Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waapishwa Ikulu, Dodoma

Bahati tu,hata Samia alipata ngekewa tu,ila akuwa na uwezo wa kuongoza,ni jinsia tu iliyombeba sio uwezo
😄😄👇👇

IMG-20210913-WA0012.jpg
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mawaziri wateule wanne na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

Mawaziri ni Dkt. Stergomena Tax Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, January Makamba Waziri wa Nishati, Prof. Makame Mbarawa Waziri wa Ujenzi na Dkt. Ashatu Kijaji Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Pia, Dkt. Eliezer Feleshi amekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

====

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametaka kuwepo Mikataba bora ya Nishati hususan ya Umeme. Amesema hayo wakati wa Uapisho wa Viongozi walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan

Amesema, "Tuna matatizo makubwa kwenye Nishati ya Petroli, Dizeli na jamii zake zote. Bei ya Petroli isipande kama inavyokwenda, tuangalie mbinu mbadala"

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema iliyokuwa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo sasa itakuwa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo

Amesema amehamisha Idara ya Habari ili Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iweze kutimia kwani kimekuwa ni kilio cha Wadau wa Sekta ya Habari kwa muda mrefu

Amefafanua, "Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ilikuwa inamezwa na Habari. Nimeona niiachie ionekane kwa uwazi zaidi kwasababu Sanaa ni Ajira kwa Vijana wengi'

Amewataka Wakuu wa Mikoa kuwapanga Wamachinga ambao sasa wameonekana kuenea kila sehemu hadi mbele ya maduka na kufanya wenye maduka baadhi kutoa bidhaa na kumpa Machinga auze

Amesema kitendo hicho kinaikosesha Serikali kodi, kwani Mmachinga halipi kodi lakini mwenye duka anatakiwa kulipa kodi. Amewataka Wamachinga kufuata Sheria zilizopo

Amesema wakati wa kuwapanga hataki kuona ngumi, kupigana, kumwaga bidhaa, kuchafuliana bali hatua zichukuliwe vema bila mwenye maduka na Wamachinga kuudhika

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi ya Waziri kwenye Wizara ya Ulinzi sio kubeba mzinga wala kupiga bunduki, bali ni kusimamia Sera na Utawala wa Wizara

Amesema, "Nimeamua kuvunja 'myth au taboo' ya muda mrefu kwamba Wizara ya Ulinzi lazima akae Mwanaume mwenye misuli yake. Nimempeleka Dkt. Stergomena Tax huko kwasababu ya upeo aliopata akiwa SADC"

Ameongeza, "Yeye anajua vema Askari wetu waliopo Msumbiji na DR Congo, kwanini wapo huko na mifumo yao. Atamsaidia vizuri CDF katika upande huo"

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendeshwa kwa matendo makali na sio maneno makali akifafanua, "Matendo makali ni kwenda kwa Wananchi na kutoa huduma inayotakiwa"

Ameeleza, "Msinitegemee nikae hapa nianze kufoka ovyo. Kwasababu nafanya kazi na watu wazima, ni imani yangu tunapozungumza tunaelewana"

Amesema, mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na Viongozi wengine Wizarani bado yataendelea


Huyu Mzanzibari kwenye wizara ya ujenzi isiyohusu muungano anatafuta nini. Hakuna watanganyika wenye uwezo wa kuiongoza mpaka apewe tx? Mjengo wake wa ghorofa saba karibu na stendi mpya ya mabasi ya mwenge naona unaenda kwa kasi ya ajabu huku ujenzi wa stendi ukiwa umesimama
 
Kwahiyo Kalemani alirelax..... So Makamba is better...!??

Hiki ni kituko..
Kituko cha Karne, huyo dogo Februrary alishaonekana ni mamluki wayback. Nimepitia mahala nikaona pia kumbe alikuwa ni kilaza tu maeneo ya skonga ila mbeleko fc zilihusika kumfikisha alipo na mpaka sasa zinaendelea.
 
Makamba, hakikisha kukatikakatika umeme itakuwa historia, mimi mlala hoi ninapata shida na kasaluni kangu ka kunyoa. Ni hako kanapeleka chakula mezani, kukatika umeme ni kamba shingoni.
We unategemea kunakwenda kuwa na unafuu wowote? Huyo dogo alikuwa anatafutiwa chance siku nyingi tu hapo ni mwendo wa kupiga tu na naskia anautakaga uraisi so anaweza akalamba dume 2025
 
Back
Top Bottom