Mawaziri Aisha Kigoda na Seif Khatibu watangaza penzi lao Bungeni

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Naibu waziri wa Afya Aisha kigoda amezima minongono ya muda mrefu ,baada ya kuamua kuweka wazi Bungeni kuwa waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano mhe Seif khatib ndiye barafu wa moyo wake

Mmambo yalikuwa hivi:

Mwenyekiti wa Bunge mh Job Ndugai alimwita naibu waziri, Dr kigoda kuchangia kwa dakika 20 kabla ya waziri wake prof mwakyusa kupewa nafasi ya kuhitimisha hoja hiyo

Baada ya kusimama, Dr Kigoda alianza kumshukuru Rais JK kwa kumwamini na kumteua kushikilia wadhifa alionao, alimshukuru bosi wake professor Mwakyusa kwa ushirikiano anaompa kazini pia akawashukuru wafanyakazi wenzake.

Naibu waziri huyo akamalizia kwa kumshukuru mpenzi wake Mhe Seif khatib ndiye barafu wa moyo wake
 
Ingekuwa hivyo kwa wabunge wote kufanya hivyo basi wachache wangebaki single mjengoni
 
Naibu waziri wa Afya Aisha kigoda amezima minongono ya muda mrefu ,baada ya kuamua kuweka wazi Bungeni kuwa waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano mhe Seif khatib ndiye barafu wa moyo wake

mambo yalikuwa hivi
Mwenyekiti wa Bunge mh job Ndugai alimwita naibu waziri, Dr kigoda kuchangia kwa dakika 20 kabla ya waziri wake prof mwakyusa kupewa nafasi ya kuhitimisha hoja hiyo
Baada ya kusimama, Dr kigoda alianza kumshukuru Rais jk kwa kumwamini na kumteua kushikilia wadhifa alionao, alimshukuru bosi wake profesor mwakysa kwa ushirikiano anaompa kazini pia akawashukuru wafanyakazi wnzake
Naibu waziri huyo akamalizia kwa kumshukuru mpenzi wake Mhe Seif khatib ndiye barafu wa moyo wake

Mi naona ni bomba tu!

Wanaonyesha mfano bora kwamba hata katika umri ule, mambo bado ni motomoto!

Amini usiamini, kauli njema humtoa nyoka pangoni, huenda jioni yake wale watu wameenda kufurahia sana unyumba wao na kujikumbusha ujana wao!
 
Huwa najiuliza haya mahusiano ya ndani kati ya wabunge na mawaziri
kama yana uhusiano wowote na utawala bora , RUSHWA PAMOJA NA MAOVU
MENGINE YANAYOENDELEA NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO
 
By the way, Aisha Kigoda si Doctor, hiyo heshima ameigushi tu! Aisha ni Medical Assistant! Kwa watu makini kama JF na pia Bungeni kumtambua Aisha kama Dr. ni ufisadi wa kielimu ambao ndio unaua professionalism nakuacha nchi ikiendeshwa kimazoea! Bungeni wapo Ma-Dr. wengi ambao wakichunguzwa watajulikana pia ni Feki!
 
Jamaa wameamua kudumisha MUUNGANO,kwa staili ya aina yake.Kwa staili hii utabiri wa sheikh Yahya unaweza kutimia.ONGERENI SANA.Msiishie hapo na ndoa mtutangazie tuje tutupe roho maana Tanga na Zanzibar,hapo si kurusha roho tena bali itakuwa kuitupa kabisa.
 
By the way, Aisha Kigoda si Doctor, hiyo heshima ameigushi tu! Aisha ni Medical Assistant! Kwa watu makini kama JF na pia Bungeni kumtambua Aisha kama Dr. ni ufisadi wa kielimu ambao ndio unaua professionalism nakuacha nchi ikiendeshwa kimazoea! Bungeni wapo Ma-Dr. wengi ambao wakichunguzwa watajulikana pia ni Feki!

Zed,

Acha roho mbaya hiyo. Je una uhakika na unachokinena?

Bi Aisha ni Assistant Medical Officer ( AMO)na alifanya kozi hii mara baada ya kumaliza Medical Assistant pale Tanga. Na kwa mujibu wa sheria za Tanzania watu hao wanatambuliwa kama madaktari.

Soma profile yake kwenye tovuti ya bunge
 
Hata watu wazima jamani, kuna vitu wavipendavyoooo!! Naampa hongera sana Dr. Aisha Kigoda kwa kuwa muwazi na mkweli kuhusu mapenzi na Waziri mwenzake.... Mapenzi ya kweli hayatakiwi kujificha jamani. Tuige mfano huu wale wanaojificha kama nanihii!!!!!!!!!!
 
Huyo ni muwazi lakini kina mama wengine hapo ndani ya mjumba wana ATM zaidi ya tatu ingewezekana kila mbunge angereijsta mpenzi wake kwa siri wangeweza kuwa na adabu.
 
Back
Top Bottom