Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 26, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

  Mwandishi Wetu Machi 26, 2008
  Raia Mwema


  SERIKALI inakamilisha taratibu za kuwashitaki mawaziri wa zamani wawili wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Raia Mwema imefahamishwa.

  Habari za uhakika zilizopatikana na kuthibitishwa na maofisa waandamizi wa Serikali zinaeleza kwamba mawaziri hao (majina tunayo) walihojiwa na vyombo vya dola kwa mara kadhaa na sasa mchakato wa kuwashitaki uko katika hatua za mwisho.

  Wote wawili walipata kuongoza Wizara ya Fedha, chini ya utawala wa Rais Benjamin Mkapa na mmoja aliteuliwa katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete kabla ya kuachwa katika mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mmoja amekuwa akichunguzwa kufanya maamuzi kadhaa yenye utata, ikiwamo kutoa misamaha ya kodi ambayo kisheria hakuwa na mamlaka nayo akiwa anatuhumiwa kuvuka mipaka ya mamlaka yake katika kutoa misamaha.

  Mwingine anaelezwa kuchunguzwa kuhusika na maamuzi kadhaa akiwa Waziri katika Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, lakini haikuweza kufahamika mara moja ni eneo gani hasa ambalo mwanasiasa huyo mstaafu amechunguzwa.

  Mawaziri wote wawili wanatajwa sana kuwa karibu na Mkapa katika masuala kadhaa ya kiutendaji na hata katika masuala kadhaa binafsi na inaelezwa kwamba baadhi ya mambo yaliyochunguzwa yanaweza kumgusa moja kwa moja Rais huyo mstaafu.

  Mkapa anatajwa kuhusika moja kwa moja na mradi mkubwa wa mkaa wa mawe wa Kiwira, akiwa na maslahi binafsi katika kampuni ya Tanpower Resources, ambayo iliuziwa hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Limited iliyokuwa ikimilikiwa na serikali kabla ya ubinafsishaji.

  Pamoja na Mkapa kutajwa katika maeneo mengi, bado kumekuwa na maelezo ya kutaka “aachwe apumzike”, huku baadhi wakitumia kinga ya kikatiba ambayo rais mstaafu anakuwa nayo pamoja na kupingwa na baadhi ya wanasheria.

  Haikuweza kufahamika mara moja mawaziri hao walichunguzwa katika maeneo gani mengine zaidi lakini kuna uhakika kwamba uchunguzi huo uligusa pia misamaha ya kodi iliyofanywa katika kipindi mawaziri hao wakiwa madarakani.

  Miongoni mwa mambo ambayo yaliguswa ni mkataba kati ya Serikali na wakaguzi wa Alex Stewarts waliokuwa wakifanya ukaguzi wa mapato katika sekta ya madini.

  Eneo jingine tata ambalo linatajwa kuguswa ni mkataba wa Serikali na kampuni ya Tanzania International ContainerTerminal (TICTS) wa kukodisha eneo la bandari ya Dar es Salaam, mkataba ambao hadi sasa umekuwa ukipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa sekta ya bandari.

  Hata hivyo, mawaziri wote wawili walikuwa ama na mahusiano ya karibu na Mkapa kikazi na hata kibinafsi mambo ambayo yanazidi kuonyesha ni jinsi gani Serikali italazimika kumtaja ama kumgusa rais huyo mstaafu katika uchunguzi na hatimaye mashitaka.

  Ikiwa wanasiasa hao watafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Kikwete kuwashitaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, akituhumiwa kuiibia Serikali Sh bilioni 2 kutokana na ununuzi wa jengo la ubalozi, Rome.

  Hata hivyo, kiu kubwa ya Watanzania kwa sasa iko kwa watu wanaotajwa kuhusika katika upotevu wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika na mradi tata wa umeme wa dharura wa Richmond Development LLC.

  Pamoja na Rais Kikwete kuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, kulikuwa na kazi iliyokwisha kuanza kufanywa na vyombo hivyo ndani ya BoT na maeneo mengine nyeti kiuchumi.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Mar 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Maneno Mengi Hayavunji Mfupa
   
 3. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mkuu sijakuelewa unamaanisha nini?
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Naona hapo ni Yona na Mramba
   
 5. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wanatolewa kafara? Kama wameahamua inabidi waunganishwe wote hata Richmond.na ikibidi sasa Mzee aliyestahafu siasa inatakiwa atoe neno. Ikibidi huko huko Butiama zile mali alizojibinafusisha/jichukulia azirudishe tu ili kulinda heshima yake.
   
 6. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sijui kama hii ndoto inawezekana hata siku moja
  utawashitaki vipi hao mawaziri waliokuwa wahusika wakuu wa Mkapa, na Mkapa ni muhusika mkuu, then yeye umuache jamani?
  Kuna kauzibe Kikwete anafanya kwa Mkapa, 'eti Muacheni mzee wa watu apumzike'Haya ni maneno ya Raisi wetu angali anajua kuwa Mkapa kaliibia Taifa na kusababisha matatizo kibao kwa Taifa na wananchi wake.
  Sijui kama hili linalozungumziwa hapa linawezekana kwa serikali hii, ambayo viongozi wote ni Mafisadi hata wasio na uchungu na nchi yetu.
   
Loading...