Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waapishwa Ikulu, Dodoma

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mawaziri wateule wanne na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

Mawaziri ni Dkt. Stergomena Tax Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, January Makamba Waziri wa Nishati, Prof. Makame Mbarawa Waziri wa Ujenzi na Dkt. Ashatu Kijaji Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Pia, Dkt. Eliezer Feleshi amekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

====

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametaka kuwepo Mikataba bora ya Nishati hususan ya Umeme. Amesema hayo wakati wa Uapisho wa Viongozi walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan

Amesema, "Tuna matatizo makubwa kwenye Nishati ya Petroli, Dizeli na jamii zake zote. Bei ya Petroli isipande kama inavyokwenda, tuangalie mbinu mbadala"

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema iliyokuwa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo sasa itakuwa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo

Amesema amehamisha Idara ya Habari ili Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iweze kutimia kwani kimekuwa ni kilio cha Wadau wa Sekta ya Habari kwa muda mrefu

Amefafanua, "Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ilikuwa inamezwa na Habari. Nimeona niiachie ionekane kwa uwazi zaidi kwasababu Sanaa ni Ajira kwa Vijana wengi'

Amewataka Wakuu wa Mikoa kuwapanga Wamachinga ambao sasa wameonekana kuenea kila sehemu hadi mbele ya maduka na kufanya wenye maduka baadhi kutoa bidhaa na kumpa Machinga auze

Amesema kitendo hicho kinaikosesha Serikali kodi, kwani Mmachinga halipi kodi lakini mwenye duka anatakiwa kulipa kodi. Amewataka Wamachinga kufuata Sheria zilizopo

Amesema wakati wa kuwapanga hataki kuona ngumi, kupigana, kumwaga bidhaa, kuchafuliana bali hatua zichukuliwe vema bila mwenye maduka na Wamachinga kuudhika

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi ya Waziri kwenye Wizara ya Ulinzi sio kubeba mzinga wala kupiga bunduki, bali ni kusimamia Sera na Utawala wa Wizara

Amesema, "Nimeamua kuvunja 'myth au taboo' ya muda mrefu kwamba Wizara ya Ulinzi lazima akae Mwanaume mwenye misuli yake. Nimempeleka Dkt. Stergomena Tax huko kwasababu ya upeo aliopata akiwa SADC"

Ameongeza, "Yeye anajua vema Askari wetu waliopo Msumbiji na DR Congo, kwanini wapo huko na mifumo yao. Atamsaidia vizuri CDF katika upande huo"

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendeshwa kwa matendo makali na sio maneno makali akifafanua, "Matendo makali ni kwenda kwa Wananchi na kutoa huduma inayotakiwa"

Ameeleza, "Msinitegemee nikae hapa nianze kufoka ovyo. Kwasababu nafanya kazi na watu wazima, ni imani yangu tunapozungumza tunaelewana"

Amesema, mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na Viongozi wengine Wizarani bado yataendelea

 
Kwa kipindi cha miezi sita nilikuwa nawasoma viongozi. Sasa nimewajua vizuri sana na kwa hiyo sijaweka kituo kwenye uteuzi bali nimeweka koma.

Nitaendelea kufanya uteuzi kila ninapoona panafaa. Jamani upole na makuzi yangu pengine watu wananichukulia poa. Kuna baadhi ya mawaziri walianza kufanya wapendavyo.

Maneno ya mama hakuna mwenye namba ya kudumu kwenye kikosi chake
 
Rais Samia amesema zoezi la kubadilisha watendaji wa wizara mbalimbali ni endelevu ndio maana leo hajawaapisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Naibu wake ambayo kimsingi ni wizara mpya baada ya kurekebishwa.

Source: ITV

My take; Bavicha kunyweni mtori nyama mtazikuta chini!
 
Kwa kipindi cha miezi sita nilikuwa nawasoma viongozi. Sasa nimewajua vizuri sana na kwa hiyo sijaweka kituo kwenye uteuzi bali nimeweka koma. Nitaendelea kufanya uteuzi kila ninapoona panafaa. Jamani upole na makuzi yangu pengine watu wananichukulia poa. Kuna baadhi ya mawaziri walianza kufanya wapendavyo.
Maneno ya mama hakuna mwenye namba ya kudumu kwenye kikosi chake
That is my president! Samia Hassan Suluhu!
 
Rais wetu Mpendwa Mama Samia leo kanena kinagaubaga kuwa kulingana na malezi aliyo yapata hana tabia ya kufokea watu wazima ambao wanafahamu au wanatambua majukumu yao, hapa aliwalenga watendaji wote wa Serikali, kuwa hana muda wa kuwafokea hadharani kiongozi yeyote yule aliye haribu au ambaye hayuko tayari kufanya kazi bali atafoka kwa kalamu yake.

Sasa wapo baadhi ya viongozi walio teuliwa wameamua ku… relax kwa kudhani Mhe. Rais ni Mpole au dhaifu...la hasha! yupo macho na macho yake yanaona kila kona/pembe ya nchi hii, kila wizara, kila ofisi, kila mtumishi wa serikali.

Hiyo ni Salamu tosha kwa wakaidi na ambao wanafanya kazi kimazoea au kwa maksudi wameamua kuzuga wakidhani Rais ni dhaifu.

Nchi hii ina hazina ya kutosha ya wasomi na weledi hivyo wale wote walio teuliwa wasidhani kuwa wao ni wazuri zaidi kuliko wengine bali uzuri wao utatokana na utendaji wao.

Hongera kwa Mhe. Rais wetu kwa kuwa na msimamo.

Tahadhari wa watendaji wote wa Serikali;
Badilikeni haraka sana, vinginevyo fagio la chuma lazima likupitie bila huruma.
Wale wote mnao zuga mnafahamika.
 
Back
Top Bottom