Mawaziri kukosoa muswada wa madini ni nguvu za demokrasia au | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri kukosoa muswada wa madini ni nguvu za demokrasia au

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msongoru, Apr 20, 2010.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  TUKIO la mawaziri wawili ambao ni Stephen Wassira, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, na Ezekiel Maige, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kuungana na wadau mbalimbali kupinga muswada wa madini limepokelewa kwa hisia tofauti.

  Tunasema kwamba hatua ya mawaziri hawa kuukataa muswada huo ni katika hali isiyo kawaida kwa kuwa tunaamini muswada wa sheria ya madini tayari ulikwishajadiliwa na Baraza la Mawaziri na kwamba kile kilichomo ndani ndicho walikubaliana.

  Kwa upande mwingine, tunaona hatua ya mawaziri hao kuupinga kasoro zilizoko kwenye muswada huo hadharani ni hatua muhimu katika kukuza demokrasia ambapo kila mtu anakuwa huru kutoa maoni kwa mujibu wa sheria.

  Kwa mantiki hiyo tunaweza kusema ukomavu wa demokrasia nchini umefikia hatua ya mawaziri kuweka kando ule utaratibu wao wa uwajibikaji wa pamoja na kutetea maslahi ya Watanzania. Kwa hatua hiyo tunaweza kuwapongeza.

  Kutokana na mawaziri hawa na wadau wengine wa sekta ya madini kugundua katika muswada wa sheria ya madini kuna kasoro, ni vema wabunge ambao ndio wana jukumu la kuichambua na kisha kuipitisha sheria hiyo wakawa waangalifu kwa maslahi ya Watanzania wote.

  Tunasema hivyo kwa sababu hoja nyingine ambazo zimejadiliwa katika mkutano wa wadau wa madini na Waziri mwenye dhamana, William Ngeleja zinadai kuwa muswada huo umejaa mapungufu makubwa na unalenga kunufaisha wachimbaji wakubwa na kuacha wadogo wakitaabika.

  Ndio maana nasi wa Mwananchi tunaungana na wadau ambao walishauri muswada huo ufanyiwe marekebisho kabla ya kuwasilishwa bungeni kwa mjadala ili ulenge kumsaidia mchimbaji mdogo.

  Tunatambua umuhimu wa muswada huu, lakini vilevile tusingependa upitishwe alafu kasoro hizi zije kuleta dosari siku zijazo

  Mwananchi.
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Sasa hatujui nani alitumwa na Bosi wao JK...kawaida huwa wana kitu inaitwa collective responsibility
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wala tusidanganyike na hakuna sababu yoyote ya kuwapongeza hao mawaziri. Kabla ya muswada wa Madini kufika Bungeni suala la madini limewahi kujadiliwa sana bungeni na nje ya Bunge lakini hakuna Waziri yoyote aliyewahi kujitokeza kukubaliana na watoa hoja kwamba nchi inafilisiwa na madini yetu yanateketea kutokana na kukumbatia wawekezaji wanyonyaji chini ya mikataba mibovu. Wala hakuna suala la kuweka kando uwajibikaji wa pamoja ama kutetea maslahi ya wananchi. Wakati wote uliopita kwa nini hatujawahi kuwasikia wakifanya hivyo?

  Huu ni mwaka wa uchaguzi, kila anayefikiria kuwania uongozi anatafuta agenda itakayomfanya asikike na akubalike kwa wananchi. Hizo ni mbinu tu za kujitafutia credit na kumendea kura za wananchi. Inakera na inakasirisha kuona viongozi wanasubiri mpaka wakati wa uchaguzi ndipo wanakuja na 'mawazo mapya' kama vile wanakurupuka toka usingizini!
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  na lazima walijadili na kupitisha katika baraza la mawaziri....kabla ya kuwa muswada
   
 5. M

  Msavila JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mawaziri hawa wanastahili kuwajibishwa kama kweli walihudhuria vikao vya Baraza la Mawaziri kama ilivyokuwa kwa Mrema. Hili si swala la kukua kwa demokrasia hata kidogo vinginevyo demokrasia ya namna hii itazaa mijadala isiyokwisha na upotezaji wa muda.
  Kama wanataka kura za Oktoba watafute njia nyingine mbadala. Mbunge/Mwkilishi wa aina hii hawezi kuwakilisha bungeni mawazo ya wapiga kura wake kama yanakinzana na mtizamo wake!!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Dawa mawaziri wasiwe wabunge....ndipo watakapowajibika vizuri....mbona madiwani sio watendaji kwenye halmashauri?
   
Loading...