data
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 26,149
- 22,723
Kwahiyo Kalemani alirelax..... So Makamba is better...!??Rais wetu Mpendwa Mama Samia leo kanena kinagaubaga kuwa kulingana na malezi aliyo yapata hana tabia ya kufokea watu wazima ambao wanafahamu au wanatambua majukumu yao, hapa aliwalenga watendaji wote wa Serikali, kuwa hana muda wa kuwafokea hadharani kiongozi yeyote yule aliye haribu au ambaye hayuko tayari kufanya kazi bali atafoka kwa kalamu yake.
Sasa wapo baadhi ya viongozi walio teuliwa wameamua ku… relax kwa kudhani Mhe. Rais ni Mpole au dhaifu...la hasha! yupo macho na macho yake yanaona kila kona/pembe ya nchi hii, kila wizara, kila ofisi, kila mtumishi wa serikali.
Hiyo ni Salamu tosha kwa wakaidi na ambao wanafanya kazi kimazoea au kwa maksudi wameamua kuzuga wakidhani Rais ni dhaifu.
Nchi hii ina hazina ya kutosha ya wasomi na weledi hivyo wale wote walio teuliwa wasidhani kuwa wao ni wazuri zaidi kuliko wengine bali uzuri wao utatokana na utendaji wao.
Hongera kwa Mhe. Rais wetu kwa kuwa na msimamo.
Tahadhari wa watendaji wote wa Serikali;
Badilikeni haraka sana, vinginevyo fagio la chuma lazima likupitie bila huruma.
Wale wote mnao zuga mnafahamika.
Hiki ni kituko..