Mawaziri Mwakyembe, Shonza na CCM mnajifunza nini kutoka kwa Aly Raisman? Wabakaji wanachukiwa dunia nzima

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
Serekali na CCM inawa-treat Babu Seya na Papii kama NATIONAL HEROES.

Wanafanya hivyo bila kuzingatia mateso waliyopitia, na wanayoendelea kupitia, WAHANGA wa matendo machafu na ukatili ya Babu Seya na Papii.

Mh.Mwakyembe, Mh.Shonza, CCM, na wote wanaowatukuza Babu Seya na Papii, wanayo ya kujifunza toka ktk hotuba hizi hapa chini.

Naomba msikilize hotuba ya Aly Raisman aliyoitoa mahakamani dhidi ya Daktari aliyemfanyia vitendo vichafu vya kinyama wakati akiwa mtoto mdogo.

JokaKuu,
Hivi nyie chadema mnakumbuka ahadi mojawapo ya mgombea (aliyekuwa) wa urais Mh Lowassa kuhusu hawa jamaa?
Au ndio gear nyingine ya angani?
Au ndio mkikosa Sera mnaanzisha topic humu ili muanze kuporomoshea watu matusi?
 
..kweli Lowassa alitoa ahadi hiyo.

..lakini kwa maoni yangu ilikosea.

..pia hakueleza atawaachia kwa utaratibu gani.

..naamini hata waliomuunga mkono Lowassa, kimoyo-moyo walikuwa wanaomba asitimize ahadi ya kuwaachia huru wabakaji hawa.

..SEREKALI na CCM wanakosea kuwapokea Babu Seya na Papii Kocha kana kwamba ni Mashujaa wa Taifa hili.

..Wabakaji hawa wameachiwa siku ambayo tulikuwa tunaadhimisha UHURU wa Tanganyika. Kitendo hicho ni sawa na kuitia najisi siku hiyo adhimu.

..Zaidi, wabakaji hao wakapokelewa Ikulu. Baba wa Taifa alituasa kuwa Ikulu ni mahali "patakatifu."

..Kama vile haitoshi, Wizara ya Utamaduni wamejitokeza kuwapa msaada wa kurekodi kazi zao. Je, wizara haikuona wasanii wengine wanaostahili msaada wa serekali kuliko kushughulika na watu waliobaka watoto wa shule?
 
Ungeanzia kwa mkuu wao. Mchungaji akiwaelekeza ng'ombe upande fulani, hakuna anayeuliza, hufuata tu. Ndio hali ilivyo Tz haijalishi una udaktari wa filosofi katika sheria, yote unatupa na kufuata ulaji katika siasa.
 
Hivi nyie chadema mnakumbuka ahadi mojawapo ya mgombea (aliyekuwa) wa urais Mh Lowassa kuhusu hawa jamaa?
Au ndio gear nyingine ya angani?
Au ndio mkikosa Sera mnaanzisha topic humu ili muanze kuporomoshea watu matusi?
Kuahidi sio kutenda. Na uelewe kuwa hakuna anayepinga kusamehewa kwa hao watu, Bali cha kushangaza ni jinsi wanavyo tukuzwa kama vile walitenda mambo mema.
 
Hivi nyie chadema mnakumbuka ahadi mojawapo ya mgombea (aliyekuwa) wa urais Mh Lowassa kuhusu hawa jamaa?
Au ndio gear nyingine ya angani?
Au ndio mkikosa Sera mnaanzisha topic humu ili muanze kuporomoshea watu matusi?
Umeelewa hoja ya mtoa mada!!??

Hoja ni kwanini mnawapraise kama heroes..!??

Yani ni kama vile mmatumia nguvu zote za kiserikali na kichama kuukosoa utawala wa JK uliomuweka ndani...

Na mnapinga maamuzi ya mahakama kuwafunga na judge aliyerule hiyo kesi...

Tukienda mbali zaidi ni sawa na kusema Familia ya Babu Seya haikuwahi baka wala lawiti...ni story tu zilianzishwa.

....ndo nimesema hapo juu...

Akili za masisiem wanazijua maccm yenyeewee....

Sh#t holes...
 
Unajua walifungwa mwaka gani? Au unataka kumaanisha kuwa serikali ya Kikwete 2004 ilikua madarakani.
 
Ni tanzania tu, kama hawakua na makosa basi taratibu za kimahakama zingefuatwa, lakini kwa sasa inavyoonekana ni raisi amewaachia huru wabakaji wa watoto, amewaalika ikuru, kisha yeye na chama chake wana washerehekea hao walawiti. Ni jambo lisilo la kawaida kabisa, hii nchi imejaa ma zombie wanao amini kila story za mitaani bila hata kuchunguza ukweli.
 
JokaKuu,

Hii habari ya Babu Seya siyo ISSUE, and you know it perfectly well na ndio sababu mwaka 2015 kule Jangwani mlishangalia mgombea aliposema atamtoa. Lakini kwa sababu we are investing kwenye petty and cheap politics inaonekana kuna hoja hapa. You can do better.
 
Nawahurumia sana wahanga wa tukio lile ambao hadi leo naamini wanishi na ile shida! Sidhani kama walifanyiwa counseling kuiondoa ile post traumatic disorder wanayoishi nayo hadi leo. Pia siamini kama hawa wahusika wameshawaza kuwaomba msamaha watoto wale badala ya kukimbilia ikulu kusifu. Hata kama hawakufanya (jambo ambalo ni 0%) walitakiwa kuomba msamaha kwa wananchi wote na fans wao.
Ni wakati sasa ccm iachane n awatu hao kwani taswira yao huku nje ina ukungu mwingi tu na ni kama wananchi wanakomolewa hivi na hata idara ya mahakama na polisi na wote waliojishughulisha na kadhia hawajisikii vyema!
 
Back
Top Bottom