Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

Mwandishi Wetu Machi 26, 2008
Raia Mwema


SERIKALI inakamilisha taratibu za kuwashitaki mawaziri wa zamani wawili wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Raia Mwema imefahamishwa.

Habari za uhakika zilizopatikana na kuthibitishwa na maofisa waandamizi wa Serikali zinaeleza kwamba mawaziri hao (majina tunayo) walihojiwa na vyombo vya dola kwa mara kadhaa na sasa mchakato wa kuwashitaki uko katika hatua za mwisho.

Wote wawili walipata kuongoza Wizara ya Fedha, chini ya utawala wa Rais Benjamin Mkapa na mmoja aliteuliwa katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete kabla ya kuachwa katika mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni.

Kwa mujibu wa habari hizo, mmoja amekuwa akichunguzwa kufanya maamuzi kadhaa yenye utata, ikiwamo kutoa misamaha ya kodi ambayo kisheria hakuwa na mamlaka nayo akiwa anatuhumiwa kuvuka mipaka ya mamlaka yake katika kutoa misamaha.

Mwingine anaelezwa kuchunguzwa kuhusika na maamuzi kadhaa akiwa Waziri katika Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, lakini haikuweza kufahamika mara moja ni eneo gani hasa ambalo mwanasiasa huyo mstaafu amechunguzwa.

Mawaziri wote wawili wanatajwa sana kuwa karibu na Mkapa katika masuala kadhaa ya kiutendaji na hata katika masuala kadhaa binafsi na inaelezwa kwamba baadhi ya mambo yaliyochunguzwa yanaweza kumgusa moja kwa moja Rais huyo mstaafu.

Mkapa anatajwa kuhusika moja kwa moja na mradi mkubwa wa mkaa wa mawe wa Kiwira, akiwa na maslahi binafsi katika kampuni ya Tanpower Resources, ambayo iliuziwa hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Limited iliyokuwa ikimilikiwa na serikali kabla ya ubinafsishaji.

Pamoja na Mkapa kutajwa katika maeneo mengi, bado kumekuwa na maelezo ya kutaka “aachwe apumzike”, huku baadhi wakitumia kinga ya kikatiba ambayo rais mstaafu anakuwa nayo pamoja na kupingwa na baadhi ya wanasheria.

Haikuweza kufahamika mara moja mawaziri hao walichunguzwa katika maeneo gani mengine zaidi lakini kuna uhakika kwamba uchunguzi huo uligusa pia misamaha ya kodi iliyofanywa katika kipindi mawaziri hao wakiwa madarakani.

Miongoni mwa mambo ambayo yaliguswa ni mkataba kati ya Serikali na wakaguzi wa Alex Stewarts waliokuwa wakifanya ukaguzi wa mapato katika sekta ya madini.

Eneo jingine tata ambalo linatajwa kuguswa ni mkataba wa Serikali na kampuni ya Tanzania International ContainerTerminal (TICTS) wa kukodisha eneo la bandari ya Dar es Salaam, mkataba ambao hadi sasa umekuwa ukipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa sekta ya bandari.

Hata hivyo, mawaziri wote wawili walikuwa ama na mahusiano ya karibu na Mkapa kikazi na hata kibinafsi mambo ambayo yanazidi kuonyesha ni jinsi gani Serikali italazimika kumtaja ama kumgusa rais huyo mstaafu katika uchunguzi na hatimaye mashitaka.

Ikiwa wanasiasa hao watafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Kikwete kuwashitaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, akituhumiwa kuiibia Serikali Sh bilioni 2 kutokana na ununuzi wa jengo la ubalozi, Rome.

Hata hivyo, kiu kubwa ya Watanzania kwa sasa iko kwa watu wanaotajwa kuhusika katika upotevu wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika na mradi tata wa umeme wa dharura wa Richmond Development LLC.

Pamoja na Rais Kikwete kuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, kulikuwa na kazi iliyokwisha kuanza kufanywa na vyombo hivyo ndani ya BoT na maeneo mengine nyeti kiuchumi.
 
Naona hapo ni Yona na Mramba

Wanatolewa kafara? Kama wameahamua inabidi waunganishwe wote hata Richmond.na ikibidi sasa Mzee aliyestahafu siasa inatakiwa atoe neno. Ikibidi huko huko Butiama zile mali alizojibinafusisha/jichukulia azirudishe tu ili kulinda heshima yake.
 
Back
Top Bottom