Mawaziri matumbo joto

Alichoandika Mwana Siasa, kinakaribiana sana na walichoandika raia mwema, Soma alichoandika Mwana siasa:

Mtanzania, je hakuna uwezekano kuwa Mwanasiasa pia anaweza kuwa anatumia source hiyo hiyo na Raia Mwema?

Au Mwanasiasa anazipata ndani ya Raia Mwema na kuzileta JF, kwani Raia Mwema inachapishwa mara moja kwa wiki lakini habari zao zinakusanywa kila siku?

Au Mwanasiasa ndiyo huyo huyo 'Mwandishi Maalumu' wa Raia Mwema na anamegea kote kote, Raia Mwema na JF (Kama afanyavyo Mwanakijiji na Maggid Mjengwa)

Kusema kuwa Raia Mwema wanamega kutoka JF halafu ndiyo wachapishe gazeti, ina ugumu sana. JF iko very dynamic na magazeti hayawezi ku-keep up nayo.
 
hapana mkubwa mi sishirikiani na mtu yoyote ,wao wapo bongo mi nipo australia nakula masters yangu,so sijui lolote kuhusu hili gazeti na hata magazeti mengineyo unless otherwise hao watu wa raiamwema walichukua habari toka hapa jf,ila si me kushirikiana nao mkubwa
 
Kweli, kwa nafasi ya Waziri kutoka Kagera JK ana wigo mdogo wa Wabunge safi wa Kuwapa Uwaziri au unaibu.
 
Mawaziri matumbo joto

Mwandishi Wetu Novemba 14, 2007
Raia Mwema

MABADILIKO katika Baraza la Mawaziri sasa ni suala la muda tu kwani wakati wowote Rais Jakaya Kikwete atatangaza timu yake mpya, Raia Mwema imefahamishwa.
.

Huenda wakamkumbuka Professor Samwel Wangwe kwenye hili baraza kwa kuwa tayari ni mjumbe wa NEC
 
Kweli, kwa nafasi ya Waziri kutoka Kagera JK ana wigo mdogo wa Wabunge safi wa Kuwapa Uwaziri au unaibu. Hawezi kunteua Kagasheki kwa sababu ni mwizi wa kimataifa na ana tuhuma ya kujibu mbele ya World Interectual Property Organisation (WIPO). Kagasheki na mtoto wa Koffi Annan waliliibia shirika na kura milungula ya kimataifa. Wizi huu unafahamika kimataifa na inashangaza vipi CCM walimruhusu mwizi huyu agombee baada ya kufukuzwa Geneva.

Kwa hapa home, Kagasheki anakabiliwa na kesi ya kutumia udini katika kampeni zake. Hali si shwari na anaweza kutengeliwa ubunge saa yoyote.

mkubwa inaonekana una details za huyu jamaa,kwani ye alikuwaga geneva?na kama alikuwa huko ni kama nani?mana nasikia tu balozi kagasheki ila sijui historia ya ubalozi wake
 
Hawa Madaktari na Maprofessor nilitegemea wawe vinara kweli kweli sasa inaonekana wameover-perform au nini?

JK anataka kutwambia tuchunguze vyeti vyao au nini kinaendelea hapa.

Anyway amefungua vyuo vingi Tanzania, Dodoma University, MUCHs University, Mzumbe University, SUA nk wataweza kujipatia ajira bila matatizo.

Hila kuna mtu mmoja sina uhakika kama atakubaliwa.

kwi kwi kwi kwi,

yaani usisome JF ukiwa kazini na bosi wako yupo around jamani unaweza kupoteza kazi hivihivi.

Wewe Kakindomaster ama kweli wewe ni master... Huyu mtu ambaye hatakubaliwa ninani sasa!

Mimi labda nikusaidia kwa kusema kuwa ni NCHIMBI - mzee wa degree za kununua na kufoji - au nimekosea!
 
Hata hivyo bado hili suala la kupata waziri toka kila mkoa limeanza lini?

Hii nchi jamani na Kikwete huyu kama ni kweli ndio sera yake hii basi inaelekea kuzimu!
 
Hata hivyo bado hili suala la kupata waziri toka kila mkoa limeanza lini?

Hii nchi jamani na Kikwete huyu kama ni kweli ndio sera yake hii basi inaelekea kuzimu!

mwafrika wa kike

Naona hukunielewa hapo awali,nilisema si sheria kuwa rais ateue mawaziri wawili kila mkoa,ana uwezo wa hata wa kuteua wabunge wote wa mkoa mmoja mawaziri,ila nilichosema ni kuwa inaonekana jk katika kuteua baraza lake last year alijaribu na akafanikiwa kutoa atleast kila mkoa uwe na watu wasiopungua wawili ndani ya cabinet yake[/U japokuwa kuna mikoa ina watatu nk .sasa unabisha naomba nieleze ni mkoa gani wa tanzania ambao una watu chini ya wawili ndani ya cabinet ya muungwana?
 
Mwanasiasa,

Sijakubishia chochote maana ulichosema inaonekana ni kweli maana nimekuwa namwandikia Kikwete kumuuliza kwanini ana baraza kubwa sana la mawaziri linalotumia bilioni moja kila mwezi na sijawahi kupata jibu toka kwake au wasemaji wake!

Ulivyosema hapa kuwa ni sera kupata mtu kila mkoa nikaona kama kuna ukweli na ndio maana nikasema kuwa kama hii sera ya JK ingefuatwa na nchi zingine basi kuna nchi zingekuwa na mawaziri zaidi ya elfu mbili hivi.

Siwezi kukubishia maana kujua watu wanatoka mikoa gani kwenye baraza la mawaziri is the last I can do mkuu wangu.

hapa sikubishii wewe ila namshangaa Kikwete kwa kuamua kuwa na baraza kubwa this much ( kwa maelezo yako) ili kuupatia kila mkoa waziri!
 
sasa mkubwa tz devil tukiangalia vizuri unapomkandia huyu bwana mdogo kwa mkoa wa kigoma,mkoa wa kigoma kuna mawaziri wawili,huyu nzanzugwanko na chizze,inasemekana kuwa huyu nzanzugwanko anaweza akaondolewa,so kwa mkoa huo anabakia peter serukamba, mpologomyi , msambya , na kijiko.
msambya tukumbuke alishakuwaga naibu enzi za mkapa kisha akavurunda akatolewa bada ya kuonyesha udhaifu wake katika utendaji

kijiko, huyu ndo hata kueleweka haeleweki,mana hata kumsikia hatumsikii .shortly yupo kama hayupo

mpologomi huyu kama tujuavyo aliboronga akiwa naibu waziri wa fedha enzi za kina mbilinyi na kumfanya apoteze cr

so nadhani aliyebaki kwa mkoa huo ni serukamba na chizze ambaye hivi sasa yumo ndani ya cabinet ya sasa

Msambya alishindwa uchaguzi ndiyo maana mnene akamtosa na kumpa Ukuu wa Wilaya. Ila JK akimpa Peter Uwaziri kwasababu ulizozitoa, nitaamini kweli Tanzania kichwa cha mwendawazimu na serikali ya Kikwete haito acomplish kitu chochote.
 
ila ndugu yangu mwafrika kwa kutumia utashi wako unadhani katika hao 10 waliotajwa wataondolewa,unadhani nani wataondoka na wakina nani wataingizwa?
 
sasa unadhani ni nani mwengine kwenye mkoa huo anaweza akapewa?sana sana labda awarudishe hao hao wakina msambya ambao ni watu waliokwishaboronga toka long time
 
sasa unadhani ni nani mwengine kwenye mkoa huo anaweza akapewa?sana sana labda awarudishe hao hao wakina msambya ambao ni watu waliokwishaboronga toka long time

Awape watu kutokana na uwezo wao wa kufanya kazi, na wala siyo mikoa waliyotoka. Kama sikukosea bado ana nafasi kama saba za wabunge wa kuteuliwa. Azitumie hizi nafasi kuteua watendaji wenye sifa ili awape uwaziri badala ya kuendelea kutuingizia usiku na watu kama akina Peter. Wakati muhimu mkuu...
 
Tz, anazo nafasi mbili tu kwenye kuteua.. halafu miye sitaki maprofesa na hawa watu wenye CVs ndeeeefu wawe mawaziri (labda Ukatibu Mkuu). Upande wa mawaziri tunahitaji breed ya watu wanaoitwa Viongozi ambao CVs zao zimejaa "uongozi"!!! Haya ya kuamini kuwa maprofesa ndio watatuokoa kutoka katika shimo walilolichimba wenyewe ni njozi za Alinacha!
 
Mkjj, ahsante kwa kunisahihisha. Halafu sina uhakika ni utaratibu gani hutumika kuwateua hawa mawaziri? Maanake kila mtu ana theory yake.
 
ila ndugu yangu mwafrika kwa kutumia utashi wako unadhani katika hao 10 waliotajwa wataondolewa,unadhani nani wataondoka na wakina nani wataingizwa?

Mwanasiasa,

Hivi kwani sasa hivi ni saa ngapi huko Australia mkuu? Ninaogopa nisikusababishe ukashindwa kulala kwa mambo yangu ambayo mengi hayamaliziki mapema! lol

Kwa kweli mimi inabidi niwe the last person kuulizwa kuhusu suala la nani awe waziri na nani asiwe waziri. Nimeandika sana ikulu na maswali mengi na ushauri kibao toka kwa memba na non membaz wa JF ila naona JK hasikilizi yeyote asiye kwenye huo mtandao wake.

Jambo moja ninaloweza kujibu kwa hakika ni kuwa mimi napinga suala la kuwa na lundo la mawaziri bila sababu ya maana (I dont buy the kila mkoa uwe na waziri thing).

Thanks!
 
Hawa raia mwema hii habari wameitoa JF. Rudieni ujumbe wa Mwana siasa unafanana sana na kilichoandikwa hapa.

Si ajabu hawa nao hawana za jikoni, na badala yake jiko lao ni JF

Ndugu Mtanzania,

Tusisahau kwamba Salva pale Ikulu ni mtu wao...wanasema wana chanzo credible pale. The fact kwamba yaliyosemwa humu JF yanafanana na yaliyoandikwa na Raiamwema, inawezekana ni kuwa ya kweli yote ndiyo maana maelezo yanafanana. Kama chanzo cha JF kilipata taarifa Ikulu, na kama taarifa ya Raiamwema pia ilitoka ikulu, basi ndiyo maana taarifa zinafanana...mnaonaje wakuu?
 
Mkjj, ahsante kwa kunisahihisha. Halafu sina uhakika ni utaratibu gani hutumika kuwateua hawa mawaziri? Maanake kila mtu ana theory yake.

hakuna utaratibu wa kisheria wa kuteua mawaziri (ukiondoa Waziri Mkuu) zaidi ya kuwa ni lazima wawe wabunge. Waziri Mkuu atachaguliwa kutoka chama chenye wabunge wengi Bungeni na ni lazima awe Mbunge wa kuchaguliwa. Mawaziri ni lazima wawe wabunge lakini siyo lazima wawe Wabunge wa kuchaguliwa. Haya mengine ya mikoa, rangi, urefu, ufupi, weupe au weusi ni mapenzi ya Rais mwenyewe!
 
Ndugu Mtanzania,

Tusisahau kwamba Salva pale Ikulu ni mtu wao...wanasema wana chanzo credible pale. The fact kwamba yaliyosemwa humu JF yanafanana na yaliyoandikwa na Raiamwema, inawezekana ni kuwa ya kweli yote ndiyo maana maelezo yanafanana. Kama chanzo cha JF kilipata taarifa Ikulu, na kama taarifa ya Raiamwema pia ilitoka ikulu, basi ndiyo maana taarifa zinafanana...mnaonaje wakuu?

Hawa akina Ulimwengu and co wako kwenye duru za uhandishi siku nyingi sidhani kama wanaweza kukosa credible sources kutoka Ikulu mpaka wakaja kunyofoa discussion hapa.

Alafu nilikuwa nafikiria one of their sources ni Salva.
 
Icadon, don't count on it... hivi unafikiri Salva ana uhusiano mzuri kiasi hicho baada ya yaliyotokea kule Rai?
 
Back
Top Bottom