Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waapishwa Ikulu, Dodoma

Rais wetu Mpendwa Mama Samia leo kanena kinagaubaga kuwa kulingana na malezi aliyo yapata hana tabia ya kufokea watu wazima ambao wanafahamu au wanatambua majukumu yao, hapa aliwalenga watendaji wote wa Serikali, kuwa hana muda wa kuwafokea hadharani kiongozi yeyote yule aliye haribu au ambaye hayuko tayari kufanya kazi bali atafoka kwa kalamu yake.

Sasa wapo baadhi ya viongozi walio teuliwa wameamua ku… relax kwa kudhani Mhe. Rais ni Mpole au dhaifu...la hasha! yupo macho na macho yake yanaona kila kona/pembe ya nchi hii, kila wizara, kila ofisi, kila mtumishi wa serikali.

Hiyo ni Salamu tosha kwa wakaidi na ambao wanafanya kazi kimazoea au kwa maksudi wameamua kuzuga wakidhani Rais ni dhaifu.

Nchi hii ina hazina ya kutosha ya wasomi na weledi hivyo wale wote walio teuliwa wasidhani kuwa wao ni wazuri zaidi kuliko wengine bali uzuri wao utatokana na utendaji wao.

Hongera kwa Mhe. Rais wetu kwa kuwa na msimamo.

Tahadhari wa watendaji wote wa Serikali;
Badilikeni haraka sana, vinginevyo fagio la chuma lazima likupitie bila huruma.
Wale wote mnao zuga mnafahamika.
Kwahiyo Kalemani alirelax..... So Makamba is better...!??

Hiki ni kituko..
 
"Nitafoka kwa kalamu"
Nimependa alivyoongea,amesema nilikuwa na miezi sita ya kuwasoma na amegundua kuna viongozi walichukulia poa wakawa wanaongoza wanavyojua wao,si vizuri sisi wengine kuyajua hayo ila yeye ameyajua ndio sababu kawatoa hao,kwahiyo waliobaki sasa wajuwe kuwa ameshakuwa mzoefu,kalamu ndio itafanya kazi...
 
umenifurahisha kumtumbua huyo kima a.k.a Ndugulile ila umekosea kumuacha kima mwingine anaitwa Nchemba kudadeki huyo jamaa nina hasira naye sana

5A0106A6-502D-4317-ACD8-C2B4AE69E1B0.jpeg
 
Hiyo wizara ya Habari ya Habari na teknolojia aweke mtu mbobezi kwenye teknolojia ya mawasiliano asituletee madaktari wapima mikojo na vinyesi hospital kama Ndugulile

Tumepiga kelele kuwa PayPal Tanzania iruhusiwe kama njia ya kupokea malipo ya biashara za mitandaoni waziri alikuwa haelewi hata PayPal ni kitu gani
 
Hotuba nzur ameongea point analeta matumain sasa watu walikuwa wanaelekea kumchukulia powa
 
Hiyo wizara ya Habari ya Habari na teknolojia aweke mtu mbobezi kwenye teknolojia ya mawasiliano asituletee madaktari wapima mikojo na vinyesi hospital kama Ndugulile

Tumepiga kelele kuwa PayPal Tanzania iruhusiwe kama njia ya kupokea malipo ya biashara za mitandaoni waziri alikuwa haelewi hata PayPal ni kitu gani
Siyo Pay Pal tu, Sasa hivi nchi nyingi zinaweka Televisheni na Redio zake kwenye satellite (tv mux) moja ambayo mawimbi yake yanafikika na kupatikana kwa urahisi ndani ya nchi husika na hivyo kuondoa kero ya upatikanaji wa habari lakini gharama za kupata taarifa na habari. Sie bado tunategemea hizi tv za kulipia ambao kila siku wanapandisha gharama za vifurushi vyao.
 
Kwa hali hii Lisu na Chadema hawana chao tena.
Tunampongeza Mh Rais kwa hatua nyingi mbalimbali. Mh. Lissu na Mh Mbowe ni wapinzani, tena sio wakitoto na tunawahitaji sana kwa kazi hiyo. Tuache kuwabambikia kesi za ugaidi nk zinazochafua sura ya nchi kwa dunia na ndani ya nchi. Lakini wajibiwe kwa utendaji wenye tija, unaokidhi matakwa ya watawaliwa na hoja zenye mashiko. Watanzania sio wajinga kama alivyosema mwendazake mwenyewe na cheo ni dhamana ya muda mfupi. Mkiwanyima wapinzani makini kuongea, watazaliwa kina Hamza. Usifikiri hawa wafadhili (EU, USA, UK, Germany etc) wanaokuja mahakamani kusikiliza kesi ya Mbowe hawana kazi, au wamekuja kutembea: There will be serious consequences in the event that justice will not be seen observed and mark my words. Tusidanganyane kwamba ati sisi ni nchi huru kwa hiyo tuna uhuru hata wa kuoneana. Nonsensical. Kwa hiyo Mh Sangaya tunakuomba uisalimishe nchi yetu.
 
Kwahiyo Kalemani alirelax..... So Makamba is better...!??

Hiki ni kituko..
cheo ni dhamana, cheo sio mali ya Kalemani wala Makamba wale yeyote yule.
Mtanzania yeyote mwenye sifa hata wewe unaweza kuwa waziri ktk wizara yoyote ile.
Jambo la msingi ni kuwatumikia watanzania kwa moyo na bidii na kwa uzalendo
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mawaziri wateule wanne na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

Mawaziri ni Dkt. Stergomena Tax Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, January Makamba Waziri wa Nishati, Prof. Makame Mbarawa Waziri wa Ujenzi na Dkt. Ashatu Kijaji Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Pia, Dkt. Eliezer Feleshi amekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

====

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametaka kuwepo Mikataba bora ya Nishati hususan ya Umeme. Amesema hayo wakati wa Uapisho wa Viongozi walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan

Amesema, "Tuna matatizo makubwa kwenye Nishati ya Petroli, Dizeli na jamii zake zote. Bei ya Petroli isipande kama inavyokwenda, tuangalie mbinu mbadala"

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema iliyokuwa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo sasa itakuwa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo

Amesema amehamisha Idara ya Habari ili Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iweze kutimia kwani kimekuwa ni kilio cha Wadau wa Sekta ya Habari kwa muda mrefu

Amefafanua, "Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ilikuwa inamezwa na Habari. Nimeona niiachie ionekane kwa uwazi zaidi kwasababu Sanaa ni Ajira kwa Vijana wengi'

Amewataka Wakuu wa Mikoa kuwapanga Wamachinga ambao sasa wameonekana kuenea kila sehemu hadi mbele ya maduka na kufanya wenye maduka baadhi kutoa bidhaa na kumpa Machinga auze

Amesema kitendo hicho kinaikosesha Serikali kodi, kwani Mmachinga halipi kodi lakini mwenye duka anatakiwa kulipa kodi. Amewataka Wamachinga kufuata Sheria zilizopo

Amesema wakati wa kuwapanga hataki kuona ngumi, kupigana, kumwaga bidhaa, kuchafuliana bali hatua zichukuliwe vema bila mwenye maduka na Wamachinga kuudhika

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi ya Waziri kwenye Wizara ya Ulinzi sio kubeba mzinga wala kupiga bunduki, bali ni kusimamia Sera na Utawala wa Wizara

Amesema, "Nimeamua kuvunja 'myth au taboo' ya muda mrefu kwamba Wizara ya Ulinzi lazima akae Mwanaume mwenye misuli yake. Nimempeleka Dkt. Stergomena Tax huko kwasababu ya upeo aliopata akiwa SADC"

Ameongeza, "Yeye anajua vema Askari wetu waliopo Msumbiji na DR Congo, kwanini wapo huko na mifumo yao. Atamsaidia vizuri CDF katika upande huo"

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendeshwa kwa matendo makali na sio maneno makali akifafanua, "Matendo makali ni kwenda kwa Wananchi na kutoa huduma inayotakiwa"

Ameeleza, "Msinitegemee nikae hapa nianze kufoka ovyo. Kwasababu nafanya kazi na watu wazima, ni imani yangu tunapozungumza tunaelewana"

Amesema, mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na Viongozi wengine Wizarani bado yataendelea


Wakachape kazi
 
Katika mambo huwa siafiki Ni hizi teua teua ambapo Raisi anateua kwa kugawa ugali na sio uwezo wa mtu!
Matokeo yake ndio hayo, Leo anateua zen miezi kadhaa mbele anatengua! Hili Jambo halijawah kuwa sawa, haliko sawa na halitakuwa sawa, otherwise, means nyngne ifanyike Kama hawaitaki katiba mpya!
Hama Nchi
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom