Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waapishwa Ikulu, Dodoma

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,546
2,000
Rais Samia amesema zoezi la kubadilisha watendaji wa wizara mbalimbali ni endelevu ndio maana leo hajawaapisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Naibu wake ambayo kimsingi ni wizara mpya baada ya kurekebishwa.

Source: ITV

My take; Bavicha kunyweni mtori nyama mtazikuta chini!
Sasa hili Jo linahusiana vipi na BAVICHA? au ulitaka kusema uvccm?
 

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,316
2,000
Katika mambo huwa siafiki Ni hizi teua teua ambapo Raisi anateua kwa kugawa ugali na sio uwezo wa mtu!
Matokeo yake ndio hayo, Leo anateua zen miezi kadhaa mbele anatengua! Hili Jambo halijawah kuwa sawa, haliko sawa na halitakuwa sawa, otherwise, means nyngne ifanyike Kama hawaitaki katiba mpya!
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,055
2,000
Kwa kipindi cha miezi sita nilikuwa nawasoma viongozi. Sasa nimewajua vizuri sana na kwa hiyo sijaweka kituo kwenye uteuzi bali nimeweka koma. Nitaendelea kufanya uteuzi kila ninapoona panafaa. Jamani upole na makuzi yangu pengine watu wananichukulia poa. Kuna baadhi ya mawaziri walianza kufanya wapendavyo.
Maneno ya mama hakuna mwenye namba ya kudumu kwenye kikosi chake
Waendelee tuu kumlinganisha na yule mropokaji wataisoma namba.
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,617
2,000
Rais Samia amesema zoezi la kubadilisha watendaji wa wizara mbalimbali ni endelevu ndio maana leo hajawaapisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Naibu wake ambayo kimsingi ni wizara mpya baada ya kurekebishwa.

Source: ITV

My take; Bavicha kunyweni mtori nyama mtazikuta chini!
Ina maana kati ya wabunge 300+ wa CCM hakuna mwenye afadhali hadi Hangaya anakopa watu nje ya bunge?
 

MASHANJARA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
301
500
Hongera HE Hangaya Samia Suluhu Hassan. Angalau kwa sasa tumeona nia yako ya dhati ya kuwa na baraza la mawaziri more inclusive na lenye sura ya Kitaifa, lakini lenye kuzingatia uwezo, uadilifu, na track record ya utendaji wa wateuliwa. Naamini tuendako wakati demokrasia yetu itakapoanza kunyanyuka tena mambo yatakuwa mazuri hasa uwakilishi wa vyama vingi bungeni. Bunge liwe bunge kweli. Kwa sasa hatuna bunge, tuna mikutano ya wanaccm, ACT Zbar na waunga juhudi za mwendazake. Tija ni ndogo sana kama wewe mwenyewe ulivyotamka. Isingekuwa ni gharama, tungewaza kukuomba ulivunje bunge tuanze upya. Lakini hongera unasonga mbele vizuri. Naamini mbeleni utapata Halmashauri kuu mpya, Kamati kuu mpya na Secretariat mpya ya chama unachokiongoza. Inshallah!
 

Magna Carta

JF-Expert Member
Jul 14, 2014
4,224
2,000
Rais wetu Mpendwa Mama Samia leo kanena kinagaubaga kuwa kulingana na malezi aliyo yapata hana tabia ya kufokea watu wazima ambao wanafahamu au wanatambua majukumu yao, hapa aliwalenga watendaji wote wa Serikali, kuwa hana muda wa kuwafokea hadharani kiongozi yeyote yule aliye haribu au ambaye hayuko tayari kufanya kazi bali atafoka kwa kalamu yake.

Sasa wapo baadhi ya viongozi walio teuliwa wameamua ku… relax kwa kudhani Mhe. Rais ni Mpole au dhaifu...la hasha! yupo macho na macho yake yanaona kila kona/pembe ya nchi hii, kila wizara, kila ofisi, kila mtumishi wa serikali.

Hiyo ni Salamu tosha kwa wakaidi na ambao wanafanya kazi kimazoea au kwa maksudi wameamua kuzuga wakidhani Rais ni dhaifu.

Nchi hii ina hazina ya kutosha ya wasomi na weledi hivyo wale wote walio teuliwa wasidhani kuwa wao ni wazuri zaidi kuliko wengine bali uzuri wao utatokana na utendaji wao.

Hongera kwa Mhe. Rais wetu kwa kuwa na msimamo.

Tahadhari wa watendaji wote wa Serikali;
Badilikeni haraka sana, vinginevyo fagio la chuma lazima likupitie bila huruma.
Wale wote mnao zuga mnafahamika.
ishu ya kufokeana fokeana kama watotohumu maofisini huwa inaniuzi sana huwa natamani kumpiga ngumi mtu anayefoka foka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom