi nchimbi, au ni deal za vigogo?
Vipi mgao wa umeme, na waziri husika, au kwenu haupo?


.....Dadadek ningepigwa chini aliyekula meno ya tembo angeyatapika live!!!
 
Baada ya hapo nimesikia vibaka wa buku 7 Lumumba wanajiandaa kuja na threads nyingi kwamba CCM ni mfano wa kuigwa kwa kufanya maamzi magumu. Hebu watazame jinsi wanavyojipanga kuleta umbeya!!
attachment.php
 
Hata hii Mkuu wanatudanganya tu!

JK hawezi mtosa Dr Kawamba na Adam Malima!

Nape anajifurahisha tu

Sitaki kuamini kuwa JK ataenda against chama ambacho yeye ni mwenyekiti wake: In fact CCM wakifeli ktk mpango huu walionzisha, wakuwapiga chini mawaziri mizigo, watazidi kupoteza imani kwa watanzania. Huyu kawambwa cjui ana ushawishi gani kwa Mr. President au ni swahiba tuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom