Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waapishwa Ikulu, Dodoma

Ina maana kati ya wabunge 300+ wa CCM hakuna mwenye afadhali hadi Hangaya anakopa watu nje ya bunge?
Hilo ni tusi kwa wanananchi, si kwa wabunge. Kazi ya waziri si mbeba bunduki wala mzinga, lakini akumbuke kuna kazi unaweza mpa mjinga yeyote na akaifanya, hata kama si kwa kiwango, lakini si kila kazi inaweza fanywa na yeyote, taaluma ina nafasi yake.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hiyo wizara ya Habari ya Habari na teknolojia aweke mtu mbobezi kwenye teknolojia ya mawasiliano asituletee madaktari wapima mikojo na vinyesi hospital kama Ndugulile

Tumepiga kelele kuwa PayPal Tanzania iruhusiwe kama njia ya kupokea malipo ya biashara za mitandaoni waziri alikuwa haelewi hata PayPal ni kitu gani
Atakwambia waziri wa tecnologia kazi yake sio kujua na kusimika minara na vikorombwezo vyake.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Siyo Pay Pal tu, Sasa hivi nchi nyingi zinaweka Televisheni na Redio zake kwenye satellite (tv mux) moja ambayo mawimbi yake yanafikika na kupatikana kwa urahisi ndani ya nchi husika na hivyo kuondoa kero ya upatikanaji wa habari lakini gharama za kupata taarifa na habari. Sie bado tunategemea hizi tv za kulipia ambao kila siku wanapandisha gharama za vifurushi vyao.
Na kifurushi ukilipia na siku ya tatu ukasafiri mwezi, ukirudi imekula kwako!

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Tunampongeza Mh Rais kwa hatua nyingi mbalimbali. Mh. Lissu na Mh Mbowe ni wapinzani, tena sio wakitoto na tunawahitaji sana kwa kazi hiyo. Tuache kuwabambikia kesi za ugaidi nk zinazochafua sura ya nchi kwa dunia na ndani ya nchi. Lakini wajibiwe kwa utendaji wenye tija, unaokidhi matakwa ya watawaliwa na hoja zenye mashiko. Watanzania sio wajinga kama alivyosema mwendazake mwenyewe na cheo ni dhamana ya muda mfupi. Mkiwanyima wapinzani makini kuongea, watazaliwa kina Hamza. Usifikiri hawa wafadhili (EU, USA, UK, Germany etc) wanaokuja mahakamani kusikiliza kesi ya Mbowe hawana kazi, au wamekuja kutembea: There will be serious consequences in the event that justice will not be seen observed and mark my words. Tusidanganyane kwamba ati sisi ni nchi huru kwa hiyo tuna uhuru hata wa kuoneana. Nonsensical. Kwa hiyo Mh Sangaya tunakuomba uisalimishe nchi yetu.
Kama atafanikiwa kuyaona ulio andika naye akayafikisha kwa mhusika.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Makamba, hakikisha kukatikakatika umeme itakuwa historia, mimi mlala hoi ninapata shida na kasaluni kangu ka kunyoa. Ni hako kanapeleka chakula mezani, kukatika umeme ni kamba shingoni.
 
Sasa wamachinga wanaondoka au hawaondoki?
Yule anasema waondoke, huyu anasema wapangwe vizuri, kweli machinga wameidhibiti serikali vizuri sana yaani haifurukuti,
Kisa kura? Au kula?
 
Prof. Mbarawa tunakuomba acha upole, kuwa mkali.
tunakufahamu wewe ni mfuatiliaji mzuri sana ila tatizo una kaupole, wapigaji na wabadhirifu huwa wanapenda sana kusimamiwa na mtu mpole ili wapate namna ya kupiga vizuri.
hivyo tunakuomba ongeza ukali ili miradi isonge kwa kasi.
 
huu wimbo wa Chadema kufa mliuimba sana na Mzee Pombe matokeao yake akafa mzee Pombe kwa korona alafu chama bado kipo.
Chadema kwa kujifariji mko sawa,chama kutoka wabunge zaidi ya Mia,leo kina mbunge mmoja tu,na migogoro kibao bado mnasema kuna chama hapo! ngoja Mfarume Mbowe anyeshewe mvua ya miaka kama kumi hivi,akina Mdee wachukue chama mdio mtajua, chadema iliisha kufa to Slaa alivyoachia ngazi, huo ndio ulikuwa mwisho wa chadema.
 
Back
Top Bottom