Mawaziri ambao hawata kuwa kwenye baraza jipya la mawaziri tuwafanye hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri ambao hawata kuwa kwenye baraza jipya la mawaziri tuwafanye hivi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichwa Ngumu, Apr 28, 2012.

 1. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  JF
  Binafsi nafarijika sana kuona mbunge wangu ambaye nimemwamini na kumpa kura yangu na baadae nagundua kuwa raisi wa nchi nae anamwamini hivyo hivyo na hata kuamua kumpa uwaziri; na sijisikii vizuri kuona mbunge ambae nilimwamini na akapewa uwaziri kavurunda katika utendaji kazi wake na hata ikafikia raisi aliye mteua kuwa waziri hamuitaji tena katika baraza lake la mawaziri kwa sababu ya utendaji kazi wake.
  najiuliza kama imethibishwa na CAG, kamati za bunge, Bunge na rais wa nchi kuwa sio mwadilifu, sio mtendaji mzuri, hafai, mwizi, fisadi.

  Je, sisi wananchi tuliomchagua kuwa mbunge katika jimbo letu ndio anatufaa?
  kama mbunge ni sehemu ya baraza la madiwani katika jimbo.
  Je, hataendeleza ufisadi wake katika kwenye halimashauri?

  Nashauri/napendekeza wanachi kupitia JF tuangalie utaratibu wa kuwavua na ubunge ili wasipate nafasi ya kuendeleza ufisadi wao.

  Wanasheria mtaliweka vizuri; katiba mpya iseme waziri atakaye jihuzuru au kuondolewa kwenye baraza la mawaziri kwa uzembe, wizi, ufisadi au tuhumu yoyote kinyume na maadili yake ya kazi basi aachie ngazi zote alizonazo katika utumishi wa uma.

  karibuni
   
Loading...