BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
Mawaziri matumbo joto
Mwandishi Wetu Novemba 14, 2007
Raia Mwema
MABADILIKO katika Baraza la Mawaziri sasa ni suala la muda tu kwani wakati wowote Rais Jakaya Kikwete atatangaza timu yake mpya, Raia Mwema imefahamishwa.
Habari zilizothibitishwa na vyanzo vya habari ndani ya Serikali zinaeleza kwamba tayari waraka maalumu wa uamuzi huo, uko mezani kwa Rais Kikwete, kabla ya kuuweka bayana wakati wowote kuanzia leo.
Habari za hivi karibuni zinataja kuachwa kwa mawaziri saba na manaibu waziri watano huku wakiingizwa wengine ambao wanatokana kwa kiasi kikubwa na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa CCM uliomalizika karibuni, Kizota, Dodoma.
Hatua hiyo inaelezwa kwenda sambamba na hali ya kisiasa na kiutendaji miongoni mwa wasaidizi hao, ambao amekua akiwapima kwa kipindi chote alichowapa madaraka na kuwapa nguvu ya kufanya maamuzi mazito.
Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanasema huenda Kikwete akapata upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake ambao wanatajwa kuwa na nguvu kubwa ndani na nje ya mfumo rasmi wa uongozi wa chama na Serikali.
Hata hivyo, matokeo ya mwisho wa uchaguzi ndani ya CCM na hata kitendo cha Kikwete kupinga waziwazi vitendo vya rushwa, vinaelezwa kuwa vinakwenda sawa na haiba yake halisi ya kuwa mtu ambaye asingependa mambo yaendelee kuwa ya hovyo.
Amekua mkimya mno na alikwisha kutoa muda kwa wala rushwa ambao alisema wazi kwamba anawafahamu, na uamuzi wa kupiga vita rushwa ndani ya CCM ni uamuzi mzito ambao kwa wengi tuliona kama anaongeza maadui zaidi kuliko marafiki ndani ya chama, lakini amefurahisha wengi ndani na nje ya chama, alisema kiongozi mmoja wa juu wa CCM.
Uteuzi wa Pius Msekwa kuwa Makamu Mwenyekiti wake Bara na kuingiza sura mpya ndani ya Sekretarieti ya chama hicho huku akimuacha Katibu Mkuu, Yussuf Makamba, kwa Bara na kuacha watendaji wote wa Visiwani, kumeelezwa kama alama za nyakati ambazo watendaji wa Serikali wanapaswa kuzisoma.
Pamoja na kuwa ni jarida hili pekee lililomtaja Msekwa kuwa mmoja wa waliokuwa wakitajwa kuwa wasaidizi wa Kikwete ndani ya CCM, bado uteuzi wake umekua wa kushitukiza kwa wengi hali ambayo huenda ikajitokeza katika mabadiliko anayotarajia kuyafanya ndani ya Serikali pia.
Ofisa mwandamizi wa Ikulu, ameiambia Raia Mwema kwamba Rais Kikwete amechelewesha mabadiliko hayo ambayo yamekuwa yakisubiriwa sana kutokana na msiba wa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia, kinyume cha maelezo ya wengi kwamba msiba huo ndio utakaomsukuma Rais kufanya mabadiliko.
Ni kweli suala hilo liko mezani kwa Rais lakini aliona si vyema kwa wakati ule kutangaza kutokana na familia ya marehemu Mbatia kuwa katika msiba, lakini sasa nadhani wakati wowote atakaoona unafaa atatangaza anachokusudia kukifanya, alisema ofisa huyo wa Ikulu, ambaye alisema hana mamlaka ya kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.
Wanaotajwa kuwamo katika timu hiyo mpya ni pamoja Mbunge wa Siha, Aggrey Mwanri, ambaye ameondolewa katika nafasi ya ukatibu uenezi wa CCM na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.
Wengine ni rafiki wa karibu wa Rais Kikwete na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ambaye naye ameondoka kwenye Uweka Hazina wa CCM na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Amos Makala.
Baada ya kutangaza Baraza jipya la Mawaziri, Serikali ya Rais Kikwete, imekabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na zile zilizosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kudura za Mwenyezi Mungu na changamoto nyingine zilizosababishwa na udhaifu wa watendaji na hali ya kiuchumi.
Ukame ulioikumba nchi ulisababisha tatizo kubwa la nishati ya umeme, hali ambayo ilisababisha Serikali kuingia mkataba wa haraka haraka uliozua utata mkubwa na kampuni ya Richmond Development ya Marekani, kampuni ambayo pamoja na kuuza mkataba wake kwa kampuni nyingine ya Dowans, ilishindwa kuzalisha umeme kwa wakati kulingana na mkataba.
Uamuzi huo ulizua malalamiko na katika mabadiliko yake ya kwanza Kikwete alimuondoa katika Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha aliyehamishiwa Wizara ya Afrika Mashariki, hatua ambayo ilionekana kama kufunika kombe mwanaharamu apite kwani mengi yameibuka baada ya hapo.
Changamoto nyingine kwa Rais Kikwete ni sakata la wanafunzi wa elimu ya juu ndani na nje ya nchi, ambao kwa wale wa ndani wamekua wakiandamana kuelekea ofisi za Bodi ya Mikopo na waliko nje ya nchi kuhangaika huku wengine wakirudishwa nyumbani baada ya kudhalilishwa kwa muda mrefu, huku Waziri wake Profesa Peter Msola, akitoa maelezo ya kujikanganya.
Hivi karibuni sekta ya madini imeibua mjadala mkubwa zaidi baada ya kuwapo kwa hoja ya kusainiwa kinyemela kwa mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, uliosainiwa London, Uingereza, na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, huku kukiwa na maswali mengi zaidi yasiyo na majibu.
Changamoto hizo na zile zilizotokana na mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM na udhaifu katika maeneo mbalimbali serikalini, yanaelezwa kuwa msingi mkuu wa mabadiliko ambayo wananchi wengi wanatarajia Rais Kikwete atayafanyia marekebisho, pamoja na kuwapo taarifa kwamba maeneo hayo hayataguswa katika mabadiliko ya hivi karibuni.
Katika nafasi ya Salome Mbatia wanatajwa wanawake wengi ambao bado kwa hakika hakuna chanzo kilichokua na angalao hakika ya majina matatu ya wanaoweza kutoka atakayeziba nafasi hiyo.
Pamoja na taarifa za mabadiliko hayo kugusa hisia za Watanzania wengi, bado Rais Kikwete, ana mtihani mgumu wa kufanya uamuzi utakaorudisha imani ya wananchi kwa Serikali yake, ikizingatiwa kwamba baadhi ya wanaoguswa wako karibu yake.