Mawaziri mzigo wahojiwa na CC ya CCM Dodoma - Kikwete aongoza kikao hicho

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
Shukuru Kawambwa(5).jpg download.jpg download (1).jpg images.jpg
Kutoka Kushoto mawaziri, Kawambwa, Kombani, Chiza, Matayo na Ghasia

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) imekutana jana mjini hapa chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, na kuanza kuwahoji mawaziri wanaodaiwa kuwa mzigo kwenye Baraza la Mawaziri.

Kamati hiyo iliyoanza kikao chake majira ya saa 5 asubuhi katika jengo la White House, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ilikuwa na agenda kadhaa, ikiwamo kuu ya kuwajadili mawaziri hao.

Suala la mawaziri hao kuwa mzigo, limekuwa gumzo hasa katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini hapa na kusababisha baadhi ya wabunge kutaka mawaziri hao wachukuliwe hatua.

NIPASHE Jumamosi ilishuhudia baadhi ya mawaziri waliotajwa kuwa mzigo wakiwa katika viwanja vya White House, wakisubiri kuitwa kwa mahojiano.

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. Mathayo David.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

Mawaziri hao waliitwa na Kamati kuu kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kulalamikiwa kuwa utendaji wao ni mbaya.

Mpaka gazeti hili linaenda mitamboni, mawaziri wawili akiwamo Kombani na Kawambwa, walikuwa wameshaitwa na kuhojiwa.

Mapema kabla ya kikao hicho kuanza, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipohojiwa na waandishi kuhusu agenda zitakazojadiliwa kwenye kikao hicho, alisema taarifa kamili zitatolewa leo.

Hata hivyo, NIPASHE Jumamosi ilishuhudia mawaziri hao wawili wakiwa tayari wameshahojiwa wakiwa nje ya ukumbi.

Hivi karibuni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nnauye, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa mawaziri hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania.

Kauli hiyo aliitoa wakati viongozi hao wa chama walipofanya ziara katika mikoa mbalimbali ya kusikiliza kero za wananchi kwa nia ya kukiimarisha chama.

Alionyesha kusikitishwa kwake na kitendo cha mawaziri hao waliopewa dhamana kushindwa kutambua wajibu wao na kueleza kuwa umefika wakati wa wao kuhojiwa na Kamati Kuu ya chama ili wachukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo aibu itarudi kwa chama chake.

Nape alitoa kauli hiyo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakati akielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.

Hisani ya Nipashe
 
Unajua uropokaji wa Nape unaweza ukawa una manufaa safari hii.
Mimi nahisi hawa viongozi wakiwa mjini huwa wanajisahau sana kuhusu wajibu wao na shida za kweli za wa tanzania. Walivoenda huko kijijini na kuona hali halisi ikawa kama a reminder.
Dah at least tumshukuru Mola kuwa hawa maCCM wana chembe ya huruma.
 
Jamani mawaziri mhurumieni rais wetu alianza kwa kuwa amini akina Lowasa na wenzake wakamwangusha,wakaja akina Ngereja,Mkulo,nk. wakamwangusha na nyinyi tena mmemwangusha kama vipi rais teua hata upizani basi....maana hawa hawabebeki.....la kuvunda halina ubani.
 
ni kweli kunaweza kukawa na mabadiliko katika baadhi ya wizara.waziri mkuu atabaki.hatua hiyo haitaleta tija yoyote kwa sababu hali imekuwa mbaya mno hususan katika mamlaka ya serikali za mitaa.
 
nani wa kuwajibishwa aliye chagua mawaziri au mawaziri.ccm mnafikiri negatively..
 
Jamani mawaziri mhurumieni rais wetu alianza kwa kuwa amini akina Lowasa na wenzake wakamwangusha,wakaja akina Ngereja,Mkulo,nk. wakamwangusha na nyinyi tena mmemwangusha kama vipi rais teua hata upizani basi....maana hawa hawabebeki.....la kuvunda halina ubani.
Upinzania ateuliwe nani? Mini kabang
 
Hakuna chochote hapo, wanatubeza na kutucheka tu.

niko pamoja na wewe,maana sidhan kama Kamati kuu ndo ilowapa uwaziri hawa viumbe,hadi iwahoji,,,,bunge na CAG wamejiridhisha kuwa ni mzigo why wasitoswe????mbona hao wengine walopigwa chini hawakuitwa na C.C
na pia C.C ina watu wasafi kwa kiasi gani????
 
Mh. Kikwete anauzoefu wa kuvunja baraza la mawaziri na kuwaondoa mawaziri mizigo, hatua hii ya kuwasikiliza kwanza kwa maana ya kuwapa nafasi ya utetezi ni hatua mhimu sana ya kufika mbele. Kwa aikili ndogo ya BAVICHA wangependa mawaziri hao mizigo watimuliwe bila hata kusikilizwa ambapo ni kinyume na utaratibu, tuwe wapole tuu hatua stahiki zitachukuliwa baada ya wahusika kusikilizwa na kujitetea!
 
Upinzania ateuliwe nani? Mini kabang

Wenye akili hili jambo walishalipuuza wewe umelikomalia jee unatutangazia biashara yako? Bahati mbaya hapa sio mahali pake peleka kule kwenye matangazo madogomadogo utawapata tuu watumiaji. Kila kila la heri aunt Saint Ivuga
 
Last edited by a moderator:
View attachment 126697 View attachment 126698 View attachment 126700 View attachment 126702
Kutoka Kushoto mawaziri, Kawambwa, Kombani, Chiza, Matayo na Ghasia

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) imekutana jana mjini hapa chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, na kuanza kuwahoji mawaziri wanaodaiwa kuwa mzigo kwenye Baraza la Mawaziri.

Kamati hiyo iliyoanza kikao chake majira ya saa 5 asubuhi katika jengo la White House, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ilikuwa na agenda kadhaa, ikiwamo kuu ya kuwajadili mawaziri hao.

Suala la mawaziri hao kuwa mzigo, limekuwa gumzo hasa katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini hapa na kusababisha baadhi ya wabunge kutaka mawaziri hao wachukuliwe hatua.

NIPASHE Jumamosi ilishuhudia baadhi ya mawaziri waliotajwa kuwa mzigo wakiwa katika viwanja vya White House, wakisubiri kuitwa kwa mahojiano.

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. Mathayo David.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

Mawaziri hao waliitwa na Kamati kuu kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kulalamikiwa kuwa utendaji wao ni mbaya.

Mpaka gazeti hili linaenda mitamboni, mawaziri wawili akiwamo Kombani na Kawambwa, walikuwa wameshaitwa na kuhojiwa.

Mapema kabla ya kikao hicho kuanza, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipohojiwa na waandishi kuhusu agenda zitakazojadiliwa kwenye kikao hicho, alisema taarifa kamili zitatolewa leo.

Hata hivyo, NIPASHE Jumamosi ilishuhudia mawaziri hao wawili wakiwa tayari wameshahojiwa wakiwa nje ya ukumbi.

Hivi karibuni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nnauye, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa mawaziri hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania.

Kauli hiyo aliitoa wakati viongozi hao wa chama walipofanya ziara katika mikoa mbalimbali ya kusikiliza kero za wananchi kwa nia ya kukiimarisha chama.

Alionyesha kusikitishwa kwake na kitendo cha mawaziri hao waliopewa dhamana kushindwa kutambua wajibu wao na kueleza kuwa umefika wakati wa wao kuhojiwa na Kamati Kuu ya chama ili wachukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo aibu itarudi kwa chama chake.

Nape alitoa kauli hiyo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakati akielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.

Hisani ya Nipashe

Watanzania kazi yao kuonyeshwa mapichapicha na kukenua meno. Mimi nilifikiri kamati ina ubavu wa kumhoji aliyewateua ni kwa nini hawawajibishi. Kwa hiyo sasa chama kitapendwa kwa kuwa kinawajibisha mawaziri; yani biashara iwe ni kuteuwa wabovu halafu kuweka vikao vya mapichapicha ili chama kipate ujiko. Kwani si kazi ya serikali yao kuteua wanaofaa na kuwawajibisha? sasa hii milolongo ya vikao na machozi ya mamba maana yake nini kama sio kutuchezea karata tatu ili tuliwe kwenye uchaguzi?
 
Nyie endeleeni na vikao timua vyenu, mnadhani CCM wanakurupuka kama Chadema? Kawaida kama kuna issue ni lazima ijadiliwe na cc ili maamuzi yatolewe kwa haki.
 
Wenye akili hili jambo walishalipuuza wewe umelikomalia jee unatutangazia biashara yako? Bahati mbaya hapa sio mahali pake peleka kule kwenye matangazo madogomadogo utawapata tuu watumiaji. Kila kila la heri aunt Saint Ivuga

Bavicha kawaida yenu si matusi.
Mimi mmenikasirisha sana chama kimeshashika moto kwenda ikulu mmekiua ... Mini kabang family akili zenu zipo kwenye masa.
 
Last edited by a moderator:
Bavicha kawaida yenu si matusi.
Mimi mmenikasirisha sana chama kimeshashika moto kwenda ikulu mmekiua ... Mini kabang family akili zenu zipo kwenye masa.

Kwa hiyo mkiambiwa ukweli ni Bavicha? Utamsemaje mtu ni Bavicha bila kujua Ideology yake? Kwa taarifa yako tupo ambao sio Bavicha na hata umri hauturuhusu kuwa huko lakini uji.nga wenu hatuuvumilii maana haujengi zaidi ya kupotosha na kuharibu majadiliano yenye tija.
Tanzania mbovu ya sasa ni mzigo kwa vizazi vijavyo tuwe makini. Imagine taifa lote liwe la watu kama wewe kweli linapaswa kuitwa taifa hilo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom